Nina makovu yaliyobaki kwenye kichwa cha uume

Status
Not open for further replies.
nunua dawa ya meno ile ya whitedent herbal siku nne hazifiki kwisha kabisa
 
Mkuu,

Kwanza pole sana.

Pili, mimi nitadili na tatizo kwenye uume. Ninachoona siyo kovu, bali ni vipele vibichi bado. Sijafahamu ilivyokuwa inaonekana hapo kabla unapodai kabla ya kukauka.

Tatu, umejitahidi sana kuelezea. Ila hujatoa muhtasari wa historia kabla ya tatizo kukupata. Lakini pia, hujaeleza alichokiona daktari baada ya kufika hospital.

Ukienda tena, kabla ya daktari kukupa dawa analazimika kukueleza tatizo linalokusibu. Hii ni muhimu sana kujumuishwa kwenye historia ya maradhi na matibabu yako tarajali. Na pengine ungeeleza ingesaidia kufikia hitimisho lenye mafanikio.

Nne, wataalam wa Regency kusema Scabies bila shaka ni kutokana na vipele miguuni na katikati ya vidole venye kuwasha.

Aciclovir ni antiviral, itumikayo kupunguza kuenea kwa magonjwa kadha wa kadha. Kwa minajili ya tatizo lako basi ni kwa ajili ya Genital Herpes. Hivyo ndiyo kusema, hao wa hospital nyingine waliona una herpes.

Tano, kwa kuangalia ninaweza kusema ni Herpes. Ili kujihakikishia kama ni Herpes basi inakubidi ufanye vipimo, HSV PCR. Hii itatoa majibu sahihi zaidi juu ya ugonjwa wenyewe.

Sita, Herpes hazina tiba. Hivyo hata kama majibu yatatoka positive basi dawa ya kuziondoa kabisa hakuna.

Kuhusu dawa ulizopewa endelea kuzitumia. Ili upate nafuu kwenye muwasho mwilini.

Nakutakia uponyaji mwema.
 
Mkuu, unaroho ngumu sana aiseeee.....🤣
 
Shukrani Dr Restart
Nilikutana na daktari wa ngozi akanielezea vizuri kuhusu tatizo langu, Ni Scabies inatabia ya kutoa viupele sehemu mbalimbali za mwili hadi kwenye genitals kwasababu wanapendelea sehemu laini.

Kuhusu Herpes
Hapana, sipo sexual active kwa miaka zaidi ya miwili sasa na nilifanya vipimo vyote vya magonjwa ya zinaa hadi herpes na majibu yalikuja negative.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…