Nina gari canter, Je niifanyie biashara gani?

Nina gari canter, Je niifanyie biashara gani?

Eñdelea na utaratibu wako kama hiyo week end unapata hela ya maana.
Baadae utakapopata mtu mwaminifu fanya nae kazi.
Kuhusu kazi ni mizigo ya sokoni, kumbebea samani mtu anayehama nà kubeba tofali, mchanga, cement na vifaa vya ujenzi kwenye site za wanaofyatua tofali.
Usiuze komaa nayo, hata kama inakuingizia hela ndogo si mbaya.
 
Kata kata uuze vyuma chakavu,spare used itakulipa ,kama utaki kumpa Dereva.
 
Ulinunua gari kwa malengo gani? Hadi hujui ufanyie nini!
 
Naona mkuu
Unashindana Na utawala wa awamu ya tano

Watu wanataka ajira wewe unabana
Acha watu wajipatie kipato

Ndio Moja ya Tanzania ya viwanda
 
Gari ni langu naendesha wikend mpaka wikend. Je nfanye biashara gani?
Huwezi fanya biashar ya gari kwa kuliendesha gari weekend mpaka weekend! Swala ikatie bima kubwa hiyo canter alafu tafuta dereva mzoefu umkabidhi afanye biashara ya kubeba mizigo au maji... Kama ingekuwa tipper ndio ingekuwa poa ziaid. Ila hata hivyo hivyo, dili za kubeba matofali sio haba.
 
Nashindwa kushauli..
Gari ina miaka minne!
Lengo la kununua gari ni nini?
Thamani ya hilo gari na hela unayo pata vinaendana?
Je kwa pesa uliyo nunua gari huna unacho kijua zaidi ukifanya kwa hiyo pesa unaweza pata pesa zaidi ya ulizo wekeza kwenye Gari?
Cha kusema uza gari fanya biashara nyingine ya mtaji Mdogo yenye faida kuliko hilo gari kwakua hiyo biashara imekushinda ,vinginevyo utakuwa unafanya kazi ya kuonekana una gari ila siyo masilahi .
 
Mimi namiliki gari aina ya center yenye uwezo wa kubeba tani 2. Nimeajiriwa na kampuni za bandarini hivyo natakiwa kila Siku ofisini gari nmepaki tu nyumbani. Wikend napata muda wa kutumia gari langu kwa shughuli za uzalishaji . Sihitaji kumpa dereva katikati ya wiki aniletee hesabu ninaendesha mwenyewe wikend tu. Je, niifanyie biashara gani? Nipe dili au toa maoni yako.
Mm n mfanyabiashara wa kuni mwenye vibal toka maliasili ila cna gar ..ka ungeweza tungeshirikiana inalipa sana
 
Hiyo ni straight forward.
Kazi ya canter ni kusafirisha mizigo
Tafta company au kuwa distributor wa cmpany ambapo utakuwa unalipwa na hata kujilipa kwa kufnya part-tme kazi zako
 
Hiyo canter unauza mkuu? Kama unauza nitumie niione, and then tuongee biashara
 
Maelezo yako ni mazuri njoo hapa kariakoo kuna Madreva uingie nao mkataba uwe unakula mpunga wako kwa week gari kukaa tu nyumbani majanga kwa uzoefu wngu unaweza kupata mpaka laki nne,kama uko tayari nicheki 0684239106
 
Wanabebea nini?
 
Mimi namiliki gari aina ya center yenye uwezo wa kubeba tani 2. Nimeajiriwa na kampuni za bandarini hivyo natakiwa kila Siku ofisini gari nmepaki tu nyumbani. Wikend napata muda wa kutumia gari langu kwa shughuli za uzalishaji . Sihitaji kumpa dereva katikati ya wiki aniletee hesabu ninaendesha mwenyewe wikend tu. Je, niifanyie biashara gani? Nipe dili au toa maoni yako.
vulia samaki, itapendeza zaidi.
Tafuta kampuni ya uchukuzi muingie mkataba, wakulipe Kwa mwezi , vinginevyo acha kazi
 
Back
Top Bottom