Nina hofu huenda nimeambukizwa UKIMWI, Naombeni ushauri wenu jamani!

Nina hofu huenda nimeambukizwa UKIMWI, Naombeni ushauri wenu jamani!

Onguluo

Hauna ukimwi ndugu yangu....kama kwako imeshindikan kuonekana basi kwa huyo mama ungeonekana... magonjwa siku hizi ni mengi na yanatisha.. Huo ugonjwa wako hujakutana na mtaalamu wake. Nenda hospital kubwa ukahudumiwe vizuri...

Mimi nilikuwa na ugonjwa unanisumbua kila nikifanya vipimo naambiwa sina tatizo mpaka nkaamua kwenda kupima HIV lakini niko vizuri, mpaka juzi nimekutana na mtaalamu Prof. aliebobea kwenye magonjwa yangu na amegundua nina tatizo na nimeanza kutumia dawa rasmi ya huo ugonjwa....tafuta mtaalamu hasa!
 
Last edited by a moderator:
Hutakuwa wa kwanza kupata maambukizi, utapaswa kuishi kwa matumaini. Nasema hivyo kwa sababu unataka kuamini na kutuaminisha kuwa una maambukizi, itafaa ijilaumu sana kwani elimu juu ya njia za kujikinga dhidi ya maambukizi hutolewa mpaka kwa Wanafunzi wa chekechea sijui ulisafiri kwenda mars elimu ikakupita!!!!!!!!!
 
yani hujawahi kukutana na mpenzi wako kimwili, halafu unamvulia chupi janamke, nimekudharau sana, na ningekua na namba ya huyo mpnz ningemwambia akupige kibuti tu, huoni hata aibu lo!

Akipigwa kibuti kisha akuchukue wewe au?
 
Duuuuhh kwanza kupma ni jambo kubwa sana na pili ni vyema ukaendekea kujipa matumain more an more koz wengi walioadhrka hufa kwa stress na sio HIV soo tengua mawazo that unao songa mbele bhaana
 
Ukiona mtu anaenda kupima mara mbili mbili ujue kuna jibu analitafuta haya bhas unao.... Umeridhika inaonekana we sio player kabisa unauza mechi mda mfup hivyo unawaswas
 
Kinacho kutesa ni uoga wa ugonjwa "the fear of illiness"

~ni tatizo la kisaikolojia umejenga picha ya UKIMWI kwenye akili yako.hivyo hata ukipatwa na tatizo dogo la kiafya unalikuza kulingana na imani yako juu ya ugonjwa wa UKIMWI "beliefs"

~Jaribu kujiamini na kuikataa hali hiyo kwa kujenga fikra chanya...
UKIMWI siyo dengue ama ebola uuupate siku hiyo hiyo na dalili zionekane siku inayofuata

~nenda kapime afya yako kwa ujumla ujue chanzo cha tatizo...alafu urudi kutupa mrejesho hapa.
 
Magonjwa ya zinaa sio HIV pekee. Nenda ukapime hali yako ya kiujumla ya afya.
 
Virusi vinaweza kuonekana baada ya miezi mitatu, subiri kwa muda wa miezi mitatu baada ya tendo, kama muda huo umepita, umepima na umejikuta negative then you are negative. Ila umesema kwamba mlienda wote kupima na wote mkawa negative kwaiyo kama yeye hana then hawezi akawa amekuambukiza chochote, labda ni STI nyingine ambayo sio HIV, stop panicking. Play it safe from now on man,,,,
 
ucogope kijana hayo yapo, kwa kuwa tu ulikumbuka kutubu bwana yu pamoja nawe hivyo usiwe na woga wala hofu yoyote juu ya afya yako uko vzuri tu hata ucjal. Bwana akubariki. Soma Upate Ushindi,Isaya 53:3
 
Habari zenu, poleni na majukumu ya siku!

Ndugu zangu ni muda wa miezi mitatu sasa nikiwa katika hali ya sintofahamu juu ya afya yangu na nimekuwa katika depression kubwa sana..

Mimi ni kijana wa kiume nina umri wa miaka 30. Nina mchumba ambaye nimedumu naye kwa muda wa mwaka mmoja sasa, hatujawahi kukuta kimwili na binti huyo, tuko wilaya tofauti ndani ya mkoa mmoja.

Tarehe15 Novemba 2014, siku ya jumamosi saa moja jioni nilienda kwa mama mmoja ana km miaka 33 hivi ni anafanyabiashara ya asali hapa mjini.

Nilienda kutafuta asali mbichi kwa ajili ya kuchanganya na dawa ya vidonda vya tumbo. nikiwa ndani mwake nilishawishiwa na yule mama kwa namna nisiyojua nikajikuta nimefanya naye mapenzi (ngono zembe) na kibaya zaidi sikutumia kondom, ilikuchukua almost dk 2 kumaliza. Nikachukua asali yangu na kuondoka kwenda kwangu.

Nikiwa njiani majuto yakaanza na kujilaumu kwann nimezini na mtu nisiyefahamu afya yake bila kinga, nilipofika home nilipiga magoti na kumuomba Mungu anisamehe dhambi yangu. Nilifikiria kumpigia yule mama usiku huo ili nimuulize juu ya afya yake ila sikuwa na afya yake, nilazimika kutafuta namba zake na kumpigia simu usiku huo.

Nilimpigia simu nikamuomba aniambie iwapo kama yeye ni mgonjwa (Muathirika wa HIV) ili niwahi kuripoti hospital within 72 hrs. Lakiniyule mama aliniambia kwamba yeye ni mzima na hata nikitaka tukapime. Majibu yake yalinipa matumaini na nikaendelea na shughuli zangu za kila siku, baada ya muda ya wiki 2 net niliugua mafua makali sana makamasi mazito sana yenye mchanganyiko na damu na hata dawa za mafua nilizotumia hazikusaidia chochote!

Baada ya wiki 2 mafua yalikata, kichwa kikaanza kuniuma sana kuanzia kwenye paji hadi utosini km muda wa wk moja hv. kwakweli niliona dalili zilizonitisha, nililazimika kumuambia yule mama kwamba ameamua kuniangamiza maisha yangu kwa kunipa maradhi makusudi, yule mama alikataa kata kata kwamba yeye anajujua ypo vuzuri hata maradhi, kwamba n wasiwasi wangu tu.

Tarehe 02 January tulienda naye tukapima HIV lkn matokeo yakawa negative wote. hyo ilikuwa muda wa mwezi mmoja na nusu tangu nisex naye.

Baada ya majibu hayo nilijipa matumaini ya uzima lakini mpaka naandika uzi huu hapa mambo totauti kabisa nimeona dalili tofauti za kunitisha, mwili hauko vizuri kwa ujumla tatzo kubwa zaidi ni maumivu ya koo na kuvimba kwa tezi shingoni karibu na taya ni muda wa km wiki tatu tangu uvimbe uanze.

Nikijaribu kusoma makala kwenye google juu ya kipimo cha HIV na kufahamu iwapo umeathirika, ile makala inaeleza kwamba kuvimba kwa tezi shingoni (mtiko) ni njia mojawapo ya kutambua kuwa una HIV. njia ya pili ni kupima HIV test.

Leo 19 February 2015 nimepima HIV Hospital ya wilaya nikaambiwa ni Negative. Nashindwa kuelewa kwamba ni muda wa irus kuonekana kwenye vipimo ndo haijafika au namna gani? Kibaya zaidi tulipanga kuoana na yule mchumba wangu mwezi machi mwanzoni na ninashindwa kumueleza kuwa mi ni mgonjwa ili hali vipimo havioneshi kwamba mi ni mgonjwa, atasema ni mbinu ya kutaka kumuacha.

Jamani nifanye nini mie sitaki kumuangamiza roho isiyo na hatia. Naombeni ushauri wenu wanajf wenzangu.

Hivi unajua uoga unaua?
Kula nyama ya ng'ombe ugenini halafu mwenyeji wako chizi akudanganganye hiyo ni nyama ya nyoka uone kama hutaharisha kwa hofu mpaka uishiwe maji kama sio kufa.
 
Kapime mpwa hapo ndio jibu sahihi utalipata kuliko hivyo unateseka moto mbona sio dili tena siku hizi
 
Onguluo unajitesa bila sababu uoyote, hebu tulia ma urudie vopimo baada ya miezi mitatu, kama utakuwa -ve then utakuwa unasumbuliwa na matatizo mengine nje ya VVU.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom