Fanya plan ya site yako ikiwezekana na atakayekuchorea ramani, Tafuta ramani ya nyumba yako yote unayotegemea, jenga msingi wote(hakikisha msingi wako unafunga mkanda kwa nondo kwa juu au weka janvi kabisa), kwa kiasi cha fedha ulichosema ni vizuri ukadhamiria kupandisha nyumba yako nusu au baadhi ya vyumba baada ya kujenga msingi wote. Kama una eneo la kuhifadhi vifaa nunua kwanza mabati, misumari & nondo(Hiki ni kichocheo cha kutokata tamaa), Mwambie fundi akupigie idadi ya tofali za nyumba yote na/au nusu utakayotaka kuanza nayo. Anza kununua kidogo kidogo hadi upate za kutosha. Tafuta fundi mwaminifu & mwenye ubora hata kama malipo yatakuwa makubwa, kwani fundi mwizi au/& asiye bora anaweza kukupa hasara ya kudumu kwa kujenga nyumba isiyo imara. Anza ujenzi, if possible hakikisha unafunga lenter. Then endelea sehemu nyingine pole pole. Ila kumbuka kama utakuwa umeshanunua nondo na bati kufunga lenter ni rahisi na ukishafunga lenter kumalizia course 2 ni rahisi na kwa kuwa utakuwa na bati utakuwa na hamasa ya ku-fight upaue. Ingawa finishing nayo inachukua ghrama kubwa lakini unaweza kufanya kwa sehemu kisha ukaendelea kumalizia ukiwa ndani(Ni bora kuliko maisha ya kupanga).