Nina 10M nahitaji kufuga Samaki naombeni ushauri

Hiyo pesa ni bora ukanunue IST uifanye UBER, pesa yako itarudi mapema tuu
 
Mkuu mbona wanasema vyuma vimekaza huko!hiyo 10milioni umetoa wapi?[emoji1]
 
Ni vizuri kutembelea hao SUMA JKT na wakulima wengine na kufanya research na kubaini yafuatao:
  1. Uwepo wa soko la uhakika wa aina ya samaki utakaofuga (kwa maeneo ya Dar- sato au kambale. Salmon wanafanya vizuri maeneo ya baridi)
  2. Aina ya mabwawa (ya kuchimba au ya kujengea)
  3. Upatikanaji wa mbegu bora
Anzia kiwango kidogo kwani bado huna uzoevu katika hili na kila biashara haikosi changamoto zake. Hii itakukupatia fursa ya kusoma practically na kufanya marekebisho yatakayoibuka bila kuingia hasara kubwa.
Kwa uzoefu wangu mdogo hauhitaji mtaji mkubwa sana katika hii phase ya kuanzia, ila katika phase ya pili- expansion ambayo utaifikia baada ya kipindi kama cha mwaka mmoja.
 
Kaka ubalikiwe sana kwa maelekezo yako mkuu...., nashukuru sana. Nami nahisi Suma JKT lazima niwatebembelee kisha niwatembelee wafungaji wawili watatu wa kawaida tu wa njia tofauti tofauti...., then baada ya hapo ndio nianze kidogo as pilot project ambayo itaruhusu makosa, then kila ninavyo expand ndio napunguza makosa uku project inakuwa.
 
mzee mpango mzima ni kambarez masamaki haya yana gharam chini sana kuwafuga, na unavuna baada ya mwaka wakiwa na kilo 4 na kilo moja elf6. kuna mzee nliwahi kumtembelea pale mbezi kwa mangi ana mabwawa matatu kila bwawa lina samaki 7000.anavuna samaki 21000 kila mwaka anawauza kati ya elf 20 hadi 24 kwa mmoja
 
Safi sana.
Mi bado niko pilot phase katika ufugaji wa kambale. Uhalisia wa mambo mengine ni tofauti kabisa na mambo niliyopata kwa watalaam au kusoma kwenye vitabu. Nimejikuta pia nikifanya makosa madogo madogo katika vitu vya msingi kama iana ya chakula, water quality,..... ambayo unahitaji kupata uzeofu halisi. Ila kuna mengi mazuri nimeokoteza mitandaoni, sana sana kutoka blog za wanaigeria- hawa wako mbali sana katika nyanja hii, tovuti ya FAO na video mbali mbali za ufugaji youtube.
Inshallah nitaanzia phase 2 hivi karibuni.
 
Karibu sana ndugu.
Nimekutumia contacts zao. Natumaini utapata muafaka na kuleta mrejesho hapa.
NB: Matenki yanakuwa matano (1000 ltrs) per system na sio moja.
Nakutakia kila la kheri mkuu.
 
Karibu sana ndugu.
Nimekutumia contacts zao. Natumaini utapata muafaka na kuleta mrejesho hapa.
NB: Matenki yanakuwa matano (1000 ltrs) per system na sio moja.
Nakutakia kila la kheri mkuu.
Mkuu umeelezea vizuri sana, naomba unisave na hizo contacts za SUMA tafadhali.
 
Hiyo yote haijalishi issue ni kufuata vigezo na mashariti iwe ni bwawa la kawaida,Tanks,Cage faida unapata tu.

Haiji akilini unataka kufanya aqua-ponics na hata hela ya kununua water pump huna.
Peleka upuuzi wako kwenye jukwaa la udaku tafadhali. Sijaja hapa kubishana, nimekuja kutoa msaada kwa mujibu wa utu na kumpa uelekeo mleta mada.
Huna hata uelewa wa nini unachozungumzia. Pathetic!
 
Peleka upuuzi wako kwenye jukwaa la udaku tafadhali. Sijaja hapa kubishana, nimekuja kutoa msaada kwa mujibu wa utu na kumpa uelekeo mleta mada.
Huna hata uelewa wa nini unachozungumzia. Pathetic!
Mimi naamini katika utaalam kwani ukubwa wa bwawa hutoa mazao mengi.

Hebu chukua case study ya Egyp na ufugaji wa mabwawa unakuta mtu ana bwawa la 1ha. Ila ndio hivyo ukimkimbiza kichaa na wewe inabidi upimwe akili.
 
watembelee banda lao la JKT mwezi ujao pale katika maonyesho ya Sabasaba ; watakupatia mashine pamoja na tank kwa 4mil hadi 6mil kulingana na ukubwa Wa mashine utakayochagua,
Ni matank mathubuti yaliyoboreshwa pia watakupatia vifaranga vya samaki kama mtaji, kwa maelezo zaidi ni Pm au fika ofisi za JKT;
Utakuwa na Uwezo Wa kuvuna samaki 200 hadi 600 kila baada ya miezi mitatu
 
Mimi naamini katika utaalam kwani ukubwa wa bwawa hutoa mazao mengi.

Hebu chukua case study ya Egyp na ufugaji wa mabwawa unakuta mtu ana bwawa la 1ha. Ila ndio hivyo ukimkimbiza kichaa na wewe inabidi upimwe akili.
Ndio umeandika nini sasa hapa!? Katika ulimwengu wa leo bado unaamini ukubwa wa eneo ndio ukubwa wa output ya mazao!? Hakika huna unalojua.
Pathetic!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…