Nina kiasi cha shilingi milioni 3. Nataka nifungue sehemu ya chips, kuku, mishkaki, Je mtaji unatosha?

Nina kiasi cha shilingi milioni 3. Nataka nifungue sehemu ya chips, kuku, mishkaki, Je mtaji unatosha?

Sasa kama pango ni laki tatu alafu mtu anataka kodi ya mwaka na inabidi ufanye refurbishment ya mamilioni ya pesa itatosha vipi ?

Lakini kama unaweka mwanvuli na viti vya plastic, kabati la aluminium na jiko la mkaa kwanini isitoshe na kubaki ?

Haya mambo mengine huenda hata pesa sio kigezo unaweza ukawa na laki nne tu unaanza kwa kukodi vitu na kununua viazi mali kauli sokoni na ukapata faida kuliko aliyeweka mamilioni na mzigo unalala daily...
 
Mkuu mimi nilifungua kwa tsh 900k pekee kodi vifaa vilinigharim 700k nikaanza na mafuta lit 20 na gunia moja la viazi na nkaweza kumaliza gunia moja ndan ya siku tatu.
Changamoto ya hii biashara ni kupata vijana hasa wamenya viaz kwa maana kwa mtaj wang sikuw na mashine ya kumenya. Kingine ni ushindani asee ukizengua tu kwenye kukausha chips utawapoteza wateja
 
Lakini hii biashara ili utoboe unahitaji uwe na mtaji mm baada ya kufanya mda kidg mtu akanipa connection mbele ya night club asee na kuna mwamba akanipa connecfion ya kuku kutoka malinyi nkamtafta mama malinyi akawa ananipakia kwenye gari ya master j kipind hicho napokelea town asee kwenye kuku ndio nilipiga hela nkawa nachoma chips kuku kuanzia saa tatu usiku mpka saa tisa alfajir naamsha zangu sema nilifanya ndan ya miez 3 tu nkaswitch kweny mchong mwingine
 
Back
Top Bottom