Albinoomweusi
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 3,433
- 8,585
Ninakubali kuwa mabadiliko ya mpira wa kisasa yanahitaji mchezaji anayeweza kufanya kwa ufasaha kazi zaidi ya moja. Ninakubali na ninaheshimu sana hilo.
Kwasababu hiyo, mpira hautaki tena mikono ya golkipa tu bali unataka golkipa awe sehemu ya kiunganishi cha mchezo, awe mpiga pasi kama viungo tu.
Kwasababu hiyo, mpira hautaki tena mabeki wanaokaba tu bali beki anatakiwa ashambulie, apige pasi za mwisho na afunge kama tu viungo na washambuliaji.
Kwasababu hiyo, mpira haumtaki tena mshambuliaji anayefunga tu bali Unamtaka mshambuliaji anayefunga, anayekaba na kuwadhibiti mabeki.
Kwasababu hii Chris Mugalu amekuwa chaguo la kwanza mbele ya Meddie Kagere ndani ya Simba chini ya Didier Gomes. Ninakubali na kuheshimu sana hili, japo nina fikra tofauti kidogo.
Fikra gani tofauti unazo ?? Kazi ya mshambuliaji ni kufunga, na anahukumiwa kwa idadi ya mabao aliyofunga. Kama anaweza kukaba au kuchezesha timu, ni faida tu za nyongeza lakini Si busara sana kumuhukumu kwa vigezo hivo.
Kwasababu hiyo, msimamo wangu unabaki kuwa, Meddie Kagere bado anastahili kuwa chaguo la kwanza mbele ya Chris Mugalu.
Bao la kwanza alilofunga leo ni matunda ya utulivu na uelewa wa lango aliokuwa nao. Mshambuliaji mwingine angeweza kupiga shuti kubwa au angepiga upande wa pili wa goli ambao kila mtu alidhani ndio sehemu sahihi ya kupiga akiwemo golkipa wa Mtibwa. Si kila mtu anafunga lile bao.
Bao la pili alilofunga ni matunda mengine mazuri ya utulivu na uelewa wa kusoma misimamo ya ukuta wa Mtibwa, utulivu wa kusubiri pasi katika eneo sahihi kisha ufanikiwe kuutoroka mtego wa offside kama alivofanya Meddie, si kila mshambuliaji anaweza.
Tamati, Katika nafasi tatu ambazo zingeweza kuwa mabao alizozipata Kagere, amefunga mabao mawili. Nini kingine anatakiwa kukifanya kama striker?
Mwisho kabisa ninamuheshimu sana Mugalu, ninamuheshimu sana Didier Gomes na kukubali kuwa anaelewa mpira kuliko mimi lakini fikra zangu zipo hivi.
Nafungua mjadala nikikubali kukosolewa kuwa, Meddie Kagere anastahili kuwa mshambuliaji chaguo la kwanza mbele ya Chris Mugalu.
.
[emoji871]@deo_mwanasoka