Nimshitaki yupi?

Tareeq

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2010
Posts
828
Reaction score
408
Nilipata huduma kutoka kampuni moja inayouza Solar na vifaa vyake.

Miongoni mwa bidhaa ilikuwepo TV set . Baada ya siku mbili sikuwa nimeridhishwa na huduma za kifaa chao niliwaarifu kwa njia ya simu na wao hudai kuwa simu zao zinarekodiwa.

Niliwalipa 180,000 kama malipo ya awali kutoka kwenye set yao yenye value ya 2,400,000/= Ndani ya mkataba wao kuna kipengele cha endapo mteja hajaridhika na huduma ndani ya siku 7 anarudishiwa pesa yake.

Mimi niliwaarifu ndani ya siku 2 lkn wakala wao hakuja kuchukua bidhaa zao hadi siku ya 7 na hapo dai lao nikuwa hawatorudisha pesa maana taarifa ya kutoridhika wao haijawafikia kwa wakati na Natamani kumshitaki wakala wao au nimshitaki yupi, wajuzi wa sheria NISADIENI
 
Kampuni ya Sun King ndugu yangu
 
Una mkataba na nani? Huyo ndio mshtakiwa no 1
 
Kampuni ya SUNKING na ile ya MYSOL zamani MOBISOL ni Kampuni za KIJAMBAZI,KIHUNI na KITAPELI,ziogope kama unavyoogopa UKIMWI,yaliwahi kunikuta nilivyochukua mkopo MOBISOL,ni MAJIZI na MAVIBAKA
 
Solar system ya Kiwango hicho si zaidi ya 1.6 vifaa vyote na kwa raha zako
 
Una ushahidi gani kuwa uliwapigia simu ndani ya siku mbili?
 
Zipo call record kwao na kwa simu yangu Outgoing calls zina automatic record hata Incoming
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…