Nina mihogo tangu mwaka jana nimekosa soko, nawaza nisage kuwa unga ndio niuze

Barackachess

Senior Member
Joined
Sep 1, 2018
Posts
156
Reaction score
122
Habari, Nililima mihogo mwaka jana ila mpaka sasa ninekosa soko , Mbegu ya mihogo niliyopanda inaitwa MKIU, Jana nikawaza nikasema labda naweza kutengeneza unga wa muhogo nikauchanganya na mahindi nikaongezea ubora nikauza. Je hii imekaaje?
 
Unaweza uza kama unga au pia ukauza kama makopa.....kazi ni kwako
 
inaonekana soko unalozungumzia wewe ni ile kufuatwa na wanunuzi huko shambani.... hapo fresh changanya dona+muhogo ukauzie wasukuma
 
Unadhani sijawahi kulima? Hata mimi hapa nakula loss ya Vitunguu.
Nilitegemea kwa mtu kama wewe ndo ungetoa ushauri wa kujenga kwa sababu tayari umepata loss na natumaini kua ulijifanyia assessment kujua ulikosea wapi na namna ya kukabiri changa moto.
Otherwise kama bado hujakubaliana na hiyo hali ya loss ni bora unyamaze kuliko kutoa ushauri wa hasira na kudidimiza mtu.Ubarikiwe ndugu
 
Una maana gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…