Nina hoja fulani kuhusu ushambuliaji Simba SC

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
3,433
Reaction score
8,585
Ninakubali kuwa mabadiliko ya mpira wa kisasa yanahitaji mchezaji anayeweza kufanya kwa ufasaha kazi zaidi ya moja. Ninakubali na ninaheshimu sana hilo.

Kwasababu hiyo, mpira hautaki tena mikono ya golkipa tu bali unataka golkipa awe sehemu ya kiunganishi cha mchezo, awe mpiga pasi kama viungo tu.

Kwasababu hiyo, mpira hautaki tena mabeki wanaokaba tu bali beki anatakiwa ashambulie, apige pasi za mwisho na afunge kama tu viungo na washambuliaji.

Kwasababu hiyo, mpira haumtaki tena mshambuliaji anayefunga tu bali Unamtaka mshambuliaji anayefunga, anayekaba na kuwadhibiti mabeki.

Kwasababu hii Chris Mugalu amekuwa chaguo la kwanza mbele ya Meddie Kagere ndani ya Simba chini ya Didier Gomes. Ninakubali na kuheshimu sana hili, japo nina fikra tofauti kidogo.

Fikra gani tofauti unazo ?? Kazi ya mshambuliaji ni kufunga, na anahukumiwa kwa idadi ya mabao aliyofunga. Kama anaweza kukaba au kuchezesha timu, ni faida tu za nyongeza lakini Si busara sana kumuhukumu kwa vigezo hivo.

Kwasababu hiyo, msimamo wangu unabaki kuwa, Meddie Kagere bado anastahili kuwa chaguo la kwanza mbele ya Chris Mugalu.

Bao la kwanza alilofunga leo ni matunda ya utulivu na uelewa wa lango aliokuwa nao. Mshambuliaji mwingine angeweza kupiga shuti kubwa au angepiga upande wa pili wa goli ambao kila mtu alidhani ndio sehemu sahihi ya kupiga akiwemo golkipa wa Mtibwa. Si kila mtu anafunga lile bao.

Bao la pili alilofunga ni matunda mengine mazuri ya utulivu na uelewa wa kusoma misimamo ya ukuta wa Mtibwa, utulivu wa kusubiri pasi katika eneo sahihi kisha ufanikiwe kuutoroka mtego wa offside kama alivofanya Meddie, si kila mshambuliaji anaweza.

Tamati, Katika nafasi tatu ambazo zingeweza kuwa mabao alizozipata Kagere, amefunga mabao mawili. Nini kingine anatakiwa kukifanya kama striker?

Mwisho kabisa ninamuheshimu sana Mugalu, ninamuheshimu sana Didier Gomes na kukubali kuwa anaelewa mpira kuliko mimi lakini fikra zangu zipo hivi.

Nafungua mjadala nikikubali kukosolewa kuwa, Meddie Kagere anastahili kuwa mshambuliaji chaguo la kwanza mbele ya Chris Mugalu.
.
[emoji871]@deo_mwanasoka
 
Sasa unamfundisha kocha kazi ya kufanya
 
Simba hatuna tabia ya kulalamika bila sababu.Tunae mwalimu na tunamwamini.

Mambo ya utopolo kudhani timu ni ya kila mtu ndio maana wanaingilia majukumu ya mwalimu.Sasa naona wanahamia Simba
 
Ukisikia Watu Wanazungumzia Kuhusu Kikosi Kipana Maana Yake Ndo hiyo...! Yaani Kocha Anakuwa na Options tofauti tofauti kulingana na mahitaji Ya mechi husika...! Ushauri mie na Weye Kazi yetu Kushangilia tu.....Baaaaaaasi
 
Goli la kwanza la MK14,kama ilo Mugalu alikosa mechi mbili tofauti.
Medii kama angepata nafasi ya kucheza muda mrefu kama Mugalu caf Champion leageu nahakika sahivi ana magoli zaidi ya manne huyu myama.

Magalu anafaa na nimzuri tu ila kwa weredi wa kutikisa nyavu anasubiri kwa AK 47,,,hivi a.k.a yake uwa ni AK 47 au MK14!?
 
MK 14, kifupi cha Medie Kagere jezi namba 14.
 
Angalia na aina ya mpinzani. Kwa mechi za bongo ambazo ni wazi simba INA uhakika Wa kutawala mchezo na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga, Kagere ni anafaa na kocha analijua hilo.
Kwa mechi kama dhidi ya Ahyl Kagere alifanya nini? Ni sifuri! Ile mechi haikuwa na umuhimu mkubwa kwa simba na kocha alimpanga makusudi Kagere ili kuuonyesha umma kuwa mechi za aina hiyo kagere hawezi. Kagere mwenyewe amejithibitisha kuwa hawezi aina hizo za mechi!
 
Kagere Hafai match yenye presure kaeni mkujua msilete mambo yenu. hamjui mpira mnajifanya kumchambua kocha. angalia timu ya taifa france walichukua kombe la dunia pasipo mshambuliaji wao girudi kufunga hata goli moja lakini angalia alichokuwa anakitoa anakabwa na mabeki wawili hicho ndicho anachofanya Mugalu
 
Mugalu ni kimeo, hatuwezi sema kazi ya Mugalu ni kukaba, anapata nafasi za wazi anashindwa kufunga, kama kocha anaona MK 14 hakai vizuri kwenye mfumo wake, mwisho wa msimu watafute striker mwingine na Mugalu aruhusiwe kuondoka.
 
Timu ambazo Simba SC inaweza kucheza nazo fainali ya Klabu Bingwa Dunia mwaka huu
1.Man City
2.Chelsea
3.Real Madrid
4.PSG"
 
Najua fika ni"MK14"
nilichofanya ni ushabiki biriani,ushabiki minyamanyama,ushabiki mishkaki ya samaki na sio ushabiki wa lawama na kulialia
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Kwamba jamaa ana uwezo wa hiyo mashine AK-47
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…