Nimshauri vipi?

Nimshauri vipi?

Inafungiwa wapi hiyo ndoa nikaweke pingamizi la haki?

Hivi Joseph hebu geuza picha iwe rafikiyo ndo nafanyiwa haya; achana na hiyo iwe ndio wewe ama mdogo wako ama kaka yako ama yeyote anayekuhusu!

Piga picha halafu uone unyama unaoshiriki kumfanyia binadamu mwenzio haki yanai LAANA na iko juu yenu nyote hata kama itawachukua 50 yrs am telling you MUNGU HAJARIBIWI hivyo hata siku moja!
Mimi sijashiriki katika hili na hivyo Mungu hatanihukumu bali rafiki yangu alikuja omba ushauri juu ya hili na nikaona niliweke hapa ili tumshauri la kufanya maana si jambo dogo na hata mimi linaniogopesha ndio maana sikuweza kumshauri kwa haraka nini cha kufanya.
Jambo la msingi alilotaka kujua ni, je mtoto akizaliwa atakuwa na haki ya kumpata akimtaka?
 
kwa nini asubiri huyo dada akajifungulie kwamwanaume mwenziye na ndipo atafute mtoto kuwa naye?
jambo la msingi mi nadhani hiyo ndoa angepinga tu, ujue si vibaya kupinga ndoa kibinadamu,
hata walipoweka hiyo taratibu hawakufanya makosa, vipi utakapoanza msala baadaye wa kudaiana mtoto?
mala wa kwangu mala si wako, ni heri ijulikane moja tu busara itumike hapo, kama kweli anajua kuwa mimba si ya muoaji bora aahirishe hiyo ndoa, maana ni laana kubwa sana mbele za Mungu
hata katika jamii inayokuzunguka ni sawa na kufuga majini, wakati wenziyo wanayapiga vita
 
Inafungiwa wapi hiyo ndoa nikaweke pingamizi la haki?

Hivi Joseph hebu geuza picha iwe rafikiyo ndo nafanyiwa haya; achana na hiyo iwe ndio wewe ama mdogo wako ama kaka yako ama yeyote anayekuhusu!

Piga picha halafu uone unyama unaoshiriki kumfanyia binadamu mwenzio haki yanai LAANA na iko juu yenu nyote hata kama itawachukua 50 yrs am telling you MUNGU HAJARIBIWI hivyo hata siku moja!
Mimi sihusiki na hivyo dhambi sitoipata,nilichokifanya ni kuomba ushauri kwa niaba ya rafiki yangu ambaye anataka kujua tu kuwa, mtoto akizaliwa yeye atakuwa na hai ya kumpata akitaka?Ndoa sijui inafanyika wapi ila send off najua ingawa nipo sehemu nyingine tofauti na walipo.
 
hilo tatizo ni zito sana na suluhisho lake ni kuweka pingamizi katika hiyo ndoa zaidi ya hapo huyo rafiki yako afunge bakuli (domo) lake milele na hasije kuja kusema kuwa mtoto ni wake wala kuendeleza mahusiano na mawasiliano na huyo binti

Akienda kinyume na hivi navyoandika ataleta majuto makubwa sana hapa duniani kwa hao wanandoa na mtoto
 
Huyo binti ameshabinafisisha akili na utu wake kwa kuendekeza ngono. Hafikirii in long terms. Mawazo yake ni leo tu, haangalii kesho.
 
rafiki yako anatakiwa apinge hiyo ndoa asipofanya hivyo basi afungu mdomo wake la sivyo

  1. atajidhalilisha yeye mwenyewe na kujitia aibu kuwa ni mume ***** ambaye kalelewa mimba na mume mwenzie
  2. atakudhalilisha wewe kwa kuwa rafiki wa karibu kuwa ulishindwa kumshauri 1.
  3. atamdhalilisha huyo mp[enziwe wakati bado anampenda
  4. ataidhalilisha familia ya huyo mpuuzi mwanamke
  5. atajenga uadui ambao ni ngumu kufutika

Huyo binti ameshabinafisisha akili na utu wake kwa kuendekeza ngono. Hafikirii in long terms. Mawazo yake ni leo tu, haangalii kesho.
 
huu ushauri utamfaa huyo ndugu
Jana (31/7/10) nilihudhuria ibada takatifu ya ndoa ya RC. Padre alichonga mno! Kawaambia kwa dhati kabisa wanandoa wapya na wa zamani kuwa ndoa si kitu rahisi. Wasifikirie wanaingia kwenye mteremko bali kwenye maisha ya kuvumiliana. Kwamba ukweli, kuheshimiana na kuaminiana katika yote hasa katika KUJAMIIANA. Pia kazi kubwa ya wanandoa ni kutakatifuzana ili mwisho wa siku kila mmoja aione pepo na si kukwazana kama ilivyo sasa. Tatizo siku zote litabaki kwenye utekelezaji wa hayo
 
Back
Top Bottom