Nina gari yangu vitz imeanza kuishiwa maji na kuchemsha

Nina gari yangu vitz imeanza kuishiwa maji na kuchemsha

Umesema kweli. Kuna mtu namfahamu mafundi wake waliwahi kumrubuni akatoa coolant na kuweka maji ya uhai, kwa ushauri kuwa maji ya uhai ni mazuri kuliko coolant, wakati kumbe siyo. Kumbe walikuwa na mpango wa baadaye kuja ku-temper na engine ya gari yake, walishaisikiliza kwenye muungurumo na namna gari inavyotembea, wakajua injini ya gari lake ni nzuri sana. Kilichotokea baada ya kubadilisha coolant, water pump ilikufa ikabidi anunue nyingine, na hatimaye akarudi tena kwenye coolant. Sasa hivi walikuwa na mpango wanamshauri abadilishe Gasket za injini, wakati injini ina nguvu sana na haina tatizo jingine lolote. Mafundi hawa wana mtandao wao pia kwa kushirikiana na kule ambako huwa anafanyia service gari llake.

Kuwa mwangalifu sana na ushauri wa watu na baadhi ya mafundi, hasa wasiokuwa mafundi wa gari lako na unapoona gari lako lina tatizo, mpelekee fundi wako na usibadilishe mafundi wa gari. Uwe na fundi mmoja wa gari milele, na ufanaye service kwa fundi mmoja milele, usibadilishe
Na unaweza kuwa na fundi wako wa milele akawa anakupotosha zaidi kikubwa ambacho mm kama muuzaji wa hivyo vilainishi ni wewe mwenye gari yako kujua na kusoma manual book za gari yako inataka uweke spare au lubricant ya aina gani full stop maana huyo mtengenezaji wa gari ndo anajua aliweka nn kwenye engine yako na kwann anakutaka wewe uweke hicho kitu anamaana kubwa sana lakini sisi wabongo wengi tumekua wabishi sana utasikia naweka tu kwa kutumia siku mbili tatu kitanisogeza kumbe hizo siku mbili umetengeneza ugonjwa mgumu sana kwenye gari yako
Na muwe makini sana na hivi vitu ambayo ni vilainishi ni mhimu sana kwenye gari kuliko kitu chochote na imeandikwa tumia maji kwa emergency tu pale ambapo umekosa coolant ila ukifika sehemu ukaipta coolant toa maji weka hata kama umeipata baada ya dakika kumi
 
Fuata yafuatayo!!

Kabla ya kuwasha gari weka maji na utazame kama yanapungua.
Yakiwa yanapungua tazama wapi yanapitia hasa angalia zile kava za rejeta ni za plastiki huenda zimeweka nyufa.

Kama hayapungui
Funika mfuniko na washa gari kisha piga less kwa muda kama wa dkk 5 hadi 10
Tazama mfuniko wenyewe au endelea kutazama kava.

Kama hayapungui,endelea kupiga less na sikiliza kama feni inapoza rejeta.

Tazama pia mtungi wa hifadhi ya maji kama unatunza maji ya kureplace au kupoza rejeta.

Angalia gear box yako inabadili gear inavyostahili!!!
Kama la badili geabox oil huenda injin na geabox haziwasiliani ktk mwendo.

Je rejeta ni safi??
Huenda njia zimeziba hivyo mzunguko wa maji ktk rejeta ni mdogo.
Asante.Mawazo yangu ni hayo.



Nimejifunza kitu. Mungu akubariki
 
Back
Top Bottom