Nina Gari lenye Friji, natafuta kazi

Nina Gari lenye Friji, natafuta kazi

Lesa360

Member
Joined
Jun 13, 2020
Posts
22
Reaction score
38
Kuna gari nnayo hapa sasa natafuta tenda za nyama au kubeba mboga mboga au vitu ambavyo vinahitaji friji na tenda iwe ya Kila siku au mwezi au hata alie na Connection ya kazi hizo tunaweza kuwa wote kwenye gari hyo
Screenshot_20221128-162430.jpg
Screenshot_20221128-162413.jpg
 
Kuna gari nnayo hapa sasa natafuta tenda za nyama au kubeba mboga mboga au vitu ambavyo vinahitaji friji na tenda iwe ya Kila siku au mwezi au hata alie na Connection ya kazi hizo tunaweza kuwa wote kwenye gari hyoView attachment 2431171View attachment 2431172
Mkuu nakushauri uwe na kampuni ya usafirishaji kisha uanze kuomba tenders za usafirishaji kwa hawa watu wa catering, mashule, taasisi mbalimbali pamoja na kuuza ice cream, kisafirisha samaki za baharini kwenda mikoani au kutoa samaki za maji baridi kuja Dar es Salaam. Fursa ni nyingi ila usitegemee zikufuate kama hujajitengenezea thamani ya biashara yako.
 
Bonge la wazo ila unaanzisha kampuni kwa gari Moja? Procedure zake unazijua? Na ukiwa na kampuni charges za Kodi ni kubwa kuliko kufanya kazi personal
 
Japo sina connection , ila niseme tu "Kila la Heri kwako mdau. Mambo yako yasonge.
 
Unaacha kuwaza core point ya Thread unakimbilia kwenyeabishano yasiyo na tija.... Kuweka picha ya Japan haimaanishi gar Iko Japan... Huna connection kausha sio lazma Kila kitu uchangiee
Kiongozi, usi-criticise watu kwa namna hiyo..!! Usisahau watu washatapeliwa sana tu kisa wali-concentrate kwenye core point ya jambo husika..!! Acha watu wajitoe wasiwasi
 
Kiongozi, usi-criticise watu kwa namna hiyo..!! Usisahau watu washatapeliwa sana tu kisa wali-concentrate kwenye core point ya jambo husika..!! Acha watu wajitoe wasiwasi
Unajua Usipende kukaza ubongo kwenye Kila kitu..... Ndio maana mnatapeliwa sababu Kila kitu unawaza utapeli... Wewe kwenye ishu yangu hii unatapeliwa wapi? Gari yangu mm naomba tu kupata mawazo na connection ambazo huusiki au hata kama utanipa nikifika huko Hamna kupeana pesa Wala nn sana sana mm ndo labda ntapeliwe lakin mtu hata uwazi kwa kina unaenda kwenye vitu kama picha una doubt huo ni ujinga.... Wenye msaada wametoa mawazo Yao wamekausha ndio uungwana na tayar nshapata msaada lakin sio hizi pumba mnaleta nyie
 
Utajiri huo uko wazi kabisa, nenda Mto ruvu ndanindani kuna sehemu wanatoa samaki kambale bei rahisi mno kule hawana barafu kipindi kama hivi ambacho mboga ni shida utapiga pesa sana maana kwa wiki wewe utapiga kazi mara nne soko lipo riverside kwa chini kule wanunuzi wa jumlajumla utawapata wenye ofisi zao unakula cash unaondoka yaani rahisi sana
 
Fuatilia issue ya maziwa fresh upande wa mkuranga huko au ikwiriri katafute connection pale riverside kwa wauzaji wa jumla kafanye tafiti kwanza, kote huko ni pesa tupu hakikisha umefanya connection pande zote wanunuzi na kule unakotoka mzigo uhakikishe mzigo wenye ubora unaenda saa kumi jinoni shambani wanaandaa mzigo saa tisa unakua sokoni kumi na mbili umemaliza biashara nenda kalale nancash yako unajiandaa tena soko kubwa ni riverside pia tafuta wauzaji wa jumla
 
Utajiri huo uko wazi kabisa, nenda Mto ruvu ndanindani kuna sehemu wanatoa samaki kambale bei rahisi mno kule hawana barafu kipindi kama hivi ambacho mboga ni shida utapiga pesa sana maana kwa wiki wewe utapiga kazi mara nne soko lipo riverside kwa chini kule wanunuzi wa jumlajumla utawapata wenye ofisi zao unakula cash unaondoka yaani rahisi sana
Kaka naomba maelezo zaidi.... Naweza kuja Pm walao nipate namba tuongee vizuri
 
Nenda Rukwa sumbawanga sehemu inaitwa mtowisa kachukue samaki wabichi perege wanaofanana na sato, watunze vyema piga gia hadi Tunduma kauze jumla pale unakamata cash yako unaondoka tena hasa kipindi hiki cha mvua biashara ni nzuri kule samaki wapo wengi kafanye tafiti pia tunduma uulizie samaki wabichi wanauzwa wapi na uende huko mtoiswa uone mzigo utavushaje kufikia gari
 
Nenda mtera au migori kachukue samaki wabichi perege wewe unacheza na Dodoma na iringa ndio masoko yako unahakikisha kwa wiki unapiga ruti tatu hadi nne bahati nzuri mtaji sio mkubwa sana , unakua na barafu zako plus gari lako ni pesa tu mwaka mmoja watakutafuta hawakupati kikubwa mzigo uwe na ubora kafanye tafiti pia migori au mtera then fika sokoni iringa mjini, mafinga au Dodoma ujue mzigo utauzia wapi
 
Back
Top Bottom