Nina deal vipi na ndugu wanaojihisi wapo enitled na pesa zangu, kujitamba kwamba wanajichotea tu

Nina deal vipi na ndugu wanaojihisi wapo enitled na pesa zangu, kujitamba kwamba wanajichotea tu

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Entitlement kwa ndugu wa kiafrika ni tatizo kubwa sana, mtu anajihisi kwamba kwavile ndugu yake kafanikiwa basi ana haki ya kupata sehemu ya mafanikio ya ndugu yake, nadhani hata wachezaji wengi wa kiafrika wamelalamika hili jambo kwamba ndugu wanahizi matatizo yao yote inabidi yashughulikiwe na ndugu yao anaecheza ulaya.

Tukija kwa upande wangu niliweza kuajiriwa taasisi flani ya kiserikali ambayo ina jina kubwa tu na vichwani mwa watu wanaichukulia kama taaisi inayolipa sana ila kwakweli mishahara ni mizuri ila sio kama watu wanavyoikuza sana.

Sasa kinachotokea ni kwamba yani ndugu wapo entitled sana kuniomba misaada kuzidi uwezo wangu kwa kipato, wao sijui ni nani aaliwadanganya nalipwa milioni 5 kila mwezi mshahara na posho basi imekuwa kazi kweli kweli, uhalisia ni kwamba kila mshahara baada ya makato + posho mwisho wa mwezi nabaki na 2.4, kitu pekee ambacho kimenipunguzia mzigo ni kwamba nyumba hainiumizi kichwa kichwa, mzazi aliwahi kuwa nazo hapo zamani, nilipewa moja ya urithi ilikuwa bado haijakamilika finishing chache sana nilihamia hivyo hivyo huku nazimalizia mdogo mdogo.

Hio 2.4 kwa usawa huu ukiwa na familia yako amini kwamba ni kiasi kidogo sana ukisomesha watoto shule za private, uwe na kigari chako kinachojitaji mafuta, matumizi ya nyumbani, hapo bado unajitolea kusomesha ndugu ehhhh !!!

Unajikuta mtupu lakini nao ndugu simu haziishi tu, tena mbaya zaidi wanajipiga vifua eti wanajichotea tu.

TATIZO LANGU SIO KUSAIDIA BALI NI KWAMBA MISAADA NAYOTOA HAIZALISHI CHOCHOTE, MTU WAWEZA MSAIDIA ANAENDA KULIA BATA MSAADA UNAOMPA, NI KWELI INABIDI TUSAIDIE NDUGU LAKINI MISAADA IWE NA LENGO LA KULETA MAENDELEO YA MUDA MREFU NA SIO RAHA ZA MUDA MFUPI AMA MATUMIZI AMBAYO YATAJIRUDI UPYA BAADA YA MUDA MCHACHE, UNASAUDIA MTU HATA LAKI 5 YEYE HAJIONGEZI HATA AENDE AFUNGUE KAMRADI AANZE KUSAKA MAISHA, INAISHIA YOTE KWENYE NGUO, KINGAMUZI, BANDO, POMBE, N.K.
 
Saidia ndugu achana na malaya
Unasaidia ndugu lakini inabidi uangalie unachosaidia kinazalisha ama kinaenda tu ??

Ukisaidia ndugu na unaona unachomsaidia kinamletea maendeleo unapata hata motisha umsaidie zaidi ili ajitegemee

Sasa unamsaidia ndugu na hazalishi chochote huko ni kumwendekeza awe tegemezi.

Tutumie sana akili tunapofanya maamuzi, dunia ya sasa sio kama zamani tumeelimika, zamani ilikuwa rahisi hata kumuambia mtu duniani tumekuja kupita tu vyote vitapita vasi mtu anaweza kuridhika kuishi maisha ya kimaskini ila sikuhizi watu wameamka kwamba duniani tumekuja kuishi na tupambane na vitu vitupitie njia zetu hata kama vitapita yukiondoka
 
Muda umebadilika sasa, ndugu waanze kuwekewa masharti misaada wanayopewa wajiongeze uwasaidie kujitafutia vipato vyao.
Weka msimamo kwamba unatoa ela kwa ajili ya biashara tu na sio vitu vingine! Ita waambie wakupe mawazo ya kibiashara ili uwape mtaji na ukishawapa mtaji usiwape tena pesa mpaka waeudishe pesa uliyowapa kama mtaji.

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
 
Hi ishu sio ya ndugu TU,Hata marafiki pia.

yaani kukujua Siku mbili tatu, tayari keshakuweka kwenye Bajeti ya matatizo yake yote in the future.

Na akipata tatzo anajua kwako Ni uhakika, sababu TU anayajua mafaniko yako flan flan yanayoonekana kwa macho ya wengi.

Unashangaa Akikupigia umpe pesa, usipompa au ukamwambia Sina ananuna,

yaan analazimisha matatzo yake yote yawe yenu nyote
 
Japo ka salary kangu ni kadogo sana hakafiki hata million ila kuna kijana wangu mtoto wa mamdogo wangu , namsaidia sana ili amalize masomo yake ya udaktari ila kila siku huwa namkumbusha siku akifanikiwa akumbuke kusaidia wengine.

Hivyo basi

Ndugu zako walipambana sana mpaka wewe kufika hapo ulipo tangu ukiwa mtoto, lazima wajivunie damu yao.

Kumbuka pia siku ukiwa mahututi watakao tafutwa ni hao hao ndugu zako.

Saidia kiasi hasa kwenye mahitaji kama vile magonjwa, elimu,ndugu anahitaji mtaji, connection ya kazi N.k

Wapende ndugu,saidia kiasi na ipende zaidi familiar yako.
 
Tatzio nadhan linaanzia Kwny mindset,

Ujamaa umetuathiri sana,
Suala la kujitegemea limekua mtihani sn

Kuna Watu Wanadhan matatzo Yao Ni lazma yatatuliwe na ndugu zao, Tena kwa lazima.

Ndo Yale mtu anaboronga kusud,
afu mzgo wote wanaangushiwa ndugu,

Kama una ka-akiba kako flan unataka ufanye maendeleo yako, kote kanaishia kwa ndugu ambae kafanya ujinga wake kusudi TU.
 
Waambie wapambane wakaze mattyakko hakuna maisha rahisi wala maisha ya bure kwa kuwa ndugu yao una vijisenti.
Maandiko yanasema asjyefanya kazi na asile sasa wanataka wale nini kama hawafanyi kazi na kupata pesa zao?
Acha kulea ujinga saidia kadiri ya uwezo wako na moyo wako ila kwenye ukweli waambie maana utawasaidia kubadilisha fikra na mizatamo ya kupenda vya bure bure.
Otherwise wape nauli waende Mombasa kulelewa..))
 
Watishe uwaambie wewe ni Frimasoni umeambiwa uanze kuwatoa kafara wote wanaokuomba hela, wakiendelea kukusumbua mpoteze mmoja kwenye mazingira ya kutatanisha
 
tatizo its yo lifestyle, unaishi vipi n watu wanaokuzunguka, tuanze hapo walijuaje unalipwa mili 5?? unajikweza unazo, ukitaka kua mchoyo ishi na watuvkwa kujifanya upoupo yan wewe lia lia tu hujulikani unacho huna
 
Wengi wakati mkisoma hakumbuki wakati mnalia Lia njaa Kwa ndugu.
Hapo tayari kuna specific na limited time ya kusaidiwa kwamba unasaidiwa wakati "Unasoma tu" baada ya hapo una gangamala.

Sasa wewe kwa vile ndugu waliku somesha, ndio watake uwasaidie throughout their Life...

Na wao ndugu watasaidiwa kwa specific time only, Sio kila wakati.
 
Siku watolee uvivu kunywa pombe utapata cha kuwaambia
 
Back
Top Bottom