Nimwache akapange au niondoke mimi?

Nilimvumilia nikijua atabadilika lakini kadiri siku zinavyokwenda hali inazidi kuwa mbaya zaidi, maana mpaka sasa kajenga uadui na ndugu zangu na mama yangu pia bila sababu yoyote
mkuu people don't change,
achana naye huyo,nasikitika kukwambia kwamba kuna mwanaume yupo naye anampa jeuri hiyo
 
Bro unasubiri akuue na presha au? kimbia Mtoto wako mchukue uishi nae
 
Mkuu nimekujibu kule ulipo bandika mara ya kwanza
 
Anza kwa kuwaweka karibu wazazi na ndugu zake wenye sauti (influence). Ukishafanikiwa "kuwateka nyara" hao wasukumizie hiyo kesi. Nakuhakikishia kuwa huyo mwanamke ataacha "ujinga" wake na wewe utaishi bila pressure na utakuwa mwenyewe nguvu kupindukia.
 
Ndugu zake hawana ushirikiano kila mmoja ni mtu wa kujitenga na wana lawama sasa mkuu, nilijaribu kufanya hivyo lakini mwisho wa siku ndugu zangu, mama yangu na mimi ndo tunaonekana wabaya.
 
Taa za Tahadhari (Njano) zimekuwakia mapeeema mno kiasi kwamba Taa ya kukusimamisha kuruhusu upande mwingine inawaka anytime ila husikii na unajifanya huioni wewe mguu umeuweka kwenye kibati. Kila la kheri kwa litakalokukuta
 
Huu ujasiri ni sawa na kujifunika shuka moja na nyoka??


"Fyekelea mbaliii huyo hajitambui"
 
Huwaga najiulizaga inakuwaje matatizo yako unampelekea Mchungaji ,...sipati jibu
 
Mkuu nilikuwa na mwanamke wa aina hiyo nlikuwa mvumilivu kama wew na pia huyo dada alikuwa akinitukana hadi usiku nayaota Yale matusi... Bt siku moja nlipiga moyo konde nikamwambia sikutaki na afanye mambo yake huwezi hamin kwasasa naongeza kilo kila mwezi nikipiga kilo naongezeka baada ya Yule mwanaharamu kuachana nae
 
So aliondoka au uliondoka na kumwachia kila kitu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…