Raimundo
JF-Expert Member
- May 23, 2009
- 13,416
- 12,618
Hmmmm! ipi ambayo mwenyewe ungependa kuitumia maishani mwako moja au zote? Kuliwahi kuwa na uzi humu wa jamaa ambaye alikuwa na dada yake baba mmoja mama mmoja na maishani mwake siku zote alijua dada yake ni mwanamke. Na alikuwa na mashoga zake ni warembo sana na mdogo mtu wa kiume hadi wengine kuwamezea mate. siku moja wawili wakaja kumtembelea dada yake nyumbani kwao na yeye akiwepo. Kisha hao wakatokomea chumbani. Mdogo mtu hakuona cha ajabu maana kwa mashoga walioshibana kuingizana chumbani si kitu cha ajabu hata kidogo. Baadaye kukaanguka varangati la kukata na shoka kule chumbani, mdogo tu akavumilia lakini uvumilivu ukamshinda maana kelele zilizidi kuongezeka na akaona asije kuumia mtu au hata kufa hivyo akaamua kuingia kule chumbani kwa nguvu na ndipo kumkuta dada yake akiwa uchi wa nyama huku dushe limesimama. Inawezekana details haziko 100% accurate lakini huo uzi umo humu na kama kumbukumbu zangu ni nzuri ulipata wachangiaji wengi sana.
Anaitwa LIKUD, mkuu umeandika kama vile umeisoma juzi.