Nina kiuvimbe shingoni kinachoniletea maumivu makali hadi sikioni

Nina kiuvimbe shingoni kinachoniletea maumivu makali hadi sikioni

tembocard

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
247
Reaction score
121
Habari zenu na poleni kwa majukumu

Naombeni ushauri wenu, nina kiuvimbe shingoni upande wa kulia kimenitokea toka mwezi wa 3 mpaka leo hakijaisha. Pia naskia maumivu kwenye koo kama vile na vidonda kuna wakati nasikia maumivu hadi masikioni.

Kuna mda kuna vitu vinatoka huku kwenye koo vipande vidogo vya rangi ya njano ukiviminya vinaminyika ila vinatoa harufu mbaya sana. Pia kwenye hizi tezi ndani ya koo kumetokewa na michirizi mekundu na zimevimba.

Nilienda hospital wakanipa Pen V sikupona. Nimerudi tena wakanipa Cipro sikupona nikarudi wakanipa tena Ampiclox sijapona bado uvimbe upo na maumivu bado nayasikia.

Naombeni msaada wenu jamani nitumie nini ili nipone?

Mungu awabariki
 
Pole sana mkuu naomba uwe na subra waje waliyosomea mambo hayo utapata muongozo pole sana aisee.
 
Koo vipi huwa haliwashi mpaka kuja masikion hivi.
 
Sio umevimba mtoki kweli?
Nahisi ndo mtoki maana uko nje ya shingo upande wa kulia ukishika kuna kiuvimbe kama kigololi cha mda mref toka mwez wa 3 ukikibonyeza kwa nguvu ndo kinauma, hv unasababishwa na nini?
 
Lilianza kuwasha kwanza ndo baadae yaka anza maumivu
Lilikuwa na tabia ya kuwasha badae nikashtuka shingoni na kiuvimbe badae nikaanza kuskia maumivu ndan ya koo ndo mpaka Leo, hata nikishika nje ya shingo mbele kwenye koromeo napata maumivu
 
Lilikuwa na tabia ya kuwasha badae nikashtuka shingoni na kiuvimbe badae nikaanza kuskia maumivu ndan ya koo ndo mpaka Leo, hata nikishika nje ya shingo mbele kwenye koromeo napata maumivu
Nenda hospital kawaone wataalamu wa kinywa.
 
Nenda hospital kawaone wataalamu wa kinywa.
Sawa asante nitaenda? Samahani hivi hao dactar wa kinywa wako hospital gan kwa Dodoma ili niende direct maana kila nikienda hospital wanaishia kunipa midawa bila mafanikio
 
Sawa asante nitaenda? Samahani hivi hao dactar wa kinywa wako hospital gan kwa Dodoma ili niende direct maana kila nikienda hospital wanaishia kunipa midawa bila mafanikio
dodoma sijajua but. Jaribu kuulizia wenyeji.
 
Mtoki huo!
Kamuone daktari,
Augumentin (antibiotic) itakufaa, mueleze daktari akupe dozi inayo kufaa!
Una infection ndiyo iliyo sababisha huo mtoki!
Nina hakika Augumentin itakufaa ingawa ni ghali kidogo!
Bora uhai!
Wakati wa unatumia hiyo doze epuka vitu vya maziwa Maana vinauwa nguvu ya dawa kiasi!
Pole sana na Mola akutangulie!
 
Kama upo Dar Es salaam Ni vyema ukaenda ocean road ukafanya vipimo bya kitaalam zaid

Huenda ikawa Ni dalili Za Awali Za Saratani japo nakuombea Kwa Mola akuepushe isiwe hivyo!

Ukiona uvimbe wahi hospital haraka
 
Mtoki huo!
Kamuone daktari,
Augumentin (antibiotic) itakufaa, mueleze daktari akupe dozi inayo kufaa!
Una infection ndiyo iliyo sababisha huo mtoki!
Nina hakika Augumentin itakufaa ingawa ni ghali kidogo!
Bora uhai!
Wakati wa unatumia hiyo doze epuka vitu vya maziwa Maana vinauwa nguvu ya dawa kiasi!
Pole sana na Mola akutangulie!
Asante mpenz Mungu akubariki sana, hyo Dawa inagharimu kama sh ngap?
 
Back
Top Bottom