Basil Lema
Member
- Jan 20, 2013
- 86
- 277
Mkuu Omujubi.mkuu Koffie,
Hawa jamaa wanaoneka walishaplani kupata urais kwa njia yoyote na wameupata. Kisichojulikana bado ni je, wataufanyia nini??
Kwa hiyo asiye hoji na asihoji lakini sio dalili njema kwa wanaoipenda Afrika na amani kwa ujumla.
Umenena kweli! Hawa watu waliutaka urais kwa namna yoyote na sasa wameupata. Je wataufanyia nini?
Watawala wa zamani waliopora mali za nchi zao sasa wanajiimarisha kwa kujirudisha madarakani kihalali.
Mipango yote ya kuwashitaki viongozi waliopora mali za umma inaelekea kufeli baada ya mtandao wa viongozi wa Afrika waliofaidika na uporaji huo kujirudisha madarakani kihalali (kwa sanduku la kura) Zoezi hili limeanza na Uhuru Kenyata huko Kenya. Litakwenda Uganda, halafu Tanzania, DRC, nk.
Afrika ole wako!!!,