Nina maswali kuhusu gari za umeme

Bavaria

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2011
Posts
53,092
Reaction score
53,496
Hello.

Nina swali moja kubwa kuhusu gari za umeme hasa charging system.

Hivi ukinunua gari ya umeme ambayo inakuja na ile charging set yake.

Uki install nyumbani kwako na ukawa unacharge gari yako.

Je charging speed itakuwa sawa na ile recommended kwenye manuals za gari au itakuwa tofauti?

Au umeme wa tanzania ni mdogo, utasumbua kujaza kwa wakati?

Wataalamu mnisaidie.
 
Gari laki Litafanya kazi propery na charging time itakuwa sawa kama factors za manufacturer zitakuwa considered.

Charger ya nyumbani mara nyingi ni ya single phase. so unaweza install nyumbani kwenye garage/ parking space yako.

Cha kuzingatia ni kitu kimoja tuu.
Haya magari huwa yanakuwa dedicated kwenye market fulani ili kusiwe na usumbufu.

Tanzania single phase ni 220V - 240V na Three phase/ Phase line ni 380V - 415V


Wakati nchi nyingine mambo huwa tofauti. kuna baadhi ya nchi single phase ni 110 na wengine ni 170 yani ni mvurugano tupu.

Kama utakumbuka enzi zile wakati tunanunua radio za mtumba toka japan. kv Sony, Sanyo, Nec na maredio mengine kama Kenwood akai, nikai nyingi zilikuwa ni 110v wakati sisi tuna 220v so ililazimu kuwa na Power adopter/ Transformer au Converter ya 220v kwenda 110v Bila hivyo ukiiweka moja kwa moja kwenye socket lazima iungue power Supply yake.

So kama unaagiza hakikisha unaangalia issue ya umeme. Nikutoe hofu tuu kuwa umeme unatosha. Najua unamiss concept fulani za umeme ndio maana unaona charging time itakuwa kubwa, Laaaa hasha haiwezekani kama umeme ni mdogo hutafanikiwa kabisa kucharge au utaunguza charger yako kutokana na low voltage ambayo ni result ya high current lakini pia vifaa vya kisasa vina protection mechanism so hakita fanya kazi kama parameters za umeme hazipo sawa


Kiambatanisho hicho kinainonesha Voltage/ Mains za kila nchi. So hakikisha kabla hujanunua charger lazima iendane na umeme wetu. Kama haiendani utalazimika na kuingia gharama kuwa na power adopters/ converters ili kutafuta compatibility
 
Asante sana.

Umenielezea vizuri sana.

Swali lingine;

Assume unataka kujaza gari lenye battery ya 100 kwh. Itachukua units ngapi za umeme?
 
Asante sana.

Umenielezea vizuri sana.

Swali lingine;

Assume unataka kujaza gari lenye battery ya 100 kwh. Itachukua units ngapi za umeme?

Battery inapimwa kwa unit mbili.
Current na Time. Yaani ampere hour (N)

Kwa hiyo Unit kWh. ni unit ya electric energy.
Kuna namna ulitakiwa uulize swali na pia uzitaje some parameters ndio upate jibu
 
Tunashukuru mkuu kwa somo zuri
Kwakweli nimefaidika nalo sana...
 
Basi hii ni nzuri kwa town trips day to day uses.


Mimi sio mtaalam but napitia pitia article za magari ya umeme
Kama nissan iko hivyo basi Tesla itakuwa Better ..since Tesla wao Betri Yao ni lithium
Kama ya simu..
Naamini Tesla itakuwa Ku charge nafuu zaidi na inakwenda kilomita nyingi zaidi .
Niliona last year Tesla wanataka kutoa malori yanayokwenda kilomita 300 bila kuchaji tena..

So kadri technology inavyozidi Ku improve baasi itakuwa cheaper na more reliable
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…