Nina Kiasi cha Milioni 1.6 je nikianza kujenga room self naishia wapi?

Kama kiwanja unacho lakini pia kama utatumia mafundi wa bei nafuu basi hata kwenye Renta utafika na utakua umeshajipa munkali wa kumalizia coz kila utakapoliona banda lako litakupa hasira zaidi ya kutafuta ili umalizie
 
Hata ukitaka vyumba ya vi3. Njoo Kibiti tukuuzie tofauli za kuchoma boy
 
Mkuu sikukatishi tamaa lakini humalizi,labda usiweke tiles na choo cha kukaa uweke cha kuchuchumaa
 
mie sio fundi mjenzi lakini ungesema unaishi mkoa gan ingesaidia ! vinarua wanamaliza sana pesa aisee !nadhan ukijibanaaa ukazitupia zote huko utamaliza kunyanyua ukuta !yaan km upo serious anza sasa uskishachenji tu 10000 imekula kwako !kila la heri !

nb kumbuka kuweka dirisha kubwa aisee !usiweke vidirisha viduchuu
 
tofali 400.. bei laki 4.. fundi hadi rinta 300,000, cement mifuko 10 bei 120,000, mchanga lori dogo bei 120,000, maji lita 1000 bei 15,000.. kokoto debe lori dogo bei 150,000 , unaweza fika mbali mkuu.

jaribu kuanza ujenzi
 
tofali 400.. bei laki 4.. fundi hadi rinta 300,000, cement mifuko 10 bei 120,000, mchanga lori dogo bei 120,000, maji lita 1000 bei 15,000.. kokoto debe lori dogo bei 150,000 , unaweza fika mbali mkuu.

jaribu kuanza ujenzi


kwenye mchanga inategemeana na mkoa na kokoto
 
Inatosha kutegemea na mkoa uliopo na vitendea kazi ulivyo nazo.... but hautopiga finishing ya uhakika.


Room kubwa self tofar za kuchoma inakula 1500 @ 50 km utafyetua na kuchoma mwenyewe= 60, 000.

Msingi utagharimu = 200000. Kwa kuwa kuna cement nyingi.. mawe na uchimbaji... kutegemea na ujenz wako.

Fundi hadi jengo kuisha kabisa hadi kupaua bati haiwez zid laki 5.

Kench na bati-laki 5.

Inayobaki ni finish ya kizembe.
 
Nunua tofali za 1000 kama 600 cement mchanga kokoto weka hapo chini. Achana huko kabisa unatafuta hela ya fundi ukija unaanza msingi
 
Chumba kimoja hakizidi tofari 400, cement mifuko kumi, kuhusu material zingine inategemea uko mkoa gani, hiyo pesa nyingi sana hats kama hautamaliza ila itaishia pazuri sana
 
Wala usijiulize kama una kiwanja kalianzishe kuna level ukifika utakuta nyumba imeisha tu bila tatizo. Anza chumba ila kiwe self contained
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…