Nimuoe nani kati ya hawa, naombeni ushauri

Nimuoe nani kati ya hawa, naombeni ushauri

Kizuri zaidi ni dini moja kama yangu, ila ubaya wa Felister ni ana mtoto alizaaga baad ya kumliza la saba hata secondary hakwenda. Na mwanaume aliezaa nae bado yupo hai kwa taariifa aliyonipa japo yeye anasema hawawasiliani na huyo mwanaume ni mwanajeshi yupo mkoa mwingine na mke wake huko.
Hapo ndipo nimeishia kusoma,

Oa huyo ambaye mtaanza 0 - 0 ,

Hii 1 - 0 haiko vyema, Kuna Changamoto zitajitokeza mbele.
 
Muoe Nurath huyo ndiye mwanamke wa kuoa, kwa muda wa miaka 9 uliojuana naye na hujaona tatizo lolote huyo ndio mke. Felister utakuja kujuta, watu wakishazaa hawaachani mjeda akihitaji mzigo saa yoyote atapewa haijalishi umemuoa kwani KIPORO hakihitaji moto mwingi.
 
Unampenda felister na kwa bahati nzuri ni dini moja afu anajitambua na ameshapiga hatua kwa swala la uchumi. Kama umesha comferm kuwa Hana mahusiano na baba wa mjesh nakushauri oa single mother Kama utaweza omba namba ya mjeda ongea nae ili ucomferm kabisa . Kama utamuoa Nurat lazima utamsaliti tu kwa Felixter...
 
Habari za muda huu wana jamvi. Natumaini wote tu wazima
naomba mchue dakika chache kupititia uzi wangu huu kuhusu ujana wangu ili mpate kunisaidia kimawazo.

Mimi ni kijana wa miaka 28 sasa, ninaishi Dodoma mjini.

Mwaka 2014 wakati nipo chuo nilibahatika kuwa kwenye mahusiano na mwanamke mmoja hivi anaitwa Nurath,
huyu ni binti ki ukweli mimi sikumpenda au sikumtongoza kwakuwa nampenda au ni mzuri kufikia kiwango kile ninachotaka mimi ila ni mzuri.

Nilimtongoza tu kwa kuwa alinizoea sana kwa kipindi hicho sikuwa na girlfriends hivyo yeye nikaona kuwa atanidharau kwa kuwa anajisogeza kwangu sana mara discussion za usiku mara out huku na huku japo mimi moyoni mwangu najua kuwa sio type yangu kabisa.

So siku zikazidi kwenda na mazoea yakazidi ikabidi nipange mazingira ya kumla ili asinidhalrau maana hawa mabinti ukiwachekea chekea wanakudharua wanakuona nyoka wa kibisaa basi nikamla na nikamla kweli kweli maana ni muda mrefu nilikuwa sijakutana na mwili wa mwanamke.

Toka hapo mapenzi yakaanza lakin mimi nikiwa na langu moyoni kuwa napita tu njia hapa sio mkaaji maana sio type yangu japo yule dada sio mbaya kwa kweli.

Basi tukamaliza first year Diploma tukiwa wote japo akili yangu ni ile ile kuwa hapa napita njia.

Tulifunga chuo kila mtu kwao, sasa nilipofka nyumbani katika pita pita zangu nikakutana na Felister huyu ni binti niliemuacha madarasa mawili kipindi namaliza darasa la saba, ki ukweli toka ndani ya moyo wangu anakila sifa za mwanamke ninaye mtaka mimi kama mimi.

Tukapiga story mbili tatu akanipa namba maisha yakaendelea na mazoea yakaanza kati yetu, siku ya siku nikaona nimwambie kuwa nampenda naye hakuwa na hiyana akanipa nafasi maisha yakaendelea vizurii tu, sasa nikawa na wanawake wawili mmoja wa chuo wa pili wa nyumbani.

Nikafanikiwa kumaliza chuo diploma nikiwa na Nurath japo akili yangu ipo kule nyumbani kuwa ndio mwanamke wa ndoto zangu, nalipomaliza chuo nikajisemea kuwa huu ndio mwish wa mimi kuwa na Nurath kwa kuwa sitaonana nae tena hivyoo nikaona ndio njia nzuri ya kuachana nae bila kumuumiza yaan kimya kimya.

Ilipofika wakati wa ku-apply chuo kwa ajiri ya degree nilichagua chuo cha kwanza tofauti na alichochagua yeye na cha pili hivyovyo ila namba tatu nikachagua chuo ambacho yeye ameweka namba moja, nikiamini hata iweje nitachukuliwa chuo namba moja au mbili na yeye sitaweza kukutana nae tena.

Ila DAH DAH huwezi amini nilichaguliwa chuo chaguo la tatu ambacho na yeye amechaguliwa yaani ikawa automatic tutaenda kukutana tena, dah hadi kufika hapo nikawa nimechoka kabisa ila yeye alifurahi kuwa tutaenda kukutana tena ila kwangu haikuwa hvyooo kabisa.

Felister ni mwanamke mzuri sana ni mcheshi mkarimu anafanya biashara zake za mpesa ana mashamba analimisha msimu ukifika wa kilimo ana piki piki kama mbili hivi( bodaboda) yaani kiufupi anajiweza kujihudumia, na anajua sana mno mapenzi ni mtaalamu haswaa.

Kizuri zaidi ni dini moja kama yangu, ila ubaya wa Felister ni ana mtoto alizaaga baad ya kumliza la saba hata secondary hakwenda. Na mwanaume aliezaa nae bado yupo hai kwa taariifa aliyonipa japo yeye anasema hawawasiliani na huyo mwanaume ni mwanajeshi yupo mkoa mwingine na mke wake huko.

Ki ukweli Felister ananipenda sana mnoo ujue ila unapendwa hadi unajua hapa napendwa ndio ipo hivyo kwangu ananipenda na nampenda pia ila changamoto ni mtoto wake.

Nurath ni mwanamke mpole sana na mcheshi na ana huruma sana na amenisaidia mengi mno hasa maisha ya chuo hasa nikiwa mwaka wa pili ilifkia wakati nilitakiwa nighailishe masomo kwa kuwa sikuwa na ada na sikuwa na mkopo na hali ya kiuchumi nyumbani kwetu ilikuwa mbaya yeye alinilipia ada mwaka mzima na kodi ya geto nilipokuwa nimepanga mwaka mzima.

Yeye alikuwa na mkopo na kwao wao wapo vizuri kiuchumi ukilinganisha na mimi (kwetu), ni mwanamke mwaminifu sana na ni mcha-MUNGU kwa sana kwa dini yake.

Hadi leo nipo nae sababu ya mazoea tu kwa kuwa nimekuwa nae miaka tisa sasa na ukarimu wake kwangu, ila kuhusu mwanamke wa ndoto zangu hajafika vigezoo nipo nae sabab ya mazoea tu nimemzoea sana siwezi pita siku hajanipgia au sijampigia, kingine ni swala la dini yeye na mimi ni dini tofauti,

Nahisi nimefika umri wa kuoa sasa, maana nimemaliza chuo na namshkuru MUNGU ninakazi nzuri na maisha ya-naendelea ila kwenye list yangu yupo Nurath na Felister, nashindwa kuchagua nimuoe nani na nikisema niendelee kutafta mwanamke wa kumuoa naona kuna possibility kubw ya kuingia mkenge maana kwanza nina huitaji mkubwa wa mke so naona matamanio yataniongoza zaidi kuliko uhalisia pili nipo na uwezo kidogo so naona mwanamke atanikubalia sababu nipo na uwezo kuliko uhalisia wa kunipenda, hivyo nabaki njia panda tu nifanye nini.

Kwa Nurath ni dini tofauti lakini fact ya kwanza sijawahi mkubali/kumpenda hadi leo hii nimejitahidi ila nimeshindwa nahisi nikiwa nae nitakuwa namchiti sana ili kutafuta kilicho bora kwangu kwa mahitaj ya moyo wang, kwa Felister shida ni mtoto wake kibaya zaidi mwanaume aliyezaa nae bado yupo hai, nahisi sitakuwa na amani kabisa japo ni mwanamke yule inaemtaka mimi haswaaa.

Naombeni msaad wa mawazooo kati hili! Asante
Chukua ferister , mtoto ni baraka , full stop
 
Man. Grow up.
FELISTER HAPANA.
Felister alishauza roho yake kwa mwanaume mwingne yaani alitoa roho yake akaunganisha na mwanaume huyo mjeshi kuunganisha kiumbe-roho mwingine ambae ni huyo mtoto.
So Iko siku roho zitataka kukutana tena kimwili. Utachapiwa na mjeda uje kulia humu.
MKEKA WANGU NAMPA NURATH.
*Hajazaa
*Anakupenda na anajitoa sana
**Anakupenda kuliko unavyompenda.

Solution. Oa anayekupenda zaidi man. Nurath mmeimmeishi wote miaka 9 . ni mingi sana plus kukusaidia chuo. ukimuacha itamuuma.Felista unaweza mtungia Sabab kuwa ni single mom.

Nurath mpk anakuwa na ww ni rahisi kubadilisha dini kwani kashaji commit kwako.

Mkeka wangu unasema umpe tick NURATH.

Mambo ya mwanamke wa ndoto zako yatakuja kukuliza afu nilitaka nisahau Felista ana jiwe so jiandae kisaikolojia atakudharau siku pesa Ikienda mrama kwako. Ila kama Nurath ashawahi kukulipia ada we ishi naye mzazi.

Nurath I love you mama .me and you forever♥♡♥♡♥♡♥♡♥

Dedication song: Chris Brown_Right here
Mkuu.
umetumia muda wako kumpatia kijana ushauri mzuri nimependa.

TATIZO ukisoma vizuri maandishi ya kijana kuna possibility kubwa sana yakuwa ni CHAI, yani huu uzi ni fictional au amespice up mambo ame exeggerate mambo ili uzi wake uwe inchresting
 
Felster ana mtoto wa jinsia gani ,kuwa single mother na baba ya mtoto kuwa hai Wala sio shida
Kama mtoto ni WA kike oa felster endelea na maisha ila kama mtoto ni WA kiume usijaribu hata kuweka miguu utapata shida sana hasa uzeeni
Nurath hapana nadhani utamtesa sio sawa kuoa mke kwa kumuhurumia maana ndoa itakuwa toxic
Mwisho kabisa ukishindwa kwa wote Rudi nyuma na jipe mda Wala usiogope kupiga chini ukuta kama umepinda kuliko kuezeka Kisha nyumba ikaanguka
Rudi nyuma tafuta relation nzuri move on ndio life
 
Oa huyo Nurath. Kakujali sana wakati wote na kakusitiri wakati wote wa ufukara wako na magumu Yako. Amekukubali tangu ukiwa 'zero' kiuchumi na 'zero' kielimu. Huyo ndiyo mke wa maisha yako. Huyu ana unconditional love kwako.

Huyo wa pili anakupendea status Yako kielimu uliyonayo Sasa. Ana expect uhakika wa future akiwa nawe. Huyu amekupendea material things na ukizingatia tayari ameshazalishwa na kutelekezwa. Huyu ana conditional love kwako.

Au kama 'ubavu' upo, oa wote. Akili kumkichwa.

-Kaveli-
Atamtesa Nurath,mkuu umeshawahi kuwa na mwanamke usiempenda!?hadi hapo TU najua Nurath ndie anaehold mahusiano na ndio maana anaenda extra mile ili apate mume I feel sorry for her ila ni Bora aumie kuvunja mahusiano kuliko kuja Kuumia kwa kudharauliwa
 
Oa huyo Nurath. Kakujali sana wakati wote na kakusitiri wakati wote wa ufukara wako na magumu Yako. Amekukubali tangu ukiwa 'zero' kiuchumi na 'zero' kielimu. Huyo ndiyo mke wa maisha yako. Huyu ana unconditional love kwako.

Huyo wa pili anakupendea status Yako kielimu uliyonayo Sasa. Ana expect uhakika wa future akiwa nawe. Huyu amekupendea material things na ukizingatia tayari ameshazalishwa na kutelekezwa. Huyu ana conditional love kwako.

Au kama 'ubavu' upo, oa wote. Akili kumkichwa.

-Kaveli-Asante kwa ushauri mkuu
 
Felster ana mtoto wa jinsia gani ,kuwa single mother na baba ya mtoto kuwa hai Wala sio shida
Kama mtoto ni WA kike oa felster endelea na maisha ila kama mtoto ni WA kiume usijaribu hata kuweka miguu utapata shida sana hasa uzeeni
Nurath hapana nadhani utamtesa sio sawa kuoa mke kwa kumuhurumia maana ndoa itakuwa toxic
Mwisho kabisa ukishindwa kwa wote Rudi nyuma na jipe mda Wala usiogope kupiga chini ukuta kama umepinda kuliko kuezeka Kisha nyumba ikaanguka
Rudi nyuma tafuta relation nzuri move on ndio life
Asante kwa ushaurii , felister ana mtoto wa kiume
 
IPO HIVI

Kuoa nijambo muhimu ila unapaswa uangalie vigezo

Kigezo cha dini ni muhimu sana. Dini tofauti utaenda kuzalisha mgogoro mbeleni, wazazi wa Nurath hawatokubali mtoto wao kuolewa na dini tofauti. Mtoto akilazimisha kwa mujibu wa uisilamu HAKUNA NDOA KATI YA DINI MOJA NA DINI NYINGINE, nani atakuozesha? (Hapo tafakari kidogo)

Pili yeye akilazimisha akabadili dini mgogoeo ukijitokeza mtaishi vipi mahali ambapo wazazi(wakwe) hampendani je tatizo likijitokeza ndani ya ndoa mtalipeleka kwa nani awashauri au mkalitatue?

Je wewe utakuwa tayari kuvadili dini? Kama upo tayari Oa Nurat mara moja. Kama unaona ugumu basi jua hata wazazi wa nurat au nurat mwenyewe ataona ugumu huo huo.

Njia rahisi mwambie kwa kigezo cha dini mimi taoa mke mwingine mtaachana tu.

NIRUDI KWA WANAWAKE WOTE NJE YA MADA

hivi kwanini mnapenda kuchezewa kirahisi hivyo, yaan unatongozwa hapo hapo unakubali unapelekwa gheto khaa, ifike mahali kuweni na misimamo nyie, MWANAUNE UKIMKAZIA KUWA HUMPI NA KWELI UKAWEKA MKAZO ATAKUOA ATAJUA HUYU NI WIFE MATERIAL

Yaani mnakutana kwenye daladala, discussion hamjuani eti mnapeana namba mara mpo gheto au guest ,duuh ase

Ndoa ni maridhiano ya wanaopendana me/ke na kisha familia zote mbili ziunge undugu zingatieni kigezo cha familia zote kubariki ndoa yenu ili hata tatizo likitokea muweze kulitatua ki familia
 
Asante kwa ushauri mkuu
 
Back
Top Bottom