Nina Kiasi cha Milioni 1.6 je nikianza kujenga room self naishia wapi?

Nina Kiasi cha Milioni 1.6 je nikianza kujenga room self naishia wapi?

Inatosha kutegemea na mkoa uliopo na vitendea kazi ulivyo nazo.... but hautopiga finishing ya uhakika.


Room kubwa self tofar za kuchoma inakula 1500 @ 50 km utafyetua na kuchoma mwenyewe= 60, 000.

Msingi utagharimu = 200000. Kwa kuwa kuna cement nyingi.. mawe na uchimbaji... kutegemea na ujenz wako.

Fundi hadi jengo kuisha kabisa hadi kupaua bati haiwez zid laki 5.

Kench na bati-laki 5.

Inayobaki ni finish ya kizembe.
Acha uongo wewe,yani chumba 1 kichukue bati za laki? Tumia simba dumu bandle tsh 300000 tu na yanatosha.kuhusu tofari fyatua mwenyewe mifuko ya saruji 10 sawa na tofali 400 na zinatosha kabisa na sawa na sh 350000 tu
 
Nilichojifunza hapa ni kuwa,wachangiaji wengi hawana uelewa na mambo ya ujenzi aidha hawajawahi kujenga na hata kusimamia tu ujenzi wakapata uzoefu
 
Kama kiwanja unacho lakini pia kama utatumia mafundi wa bei nafuu basi hata kwenye Renta utafika na utakua umeshajipa munkali wa kumalizia coz kila utakapoliona banda lako litakupa hasira zaidi ya kutafuta ili umalizie
Mmhhh... Hapo unazungumzia tofali ngapi? Cement kiasi gani na nondo ngapi? Hapo sijaweka gharama za ufundi, maji, mchanga na kokoto.
 
Mmhhh... Hapo unazungumzia tofali ngapi? Cement kiasi gani na nondo ngapi? Hapo sijaweka gharama za ufundi, maji, mchanga na kokoto.
Babu raha ya ujenzi kuanza,mwache aanze
 
Acha uongo wewe,yani chumba 1 kichukue bati za laki? Tumia simba dumu bandle tsh 300000 tu na yanatosha.kuhusu tofari fyatua mwenyewe mifuko ya saruji 10 sawa na tofali 400 na zinatosha kabisa na sawa na sh 350000 tu
Nimeandika kench na bati laki 5.

We unasema acha uongo bati za laki hazitosh... bati ni laki 3.

Bangi mbaya saana usipokua makini.
Sawa fundi

Sent from "La -Vista"
 
Wala usijiulize kama una kiwanja kalianzishe kuna level ukifika utakuta nyumba imeisha tu bila tatizo. Anza chumba ila kiwe self contained
Hhahah! Hiyo 'self contained' unamaasha aweke partition ya kuegesha mtondoo, au!? Maana self inataka septic tank na kwa hyo 1.6 kufanya hayo yote sjui ka itatosha mkuu
 
Ok... kumbe lengo lilikuwa kumtia moyo sio?

Nimekusoma...
Ndio Babu, tumtie moyo kijana kujenga si lazima uwe na mil 10 hata laki 5 ukiwa na kiwanja waweza anza kusanya hata mahitaji
 
Mkuu hiyo pesa utaishia kuchukiana na mafundi buree!!, nakushsuri iyo pesa kwa vle una kiwanja jenga mabanda ya mifugo ununue mifugo ufuge hapo ata miska mi3 kisha kusanya pesa yako ya faida ujenge
 
Inategea unaishi mkoa gani mkuu ila kama ni huku kwetu kijijin rom3 unapata tena bila waswas yan
 
Inategemea na sehemu...kuna ardhi na ardhi, fanya utafiti wa eneo ulipo ujue aina ya ardhi ya hapo...kuna ardhi nyingine hiyo yote inaweza kumezwa kwenye msingi tu.
 
Back
Top Bottom