Nina $ 23,000 ila sijui biashara gani inanifaa

Nina $ 23,000 ila sijui biashara gani inanifaa

Kama ni hela ya pension ndo unategemea ufanyie biashara baada ya kustaafu....dont hiyo hela ndogo kwa biashara kwa wakati huu utakufa kwa frustration na stress think twice
Unajua ni bora ujarbu ili uone nini matokeo badala ya kuziweka ndani hakuna matokeo kama umefel au la
 
Hii inakuwaje mkuu toa maelezo
Ni tovuti yakuuza bidhaa asili za kitanzania(made in Tanzania) pia ni maalumu kwa wafanyabiashara ambao wapo Tanzania.

Kazi yetu nikuhakikisha pesa yamnunuaji haipotei na bidhaa ya muuzaji haipotei wanapofanya biashara.
 
Kwa hiyo pesa usiitetemekee sana wala kuiendea pupa kumbuka idea nyingi mpya hufa hasa unapoanza biashara, tafuta biashara ambayo ishaanza ufanye kazi.....

Namaanisha tafuta big companies yaani zile strong ambazo watu wananunua shares na bonds mfano kampuni ya sigara omba uwakala huko kwenye kampuni ya sigara Tcc alafu open branch uwe branch agent mkoa kama simiyu, lindi, manyara ukiwa Kama wakala wa sigara.

tcc Ni kampuni kubwa haijawahi kupata wapinzani na bidhaa zake zinatoka sana ambazo Ni sigara sm, sport, safari, club, embassy n.k wao kama kampuni watakupa support sana uko baadaye ndiyo uje ufungue biashara yako, ukashindwa sigara nenda bia tbl, au fungua ofisi kubwa uwe wakala wa huduma za kifedha, pia wakala wa kampuni kubwa za bima insurance companies, au ingia kwenye uwakala wa bidhaa za cements, bati, na vifaa vya ujenzi....

mkuu yangu ni hayo ningekuwa Mimi ningeanza hivo usiende njee bongo bado fursa zipo kuliko huko.
 
M
Kama ni pesa huitegemei kwa chakula basi ingia Zanzibar, tafuta kampuni ya utalii ongea nao ziko nyingi haswa zenye magari ya kukodisha mkubaliane bei huwa sio chini ya laki tano kwa mwezi kama utampabdereva moja moja au inaweza fika dollar 30 kwa siku kama kampuni wataichukua maana wao wanakodisha kwa dollar 50 mpaka 60 kwa siku. Ukishapata kampuni sasa nunua alphard 3 kila moja Zanzibar haizidi milioni 12 mpaka na usajili hapo pia unaweza changanya magari ukawa na ya aina tofauti ila alphard isikose ndio habari ya mjini kwa sasa kwa kampuni ikiwa sambamba na prado tx (model flani ya kati hivi sio old ila prado ghari wewe chukua gari zisizidi m12), unaweza chukua Alphard na suzuki vitara au na toyota hizi size ya suzuki vitara. Kwa kila mwezi hutokosa 1.5m sasa sio ya kula hiyo unakusanya unaongeza magari hapo inamaana kila miezi 6 unaongeza gari moja zikifika kumi basi zinatosha, usihofu kuhusu kuharibika barabara za zenji nzuri utafanya kazi ya service tu ambayo kwa mwezi ni kumwaga oil pekee ndio kinafanyika huku. Wakati ukiwa umezikodisha kwa mtu fungua website anza kutafuta wageni mtandaoni na kukodisha magari kwa wahitaji wazawa na wageni, basi utafurahi mwenyewe.

Kwanza uje utazame fika pale Forodhani kuna kijiwe cha madereva tax, wale ndio wanabeba watalii huku watakupa abc zote. Kuna mtu nimesomea nae primary yaani ni mate wangu mpaka umri kazi yake ndio hiyo now anamalizia ujenzi wa nyumba yake ya milioni 200 so nikikueleza iko hela tambua iko tatizo la watu huwa mitaji na wewe mtaji huo unao. Nimekuchagulia zenji sababu barabara nzuri, kuna bahari sio rahisi watu kuvusha gari kwa nia ya kuiba, wengi wanakuja zenji kutalii hivyo wazawa na wageni wanakodisha sana magari sio bara mpaka upate kampuni ndio watakodisha gari kwako.
Ahsante sana
Mkuu unamshauri anunue magari kwa ajili ya kusafirisha watalii Zanzibar au vipi ?
 
Mkuu inategemea uko location gani.
Ila Kama upo dar au dodoma biashara rahisi na isiyooza ni ya vifaa vya ujenzi.

Ingekuwa Mimi ndio ww na Nina mtaji Kama huo nisingeumiza kichwa.

Ningechukua milioni 20 nikaanzisha hardware nje ya mji maeneo Kama kiluvya,goba,madale,vikindu n.k.

Halaf ile m 30 ingekaa tu kwenye akaunti wakati huo naisoma biashara inakwendaje?

Yaani wala usijiingize kwenye mabiashara makubwa yanayohusisha vibali vya maliasili au vibali vya kusafirisha nje ya nchi,utajikuta hela imepukutika wakati hata hyo biashara haijaanza kufanyika.

Milioni 50 Ni hela nzuri ukituliza kichwa lakini pia ni hela ndogo ukibugi utajikuta inakupita Kama upepo.
sure vitu vidogo ndo vina chance kubwa ya kudevelop kama vikisimamiwa vizuri sema
 
Ni tovuti yakuuza bidhaa asili za kitanzania(made in Tanzania) pia ni maalumu kwa wafanyabiashara ambao wapo Tanzania.

Kazi yetu nikuhakikisha pesa yamnunuaji haipotei na bidhaa ya muuzaji haipotei wanapofanya biashara.
Nmejaribu kitembelea na nimeilewa inalenga nini
Ni kazi nzuri na imesimama,
Ni vyema nawezq kununa bidha gani ikanitoa kwa mkoa wa mwanza

..ila mimi ni marekani,huwa natumia amazon nq wish......
 
Pesa za dili unazipata kwa mkupuo mmoja hafu unajikuta huna akili ya kuzifanyia lolote.
Wanajamii nimekuwa na wakati mgumu wa kuamua kufanya biashara gani itakayonifaa nitakapoamua kuacha kuangaika kwenye kazi za watu,

Nahisi pesa nilionayo($23,000=milioni 50 hivi za shilingi) inafaa kuwekeza ila nakuwa na wakati mgumu wa biashara hipi inafaa kulingana na pesa nilionayo au njia zipi nipitie ili niwe na mafanikio katika biashara yangu

Kwa mwenye kuwa na uelewa au uzoefu na maswala ya biashara na ushauri wa mambo haya anaweza kunishauri nipite njia zipi au nini nifanye kuwa bora katika biashara yangu ya aina yeyote ninayotaka kufanya

NINAWAKARIBISHA WAKUU.
 
Kwa hiyo pesa usiitetemekee sana wala kuiendea pupa kumbuka idea nyingi mpya hufa hasa unapoanza biashara, tafuta biashara ambayo ishaanza ufanye kazi.....

Namaanisha tafuta big companies yaani zile strong ambazo watu wananunua shares na bonds mfano kampuni ya sigara omba uwakala huko kwenye kampuni ya sigara Tcc alafu open branch uwe branch agent mkoa kama simiyu, lindi, manyara ukiwa Kama wakala wa sigara.

tcc Ni kampuni kubwa haijawahi kupata wapinzani na bidhaa zake zinatoka sana ambazo Ni sigara sm, sport, safari, club, embassy n.k wao kama kampuni watakupa support sana uko baadaye ndiyo uje ufungue biashara yako, ukashindwa sigara nenda bia tbl, au fungua ofisi kubwa uwe wakala wa huduma za kifedha, pia wakala wa kampuni kubwa za bima insurance companies, au ingia kwenye uwakala wa bidhaa za cements, bati, na vifaa vya ujenzi....

mkuu yangu ni hayo ningekuwa Mimi ningeanza hivo usiende njee bongo bado fursa zipo kuliko huko.
Vizuri mkuu,inagharimu shi ngap kuwa wakala wa campuni moja wapo tajwa hapo juu na vipi wewe unapata faida
 
Mkuu ukiwa unasubiria biashara ya kufanya chukua Dola 500 leo Man City (win)
Liverpool (win)
Man U (win)
Barcelona (win)
Chelsea under 4.5
Spurs under 4.5
Newcastle under 3.5

Asbh una $6000
 
Back
Top Bottom