Nimwache akapange au niondoke mimi?

Nimwache akapange au niondoke mimi?

Kuondoka anasema mpaka mwakani, mimi nimechoka sana na nikimwona najawa na hasira sana kiasi kwamba huwa naondoka tu home na kwenda matembezi yangu sometimes naenda kulewa. I am so stressed kiasi kwamba sitaki ugomvi kabisa
Pombe ndio itakuongezea matatizo baada ya kumuacha mwanamke eti naenda kulewa zangu. Yaani wewe unajisainisha kuwa maskini mwenyewe.Pole bwana kunywa pombe sio Suluhisho la matatizo yako . Kaa nae mwambie a to z na Kwa sasa iwe mwisho wa mahusiano yenu. Uyo atakuwa jini
 
Chukua mtoto peleka kwa bibiake (mama yako) then piga chini achana nae huyo mwanamke ambae hajitambui kama kuna jamaa anamdanganya na anamdanganya kweli. Mwanamke gan unampeleka kwenu hachangamkii watu kaz kuchati tu.
Kwahyo mkiendaga kwenu hata jikon inaonekana huwa haingii kwa hiyo apikiwe na nan.
Hakaf inaonekana unampenda sana na alishalijua hilo haiwekan umwachie biashara na unsona haileti matunda unaangalia tu
Mtoto siyo kigezo na utajuta ukiendelea nae huyo asiejitambua
Piga chini wanawake wanaotaka kuolewa n wengi mno.
Ushaurii mzuri.. Nlikifikiri hivyo hivyo
 
Kuondoka anasema mpaka mwakani, mimi nimechoka sana na nikimwona najawa na hasira sana kiasi kwamba huwa naondoka tu home na kwenda matembezi yangu sometimes naenda kulewa. I am so stressed kiasi kwamba sitaki ugomvi kabisa
Demu anafanya upuuzi wote huo Hujawahi kumnasa hata Vibaoo... Au limbwata baba????[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mtoto peleka kwa Bibi, yeye rudisha kwao kama kifurushi tu, kinachotumwa kwenda Ulaya
 
Habari wanaJF, naomba mnishauri pia kwa hili.

Nilikutana na binti mmoja mwaka 2012 katika mazingira ya kazini na tukaingia katika mahusiano, binti huyo alikuwa akiishi kwa dada yake mkubwa ambaye wamechangia mama. Kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba dada yake huyo alikuwa akimnyanyasa na kitendo kile kiliniuma sana nikaamua kumpangishia chumba akaanza maisha yake hapo, hiyo ilikuwa ni 2013. Tuliendelea na mahusiano mpaka niliamua kujitegemea mwaka 2015 na tangu mwanzo wa mahusiano yetu alikuwa akija mpaka nyumbani kwetu na ndugu zangu wote wanamfahamu. Aliamua kuja kuishi na mimi hivyo nilimkaribisha tukaishi wote, sasa hapa ndo matatizo yakaanza.

Alianza kuzua migogoro ndani na hatukuwa tunaelewana mara nyingi, nilikuwa na biashara nikamweka asimamie biashara ile nilikuwa najua inaingiza kiasi gani lakini tangu aanze kusimamia iliyumba na hakuwa ananishirikisha mauzo ya siku. mostly jibu lake lilikuwa biashara mdogo mdogo, mwaka huo huo akashika mimba na Mungu akajalia akajifungua 2016 March, kipindi hicho nilikumbwa na mtikisiko mkubwa kiuchumi hivyo hali haikuwa nzuri. Katika maisha yetu alikuwa ni mtu wa kufanya maamuzi peke yake na nikijaribu kuhoji inakuwa ugomvi nikaamua kukaa kimya kuepusha shari. Hivyo aliwaleta ndugu zake kuishi kwangu bila idhini yangu maana hali ya uchumi ilikuwa si nzuri. Akaanza kulaumu kuwa ndugu zangu wanamchukia ilhali yeye alikuwa akienda kwetu hafanyi chochote ni kuketi tu muda mwingine hamsemeshi mtu anakuwa busy na simu yake. Tukitoka anaanza kutupa lawama kwangu kwamba ndugu zangu na mama yangu hawampendi. Nilijaribu kumwelewesha na kumwambia kuwa mama hapendezwi na tabia ya yeye kujitenga maana kama anahitaji kuolewa na mimi lazima achangamane na familia yangu lakini haikufua dafu. Hali hiyo iliendelea hata kufikia hatua mama yangu akimpigia simu hapokei kwa makusudi, nikimuuliza anasema hajisikii kuzungumza na simu, mama akipiga kwangu nikimpa pia jibu ni lile lile.

Hali hiyo ilinitesa sana maana nikiangalia maisha yake ya nyuma napata ugumu kumuacha maana namsikitikia mwanangu atateseka sana. Nilifanikiwa kupata kazi nyingine hapa Dar na kuhamia hapa mwaka 2017 July, nilianza kazi vizuri na nikawa natuma pesa za kutumia kama kawaida nilikuwa nikituma laki 2 kila mwezi kwa ajiri ya matumizi, na biashara ile ilikuwa ikiendelea kama kawaida japo sikuwahi kujua mapato yake kabisa. Cha kushangaza ni kwamba kila baada ya wiki mbili niliambiwa hakuna pesa ya kutumia na hakuna chakula mtoto hana chakula pia, ilinibidi nitoe pesa yangu ya kujikimu niitume kwao kitu ambacho kiliendea kuwa hivyo kwa muda wa miezi 5. Wakati mwingine sikuwa na pesa kabisa kwa sababu ya matumizi kwake kuwa mengi na nilijaribu kuhoji pesa inatumika vipi ilizua mgogoro sana. Na alikuwa mtu wa kulalamika na kunitumia sms za matusi[Zipo Zote] kunitukana lakini sikuangalia hayo maana imani yangu ilikuwa ni kujenga familia na huyo dada. Mwaka jana mwezi wa 12 nilimwambia ajiandae ahamie huku hivyo vitu vyote nikampa melekezo avipeleke kwa mama yangu na ndivyo tulivyokubaliana. Nilituma pesa ya nauli Tshs 210,000/= Kwa ajili ya safari (100,000/=) na kumalizia kodi ya nyumba (100,000/=) lakini huwezi amini kabla ya siku moja safari kuanza aliniambia kuwa hana pesa ya nauli nimtumie nauli.

Nilishikwa na hasira sana na tayari nyumba niliwambia wakabidhi kwa mwenyewe, Vitu aliamua kuita ndugu zake wakaja kuchukua bila kunishirikisha. Nilipigiwa simu na mdogo wangu akiniambia mbona mambo yako tofauti na mlivyopanga? kwa hekima niliwaambia wadogo zangu waondoke tu lakini pia haikutosha ndugu zake na huyo dada walianza kuwamwagia wadogo zangu matusi kiasi cha kushangaa kuna nini mpaka iwe hivyo. Nilimpigia huyo dada na kumuuliza kuhusu tukio hilo niliambulia matusi ya ajabu sana na hapo nimetoa tena pesa nyingine ya nauli ili tu mwanangu awe karibu yangu.

Nikajisemea kuwa akifika nitamhoji anieleze vizuri, lakini alipofika alikuwa ni mtu mwenye maneno mengi sana na matusi makali, niliamua kuachana nayo hayo na kufungua ukurasa mwingine wa maisha (Kumsamehe). Tukaishi maisha ambayo kila siku anazua jambo, wakati mwingine namsalimu haitikii, namsemesha hajibu ikafika wakati nikaamua kumtizama tu. Nilipanga niende kwao kutoa mahali mwezi wa 11 mwaka huu lakini kwa tabia hizi sidhani kama naweza. NImeshajaribu kuzungumza naye, kumshirikisha mchungaji wa kanisa analosali, kwa muda fulani nikaona mabadiliko lakini hali ilirudi vile vile. Ilifika kipindi nimetoka kazini nikamkuta ndugu yake kaja kumsalimu, kabla sijaingia ndani nilisikiwa wakinizugumza vibaya sana. Nilichukia sana lakini nikamwambia Mungu kwamba ikiwa mimi ndiye nimemfanya mtu huyu awe hapa sina haja ya kuchukia kwa hiki anachonena kuhusu mimi. Niliingia ndani nikabadili nguo zangu na kutoka kwenda matembezi.

Hivi karibuni kuna ndugu yangu alikuwa anaolewa huko kanda ya ziwa, nikamwambia huyo dada apige hesabu ya mahitaji yake na mtoto kwa ajili ya harusi. Alinipa hesabu yake nikasema sawa ilikuwa around 200K nikatafuta pesa Mungu akajalia nikapata 1M nikamwambia kuna pesa hii imepatikana so wajiandae kwa ajili ya kwenda kwenye harusi. Tulipanga kwenda kufanya shopping the next day. Tulikwenda kariakoo kuanza shopping, cha ajabu yale aliyopanga kununua nikaona anatafuta nguo za mama yake (Kitu ambacho hakuwa amenishirikisha na ilikuwa nje ya budget) nilikaa kimya nikamnunulia mwanangu, yeye alipomaliza kununua alivyokuwa ananunua akanambia anahitaji pesa ya kujinunulia yeye pia.

Seriously nilishikwa na hasira sana maana haikuwa katika budget, na ukizingatia tunakwenda kwa siku chache tu na hatukupanga kufanya yote hayo maana kulikuwa na mambo mengine ya muhumi ya kufanya baada yakurudi dar. Siku hiyo ilikuwa mbaya sana kwangu maana aliongea maneno makali sana kiasi kwamba nikashikwa hasira nikampa hiyo pesa aliyohitaji, aliema asante but sikumjibu kabisa. Tulikwenda nikijua tunafikia kwenye tukio lakini kumbe kwake ilikuwa ni tofauti tulipo fika alinambia nimpeleke kwa dada yake, nilifanya kama alivyohitaji. Nikategemea asubuhi atakuja ajishughulishe katika shughuli za tukio hakuonekana simu hapokei mara nakuja baada ya nusu saa mpaka ikafika jioni. Kesho yake nikamwambia ajitahidi kuwahi aje kujumuika na kusaidiana na wenzake lakini alikuja saa nne asubuhi na kunifuata moja kwa moja anaomba pesa aende salon. Sikumpa nilimwambia sina maana tayari alishaniudhi. Akaingia ndani kwamba anakwenda kubadili nguo aje kufanya kazi, kumbe haikuwa hivyo akaondoka kwenda zake salon. Sasa tangu hapo hakukanyaga tena kwetu, mpaka siku ya harusi yenyewe ndo akaonekana tena. Tulijumuika na baada ya sherehe kuisha nilianza maandalizi ya kurudi Dar, siku iliyofuata akaniambia anahitaji kuzungumza na mama yangu, mimi na ndugu zangu nikasema sawa. Akatuita tukaketi kumsikiliza akaomba msamaha wa kilichotokea na kuhusu matusi yaliyotukanwa kwenye sakata la vitu na mengine mengi wakamsikiliza na wakamwambia wao hawana tatizo kabisa, akanaambia nimsindikize kwenda kwa dada yake nikamsindikiza.

Huko njiani alinitolea maneno makali sana nikajiuliza kwamba huo msamaha aliokuwa akiomba alimaanisha nini? au alikuwa akiwajaribu ndugu zangu na mama yangu? sikutaka mengi wala sikujibu kitu nikamfikisha nikaondoka. Sasa mwezi huu ilikuwa niende kwao nikatoe mahali lakini moyo wangu sasa haumuhitaji tena maana naona tunakoenda nitafanya kitu cha ajabu juu yake kinachoniumiza ni mwanangu tu.

Nilimweleza kuhusu kuachana mimi na yeye akasema ataenda kupanga chumba hapa hapa Dar kitu ambacho nikifikiria mazingira hayo kwa mwanangu siyo kabisa, naombeni ushauri wenu nifanyeje? maana jambo hili limenichosha sana. binti ni mzuri but tabia zimenishinda

Mkuu wewe ni malaika.
 
Mi nahc ninaroho ya unyama siwez kung'ang'ania matatzo kisa eti mtoto tena huyo anavoonekana atakuja kukuua mbele ya safari ili awehuru zaidi
 
Huwa najiuliza huko daslamu siku hizi kuna nini??

Mbona kila mwanaume akienda huko akili inabadilika??

Ushauri,
Usiishi na mtu kwa sababu imezaa nae, mtamtesa mtoto maishani mwake.
Mnakoelekea ni kuanza kuaibishana mbele ya mtoto
Bora akaishi huko na mama najua anapata visa vingi vya kutunga lakini huwa ni vya muda.
 
Habari wanaJF, naomba mnishauri pia kwa hili.

Nilikutana na binti mmoja mwaka 2012 katika mazingira ya kazini na tukaingia katika mahusiano, binti huyo alikuwa akiishi kwa dada yake mkubwa ambaye wamechangia mama. Kwa mujibu wa maelezo yake ni kwamba dada yake huyo alikuwa akimnyanyasa na kitendo kile kiliniuma sana nikaamua kumpangishia chumba akaanza maisha yake hapo, hiyo ilikuwa ni 2013. Tuliendelea na mahusiano mpaka niliamua kujitegemea mwaka 2015 na tangu mwanzo wa mahusiano yetu alikuwa akija mpaka nyumbani kwetu na ndugu zangu wote wanamfahamu. Aliamua kuja kuishi na mimi hivyo nilimkaribisha tukaishi wote, sasa hapa ndo matatizo yakaanza.
Huko njiani alinitolea maneno makali sana nikajiuliza kwamba huo msamaha aliokuwa akiomba alimaanisha nini? au alikuwa akiwajaribu ndugu zangu na mama yangu? sikutaka mengi wala sikujibu kitu nikamfikisha nikaondoka. Sasa mwezi huu ilikuwa niende kwao nikatoe mahali lakini moyo wangu sasa haumuhitaji tena maana naona tunakoenda nitafanya kitu cha ajabu juu yake kinachoniumiza ni mwanangu tu.

Nilimweleza kuhusu kuachana mimi na yeye akasema ataenda kupanga chumba hapa hapa Dar kitu ambacho nikifikiria mazingira hayo kwa mwanangu siyo kabisa, naombeni ushauri wenu nifanyeje? maana jambo hili limenichosha sana. binti ni mzuri but tabia zimenishinda

One thing, ndugu wanazingua sana lakini tuna upendo wa asili wa kuvumilia hasa kama ndugu mnashea wazazi. Mara nyingi ukiona mtu hapatani na ndugu yake usikurupuke kuangalia upande mmoja.
Mahusiano yako naona umeyaharibu mwenyewe toka mwanzo (sikulaumu kabisa maana najua mapenzi yalivyo). Hii ni kwa kukubali akuendeshe. Pia alipokuwa anakaa, wakati ndugu zake na yeye wanafukuza na kuwatukana ndugu zako na akatumia hela ya nauli ulitakiwa usitishe zoezi hapohapo.
Cha kufanya, nenda kwao ukalipe mahari/fine (ni mbaya kumzalisha binti wa watu na kwao hawakujui officially). Kisha Quit the relationship . Tafuta mwanamke anayeeleweka, huyo muache akue
 
Kwanza mkatie mwanao bima ya afya, ili upunguze ile mizina ya mtoto anaumwa sana kumbe ukituma hela yy anaenda saluni, ustawi wa jamii mtoto kwa mwezi ni kama elfu 80 hivi so yy ataambulia hiyo tu... piga chini
 
Kuondoka anasema mpaka mwakani, mimi nimechoka sana na nikimwona najawa na hasira sana kiasi kwamba huwa naondoka tu home na kwenda matembezi yangu sometimes naenda kulewa. I am so stressed kiasi kwamba sitaki ugomvi kabisa
Mkuu unatafuta hasara kwa ndugu zako hasa mamako. Kumbuka unategemewa na ndugu zako hivyo kuanza kupata ugonjwa wa moyo ni kuhatarisha maisha yako na wazazi wako.

Plz plz plz bro sijui umeumbwaje wewe maana mwanamme mvumilivu hivyo kizazi hiki hayupo. Ila mwisho wake utakufa alafu umwache yeye.

Fanya yafuatayo kama hataki kuondoka we fanya yafuatayo
1. Tafuta safari yoyote ya yeye kwa gharama yoyote ile aende kwao.
2. Akiondoka tafuta nyumba uhame na ikiwezekana badili na mawasiliano na umwambie asirudi tena maana umehama na hutaki maisha na yeye tena.

Bila shaka utaponya nafsi yako
 
Ninampango wa kuondoka nimwachie kila kitu maana uwezo wa kununua vingine upo so vitu kwangu siyo shida, labda nguo zangu tu na vifaa vyangu vya kazi
Nguo na vifaa vya kazi chukua na baadhi ya vitu chukua. Mkuu mbona mbinu ya kuchukua vitu ni simple mkuu. Mpe hela aende saloon akitoka we chukua gari somba vitu vyako mwachie jiko na kitanda na ndoo ya kuogea tu lakini mezani mwachie nauli na barua ya kumweleza aende kwao na huku ikiwezekana badili lain ya simu kwa mda. Ila ukibadili lain watu wa karibu waeleze juu ya kumiliki lain nyingine
 
Back
Top Bottom