DR HAYA LAND
JF-Expert Member
- Dec 26, 2017
- 23,928
- 63,499
Haya bhana, ila shemeji kwa nani 😁🤣Intelligent businessman hujui tu wewe ni my best friend na sikujuagi ila basi tu siwezi kukudharau shemeji yangu
Tumia amoxicillin, tridamol, na trinidazole uta pata nafuu kubwa Smart ContractKuharisha damu ni swala moja ila tumbo kutokuuma hilo ni swala tofauti kabisa.
Kwa uzoefu wangu utotoni niliwahi kuumwa Amoeba ila sikufika hatua ya kupata choo chenye damu lakini tumbo lilikuwa linauma kwa kukata mpaka unaenda chooni unatembea ukiwa umeinama, hivyo kwa maelezo yako sidhani kama ni Amoeba.
Pia sidhani kama ni Ulcers maana mpaka muda huu ninaandika ninazo na huwa zikichachamaa tumbo linauma unaweza kupiga ukelele wa kuomba msaada, pamoja na hayo sijawahi pata choo chenye damu hivyo sidhani kama ni Ulcers.
Kuhusu kichocho sina uhakika kwa sababu sina experience nacho ila ninachojua dalili moja wapo nikutoa mkojo uliochanganyika na damu kwa sababu wataalamu wanadai kichocho ni UTD's (Urinary Transmitted Disease) kwa mantiki ni kwamba zinaaffect njia ya mkojo sasa kwa haja kubwa sijajua, labda tusubiri wataalamu.
Acha uchizi umeshasau na huku nimesikia umempigisha mimba 2 aisee (utasikia acha matusi wewe ni kupigwa mikwara hadi mwaka uishe )Haya bhana, ila shemeji kwa nani 😁🤣
Tangu jana nimekuwa nikiharisha damu. Sina maumivu yoyote ya tumbo na wala sipandishi homa.
Leo nimeenda hospitali wamenipa dawa za minyoo. Je minyoo inaweza kusababisha uharishe damu?
Au ndio nimekutana na daktari kihiyo?
Sina mtoto wangu wa damu, nina my last sibling.Acha uchizi umeshasau na huku nimesikia umempigisha mimba 2 aisee (utasikia acha matusi wewe ni kupigwa mikwara hadi mwaka uishe )
Thanks brohTumia amoxicillin, tridamol, na trinidazole uta pata nafuu kubwa Smart Contract
Hapana. Kama ni tapeworm (kwa kiswahili ni Tegu),Tafuta Lodwaa au Ngetsi(botanical name :embelia schimperi) na mchezo umeisha.Kwamba tapeworm!?taenia sollium!!?
Hiyo ni noma Haina tiba , surgery tu ya intestine!!
DuhI miss u mganga wangu wa ukoo National Anthem aisee happy new year we jamaa nimekumiss tulichinja mbuzi ila hujaconnect na mie uje na familia ukatambikiwe uache kuzeeka mapema uwe kijana upige pipe za michepuko hatari .
Waende wengine labour uadopt watoto wawatuSina mtoto wangu wa damu, nina my last sibling.
👉Ndo namchukulia ka mwanangu.
Unaharisha damu unakuja kuanzisha uzi jf, kweli wewe mwamba, unaharisha damu unaenda dispensary ama private kweli wewe mwamba. Huyu dakitari chapa vibao kabisa utakuja shtuka bandama lote halimo tumboni we chekelea tuTangu jana nimekuwa nikiharisha damu. Sina maumivu yoyote ya tumbo na wala sipandishi homa.
Leo nimeenda hospitali wamenipa dawa za minyoo. Je minyoo inaweza kusababisha uharishe damu?
Au ndio nimekutana na daktari kihiyo?
Asante sana kwa chapisho bora kabisaHapa hutegemea na aina ya damu(iliyoharibika vs mbichi). Kama ni damu mbichi/nyekundu inatoka kwenye Lower Gastrointestinal Tract (LGI).
Njia ya chakula imegawanywa kwenye maeneo mawili:
1: Eneo la juu/upper GI
2: Eneo la chini/ lower GI
Damu inayotoka juu ya tumbo la chakula huweza kumeng'enywa na enzymes na hivyo kutoka ikiwa imeharibika (altered). Wakati damu inayotoka baada ya tumbo la chakula kurudi chini ndo huweza kutoka ikiwa fresh/ nyekundu.
Kwa kuwa hakuna maumivu, vitu vifuatavyo vyaweza kuwa ni visababishi:
A: Diverticular disease.
Huu ni mfuko kama pochi unaoweza kujitokeza kwenye utumbo wako. Pakitokea shida ya maambuki, tatizo hilo hujitokeza.
B: Inflammatory bowel disease (IBD).
Hii huusisha ulcerative na Crohn's disease, ni magonjwa yanayohusisha utando wa utumbo na misuli ya utumbo pia.
C: Proctitis.
Hii huusisha kututumka kwa sehemu ya mwisho ya njia ya haja kubwa.
D: Tumors/uvimbe.
Uvimbe wowote unaoweza kujitokeza ndani ya mfumo wa chakula..
E: Colon polyps.
Mkusanyiko wa seli ndani ya utando na ukuta wa njia ya haja kubwa.
F: Hemorrhoids/Bawasiri.
Kuvimba kwa mushipa ya damu/veins kwenye sehemu ya mwisho ya njia ya haja kubwa.
G: Anal fissures.
Ni kuchanika kwa eneo la mwisho la njia ya haya kubwa.
H: Lower GI Ulceration
Vidonda kwenye eneo la chini la utumbo.
Kwa kuangalia idadi ya matatizo, huwa ni vyema kufanyiwa vipimo byema ili kung'amua chanzo na kiasi cha tatizo.
Suala hili kulingana na kiasi cha damu kinachotika, huweza kusababisha:
1: Upungufu mkubwa wa damu.
2: Shock
3: Kupoteza maisha
NB: Hakikisha unapata utambuzi sahihi wa chanzo cha damu kwa eneo hili. Hivyo, fika hospitali kubwa kwa uchunguzi na tiba zaidi.