Nina harisha damu yenye matone kama kamasi

Vincenzo Jr

Platinum Member
Joined
Sep 23, 2020
Posts
24,262
Reaction score
58,728
Shida ilinianzia jana jioni nikatanguliza choo cha kawaida baadae ikaanza choo chenye makamasi yenye damu shida Itakuwa Nini au ndio Dalili za kuvuta hizi wiki hii nimekuwa nikisumbuliwa sana na tumbo pia Nina vidonda vya tumbo ila sio chronic jana na Leo ninateseka sana soon nakufa 😭😭
 
Nendq hospital mkuu
 
Unapata na shida gani nyengine kabla ya hapo ?
 
Tangulia mkuu.
Chumvi umeila si haba.
Usisahau tu kuacha mirathi.
Buriani kamanda!.
 
Pole sana ndugu yangu. Tafadhali huu muda unaoutumia hapa nenda hospitali, ukija tena hapa uwe ni umetoka hospitali tayari.

Usiogope wala kukata tamaa, ugonjwa ni suala la kawaida ila ukifanya uzembe ndio hatari.
 
Bora uwahi hospital man isije kuwa vidonda vimetibuka
 
Ugonjwa wa kuhara (uliojulikana kama kuhara damu au kuharisha damu ) ni maradhi yanayotokana na machafuko ya ini ......( Kwa mujibu wa Wikipedia)

Huenda pia ikawa ni dalili ya vidonda vya tumbo vilivyo kwenye stage ya juu ( Kwa mujibu wa Dokta Mwaka)

Nashauri uwahi hospitali Kwa vipimo zaidi

Binafsi nakuombea upate nafuu haraka πŸ™πŸ™πŸ™πŸ™
 
Asante sana babu ukiona nimepotea jukwaani ujue nimevuta 😭😭😭😭
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…