Nina $ 23,000 ila sijui biashara gani inanifaa

Bullshit

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
1,357
Reaction score
1,596
Wanajamii nimekuwa na wakati mgumu wa kuamua kufanya biashara gani itakayonifaa nitakapoamua kuacha kuangaika kwenye kazi za watu,

Nahisi pesa nilionayo($23,000=milioni 50 hivi za shilingi) inafaa kuwekeza ila nakuwa na wakati mgumu wa biashara hipi inafaa kulingana na pesa nilionayo au njia zipi nipitie ili niwe na mafanikio katika biashara yangu

Kwa mwenye kuwa na uelewa au uzoefu na maswala ya biashara na ushauri wa mambo haya anaweza kunishauri nipite njia zipi au nini nifanye kuwa bora katika biashara yangu ya aina yeyote ninayotaka kufanya

NINAWAKARIBISHA WAKUU.
 
Tafuta wateja ufanye biashara ya EXPORT ya COFFEE ( ARABIKA ), COPPER ( CATHODES + ANODES ), VENEER + PLYWOOD, MANGANESE ORES, LEAD ORES, MBAO na MAGOGO ( TEAK, MKURUTI n.k ).
 
Tafuta wateja ufanye biashara ya EXPORT ya COFFEE ( ARABIKA ), COPPER ( CATHODER + ANODES ), VENEER + PLYWOOD, MANGANESE ORES, LEAD ORES, MBAO na MAGOGO ( TEAK, MKURUTI n.k ).
Ujafanunua vizur mkuu biashra inafanyikaje
 
Hayo ni malighafi za viwandani, unanuna zinakopatikana huku Africa then unasafirisha ( export ) kwenda kwa mteja wako nje ya nchi. Soko kubwa liko Ulaya, Asia na Marekani.
Ok,ngoja nilifanyue uchunguz mkuu
 
Kama ni hela ya pension ndo unategemea ufanyie biashara baada ya kustaafu....dont hiyo hela ndogo kwa biashara kwa wakati huu utakufa kwa frustration na stress think twice
 
Mkuu inategemea uko location gani.
Ila Kama upo dar au dodoma biashara rahisi na isiyooza ni ya vifaa vya ujenzi.

Ingekuwa Mimi ndio ww na Nina mtaji Kama huo nisingeumiza kichwa.

Ningechukua milioni 20 nikaanzisha hardware nje ya mji maeneo Kama kiluvya,goba,madale,vikindu n.k.

Halaf ile m 30 ingekaa tu kwenye akaunti wakati huo naisoma biashara inakwendaje?

Yaani wala usijiingize kwenye mabiashara makubwa yanayohusisha vibali vya maliasili au vibali vya kusafirisha nje ya nchi,utajikuta hela imepukutika wakati hata hyo biashara haijaanza kufanyika.

Milioni 50 Ni hela nzuri ukituliza kichwa lakini pia ni hela ndogo ukibugi utajikuta inakupita Kama upepo.
 
Kama ni pesa huitegemei kwa chakula basi ingia Zanzibar, tafuta kampuni ya utalii ongea nao ziko nyingi haswa zenye magari ya kukodisha mkubaliane bei huwa sio chini ya laki tano kwa mwezi kama utampabdereva moja moja au inaweza fika dollar 30 kwa siku kama kampuni wataichukua maana wao wanakodisha kwa dollar 50 mpaka 60 kwa siku. Ukishapata kampuni sasa nunua alphard 3 kila moja Zanzibar haizidi milioni 12 mpaka na usajili hapo pia unaweza changanya magari ukawa na ya aina tofauti ila alphard isikose ndio habari ya mjini kwa sasa kwa kampuni ikiwa sambamba na prado tx (model flani ya kati hivi sio old ila prado ghari wewe chukua gari zisizidi m12), unaweza chukua Alphard na suzuki vitara au na toyota hizi size ya suzuki vitara. Kwa kila mwezi hutokosa 1.5m sasa sio ya kula hiyo unakusanya unaongeza magari hapo inamaana kila miezi 6 unaongeza gari moja zikifika kumi basi zinatosha, usihofu kuhusu kuharibika barabara za zenji nzuri utafanya kazi ya service tu ambayo kwa mwezi ni kumwaga oil pekee ndio kinafanyika huku. Wakati ukiwa umezikodisha kwa mtu fungua website anza kutafuta wageni mtandaoni na kukodisha magari kwa wahitaji wazawa na wageni, basi utafurahi mwenyewe.

Kwanza uje utazame fika pale Forodhani kuna kijiwe cha madereva tax, wale ndio wanabeba watalii huku watakupa abc zote. Kuna mtu nimesomea nae primary yaani ni mate wangu mpaka umri kazi yake ndio hiyo now anamalizia ujenzi wa nyumba yake ya milioni 200 so nikikueleza iko hela tambua iko tatizo la watu huwa mitaji na wewe mtaji huo unao. Nimekuchagulia zenji sababu barabara nzuri, kuna bahari sio rahisi watu kuvusha gari kwa nia ya kuiba, wengi wanakuja zenji kutalii hivyo wazawa na wageni wanakodisha sana magari sio bara mpaka upate kampuni ndio watakodisha gari kwako.
Ahsante sana
 
Vizuri sana mkuu nashukuru kwa usharuri wqko,nina ndugu zngu wa tatu fundi ujenz naisi watanisaidia hata kununua vfaa hvyo,hata kunipa maelezo biaahara inayofaa
 
Shukrani mkuu kwa ushauri wako,,,,,,nitaufanyia kazi ili nipata data zaidi
 
Vizuri sana mkuu nashukuru kwa usharuri wqko,nina ndugu zngu wa tatu fundi ujenz naisi watanisaidia hata kununua vfaa hvyo,hata kunipa maelezo biaahara inayofaa
Yes mkuu na ukishaanza biashara hao mafundi ndio watakusaidia kuleta wateja.
Wenzako wanachofanya ni kwamba fundi akimleta mteja au akija kununua yeye mwenyewe unampunguzia bei kidogo ili abakiwe na hela kidogo hata elfu 20 au 30.
Baada ya hapo kila akipata saiti atakuja kununua kwako na pia atawaambia wenzake wote wawe wanakuja kununua kwako.
 
Huu ushauri mzuri mkuu nitaufanyia kazi siku nikikamilisha hlo duka nitarudi kwako
 

Salute. Uko sahihi 100%
 
Vipi location ya mwanza inalipa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…