Nimuoe nani kati ya hawa, naombeni ushauri

Hapo ndipo nimeishia kusoma,

Oa huyo ambaye mtaanza 0 - 0 ,

Hii 1 - 0 haiko vyema, Kuna Changamoto zitajitokeza mbele.
 
Muoe Nurath huyo ndiye mwanamke wa kuoa, kwa muda wa miaka 9 uliojuana naye na hujaona tatizo lolote huyo ndio mke. Felister utakuja kujuta, watu wakishazaa hawaachani mjeda akihitaji mzigo saa yoyote atapewa haijalishi umemuoa kwani KIPORO hakihitaji moto mwingi.
 
Unampenda felister na kwa bahati nzuri ni dini moja afu anajitambua na ameshapiga hatua kwa swala la uchumi. Kama umesha comferm kuwa Hana mahusiano na baba wa mjesh nakushauri oa single mother Kama utaweza omba namba ya mjeda ongea nae ili ucomferm kabisa . Kama utamuoa Nurat lazima utamsaliti tu kwa Felixter...
 
Chukua ferister , mtoto ni baraka , full stop
 
Mkuu.
umetumia muda wako kumpatia kijana ushauri mzuri nimependa.

TATIZO ukisoma vizuri maandishi ya kijana kuna possibility kubwa sana yakuwa ni CHAI, yani huu uzi ni fictional au amespice up mambo ame exeggerate mambo ili uzi wake uwe inchresting
 
Felster ana mtoto wa jinsia gani ,kuwa single mother na baba ya mtoto kuwa hai Wala sio shida
Kama mtoto ni WA kike oa felster endelea na maisha ila kama mtoto ni WA kiume usijaribu hata kuweka miguu utapata shida sana hasa uzeeni
Nurath hapana nadhani utamtesa sio sawa kuoa mke kwa kumuhurumia maana ndoa itakuwa toxic
Mwisho kabisa ukishindwa kwa wote Rudi nyuma na jipe mda Wala usiogope kupiga chini ukuta kama umepinda kuliko kuezeka Kisha nyumba ikaanguka
Rudi nyuma tafuta relation nzuri move on ndio life
 
Atamtesa Nurath,mkuu umeshawahi kuwa na mwanamke usiempenda!?hadi hapo TU najua Nurath ndie anaehold mahusiano na ndio maana anaenda extra mile ili apate mume I feel sorry for her ila ni Bora aumie kuvunja mahusiano kuliko kuja Kuumia kwa kudharauliwa
 
 
Asante kwa ushaurii , felister ana mtoto wa kiume
 
IPO HIVI

Kuoa nijambo muhimu ila unapaswa uangalie vigezo

Kigezo cha dini ni muhimu sana. Dini tofauti utaenda kuzalisha mgogoro mbeleni, wazazi wa Nurath hawatokubali mtoto wao kuolewa na dini tofauti. Mtoto akilazimisha kwa mujibu wa uisilamu HAKUNA NDOA KATI YA DINI MOJA NA DINI NYINGINE, nani atakuozesha? (Hapo tafakari kidogo)

Pili yeye akilazimisha akabadili dini mgogoeo ukijitokeza mtaishi vipi mahali ambapo wazazi(wakwe) hampendani je tatizo likijitokeza ndani ya ndoa mtalipeleka kwa nani awashauri au mkalitatue?

Je wewe utakuwa tayari kuvadili dini? Kama upo tayari Oa Nurat mara moja. Kama unaona ugumu basi jua hata wazazi wa nurat au nurat mwenyewe ataona ugumu huo huo.

Njia rahisi mwambie kwa kigezo cha dini mimi taoa mke mwingine mtaachana tu.

NIRUDI KWA WANAWAKE WOTE NJE YA MADA

hivi kwanini mnapenda kuchezewa kirahisi hivyo, yaan unatongozwa hapo hapo unakubali unapelekwa gheto khaa, ifike mahali kuweni na misimamo nyie, MWANAUNE UKIMKAZIA KUWA HUMPI NA KWELI UKAWEKA MKAZO ATAKUOA ATAJUA HUYU NI WIFE MATERIAL

Yaani mnakutana kwenye daladala, discussion hamjuani eti mnapeana namba mara mpo gheto au guest ,duuh ase


Ndoa ni maridhiano ya wanaopendana me/ke na kisha familia zote mbili ziunge undugu zingatieni kigezo cha familia zote kubariki ndoa yenu ili hata tatizo likitokea muweze kulitatua ki familia
 
Asante kwa ushauri mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…