Nina kiwanja Nataka kujenga Nyumba

Nina kiwanja Nataka kujenga Nyumba

Super Sub Steve

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2011
Posts
17,404
Reaction score
10,900
Nina kiwanja sehemu za Kwembe nataka kujenga sijui nianze vipi! uwezo wangu wa kuweka hela ni kuwa kila baada ya mwezi mmoja naweza kuwa na laki mbili mpaka nne tu si zaidi ya hapo.Hivi yawezekana nikawa nanunua tofali kidogo kidogo mpaka nikawa na stock ya kutosha? then nkaanza kujenga msingi halafu nikapandisha kidogo kidogo yawezekana?wenye uzoefu je hili linawezekana kweli mpaka siku moja nami nikawa na nyumba yangu?
 
Inawezekana kujenga mdau usihofu, tafuta kwanza ramani ya nyumba unayotaka kisha mchukue fundi uende nae site ili aone kiwanja chako alafu akupe gharama ya kupiga msingi kwanza yaani materials yanayohitajika na gharama za ufundi kisha jipange kwa kiasi hicho cha fedha utakindunduliza kwa muda gani kufikisha hizo gharama za ujenzi. Kama hakuna udokozi, si vibaya kununua tofari kidogo kidogo ili zikitosha za kupiga msingi unaanza na msingi kwanza ili utafute nguvu ya kutafuta kunyanyulia nyumba
 
Udokozi wa tofali hiyo site haupo,mkuu hapo nadhani nataka simple house ngoja nitafute hizo za msingi kwanza,kuna jamaa jirani kjenga nyumba kimasihara mpaka sasa anakaa kwenye nyumba yake,imenipa ujasiri.asante mkuu
 
Inawezekana usikate tamaa
 
Fanya plan ya site yako ikiwezekana na atakayekuchorea ramani, Tafuta ramani ya nyumba yako yote unayotegemea, jenga msingi wote(hakikisha msingi wako unafunga mkanda kwa nondo kwa juu au weka janvi kabisa), kwa kiasi cha fedha ulichosema ni vizuri ukadhamiria kupandisha nyumba yako nusu au baadhi ya vyumba baada ya kujenga msingi wote. Kama una eneo la kuhifadhi vifaa nunua kwanza mabati, misumari & nondo(Hiki ni kichocheo cha kutokata tamaa), Mwambie fundi akupigie idadi ya tofali za nyumba yote na/au nusu utakayotaka kuanza nayo. Anza kununua kidogo kidogo hadi upate za kutosha. Tafuta fundi mwaminifu & mwenye ubora hata kama malipo yatakuwa makubwa, kwani fundi mwizi au/& asiye bora anaweza kukupa hasara ya kudumu kwa kujenga nyumba isiyo imara. Anza ujenzi, if possible hakikisha unafunga lenter. Then endelea sehemu nyingine pole pole. Ila kumbuka kama utakuwa umeshanunua nondo na bati kufunga lenter ni rahisi na ukishafunga lenter kumalizia course 2 ni rahisi na kwa kuwa utakuwa na bati utakuwa na hamasa ya ku-fight upaue. Ingawa finishing nayo inachukua ghrama kubwa lakini unaweza kufanya kwa sehemu kisha ukaendelea kumalizia ukiwa ndani(Ni bora kuliko maisha ya kupanga).
 
HIZO NI PESA NYINGI SANA, UNAWEZA. Hata laki kwa mwezi unaweza, ila muda ndo unakuwa mrefu, acha woga
 
usinunue tofali, nunua mchanga wa trip hata tano(laki laki) nunua mifuko ya cement 50-100, tofali fyatua mwenyewe.
 
usiulize gharama kwa fundi we anza tu , akikwambia 45m utakata tamaa, we anza tu, ila tafuta vibarua kuwafyatulie tofali
 
Nimesoma post yako ikaniumiza moyo,Mungu akusaidie na akutie nguvu na wala usiakate tamaa..
 
hakika unaweza, unachohitaji zaidi ni moyo wa uthubutu. uthubutu huanza kwa kuanza! Mungu akutangulie. Pia endelea kutushirikisha katika kila hatua, maana nimeona wana jf wamekupa mawazo mazuri sana.
 
Anza kaka wala usiwe mwoga! Ila mtsngulize MUNGU kwanza
 
mkuu anza, mm nilianza nyumba na laki moja na sasa imeisha kama masihara vile, sasa hivi naanza nyingine kama mwanzo... jipe moyo mambo yanakwenda usiogope
 
usinunue tofali, nunua mchanga wa trip hata tano(laki laki) nunua mifuko ya cement 50-100, tofali fyatua mwenyewe.

Kufyatua tofali kunahitaji usimamizi wa karibu sana maana wafyetuaji wengine ni wezi wanaiba cement lakini idadi ya tofali watakupa kama mlivyokubaliana ila yanakuwa mchanga/sio imara. Hivyo kama ana muda afyatue lkn kama hana ni bora kununua matofali yaliyo bora kidogo kidogo.
 
usinunue tofali, nunua mchanga wa trip hata tano(laki laki) nunua mifuko ya cement 50-100, tofali fyatua mwenyewe.

kama ana ujuzi,muda na maji kwenye eneo lake hii ni nzuri ila kama hana hivyo nilivyotaja ni bora yakununua la sivyo atakula hasara
 
Wanaja jf mlinipa moyo nimekusanya vihela na nimeweza kununua tofali nilishindwa kufyatua tofali kulingana na mazingira na muda nilionao,nimenunua tofali na vihela vya fundi nina uhakika by June foundations nitakamilisha then nitakuwa napanda kidogo kidogo,jamiiforum ni darasa tosha
 
Daa wadau na mimi nafikiri kuanza ujenzi thread hii ni very useful for me, na mimi nitaanza kidogo kidogo.
 
Wanaja jf mlinipa moyo nimekusanya vihela na nimeweza kununua tofali nilishindwa kufyatua tofali kulingana na mazingira na muda nilionao,nimenunua tofali na vihela vya fundi nina uhakika by June foundations nitakamilisha then nitakuwa napanda kidogo kidogo,jamiiforum ni darasa tosha
Asante kwa kuleta feedback
 
Aisee nimepata moyo na nguvu saaaaana, nami nitaanza ya kwangu mdogo mdogo
 
Nami nimetiwa moyo kwa darasa hili,nitaanza polepole mwezi july
 
Back
Top Bottom