Tangu jana nimekuwa nikiharisha damu. Sina maumivu yoyote ya tumbo na wala sipandishi homa.
Leo nimeenda hospitali wamenipa dawa za minyoo. Je minyoo inaweza kusababisha uharishe damu?
Au ndio nimekutana na daktari kihiyo?
Hapa hutegemea na aina ya damu(iliyoharibika vs mbichi). Kama ni damu mbichi/nyekundu inatoka kwenye Lower Gastrointestinal Tract (LGI).
Njia ya chakula imegawanywa kwenye maeneo mawili:
1: Eneo la juu/upper GI
2: Eneo la chini/ lower GI
Damu inayotoka juu ya tumbo la chakula huweza kumeng'enywa na enzymes na hivyo kutoka ikiwa imeharibika (altered). Wakati damu inayotoka baada ya tumbo la chakula kurudi chini ndo huweza kutoka ikiwa fresh/ nyekundu.
Kwa kuwa hakuna maumivu, vitu vifuatavyo vyaweza kuwa ni visababishi:
A: Diverticular disease.
Huu ni mfuko kama pochi unaoweza kujitokeza kwenye utumbo wako. Pakitokea shida ya maambuki, tatizo hilo hujitokeza.
B: Inflammatory bowel disease (IBD).
Hii huusisha ulcerative na Crohn's disease, ni magonjwa yanayohusisha utando wa utumbo na misuli ya utumbo pia.
C: Proctitis.
Hii huusisha kututumka kwa sehemu ya mwisho ya njia ya haja kubwa.
D: Tumors/uvimbe.
Uvimbe wowote unaoweza kujitokeza ndani ya mfumo wa chakula..
E: Colon polyps.
Mkusanyiko wa seli ndani ya utando na ukuta wa njia ya haja kubwa.
F: Hemorrhoids/Bawasiri.
Kuvimba kwa mushipa ya damu/veins kwenye sehemu ya mwisho ya njia ya haja kubwa.
G: Anal fissures.
Ni kuchanika kwa eneo la mwisho la njia ya haya kubwa.
H: Lower GI Ulceration
Vidonda kwenye eneo la chini la utumbo.
Kwa kuangalia idadi ya matatizo, huwa ni vyema kufanyiwa vipimo byema ili kung'amua chanzo na kiasi cha tatizo.
Suala hili kulingana na kiasi cha damu kinachotika, huweza kusababisha:
1: Upungufu mkubwa wa damu.
2: Shock
3: Kupoteza maisha
NB: Hakikisha unapata utambuzi sahihi wa chanzo cha damu kwa eneo hili. Hivyo, fika hospitali kubwa kwa uchunguzi na tiba zaidi.