Nina chuki na wanaopendana

Nina chuki na wanaopendana

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
Mtu na mwenzi wake wakiwa wanapendana mi nachukia kwelikweli, wakiwa kwenye migogoro naona rahaaaa mustarehe.
Sijui ntakuwa nasumbuliwa na ugonjwa gani?
 
wewe lazima utakuwa na kichaa cha mimba, hebu jifanyie diagnosis
 
Mtu na mwenzi wake wakiwa wanapendana mi nachukia kwelikweli, wakiwa kwenye migogoro naona rahaaaa mustarehe.
Sijui ntakuwa nasumbuliwa na ugonjwa gani?

mwanaume una gubu wewe.........
 
Una matatizo ya kisaikolojia
haiwezekani mtu na akili zako timamu ufurahie migogoro ya watu
 
Mtu na mwenzi wake wakiwa wanapendana mi nachukia kwelikweli, wakiwa kwenye migogoro naona rahaaaa mustarehe.
Sijui ntakuwa nasumbuliwa na ugonjwa gani?

Duniani kuna mambo, utakuwa una tatizo wewe si bure yaani wewe watu wakipendana unachukia na unapata faida gani ukichukia, utakufa siku si zako kwa stress maana huko ni kujitengenezea pressure zisizokuwa na maana yoyote kwa kuwachukia watu.
 
Mtu na mwenzi wake wakiwa wanapendana mi nachukia kwelikweli, wakiwa kwenye migogoro naona rahaaaa mustarehe.
Sijui ntakuwa nasumbuliwa na ugonjwa gani?

Hebu tuambie vizuri, hicho kinachokufurahisha wakigombana ni nini na kinachokukera ni nini?? Isijekuwa ndio nyie mnaotega midomo kama vikinda vya njiwa kungoja wengine wateme na nyie mnyakue, hebu tuweke sawa hapa mpwa.
 
Mtu na mwenzi wake wakiwa wanapendana mi nachukia kwelikweli, wakiwa kwenye migogoro naona rahaaaa mustarehe.
Sijui ntakuwa nasumbuliwa na ugonjwa gani?

Duh unaroho ya kwa nini kisheenziii halafu hujawahi kupendwa.
 
inawezekana ni aina ya familia na malezi uliyopata ukiwa mtoto, yawezekana umeshuhudia magonvi na mafarakano matupu katika ukuaji wako wote ndo maana hujui maana ya kupenwa na kupendana. si kosa lako, tafuta usaidizi.
 
utakuwa unahitaji mtu akupende, kam ni wa kike basi tafuta wa kiume and vrse vesa ni tru
 
Back
Top Bottom