Nina mihogo tangu mwaka jana nimekosa soko, nawaza nisage kuwa unga ndio niuze

Mihogo Ulaya inauzwa bei mbaya sana kwenye supermarkets na ethnic shops. Mara nyingi inatoka India, Jamaica na Latin America.

Wahindi humenya na kuifreeze, kilo moja inafika Tsh20,000. Kama tutaweza kujisogeza hata mkulima akipata Tsh 4,000 soko likiwa la uhakika itamsaidia
 
Mkuu ulijaribu kutafuta masoko masokoni??Mimi next week nadhani ntaanza kutafuta masoko ya mihogo
 
Habari, Nililima mihogo mwaka jana ila mpaka sasa ninekosa soko , Mbegu ya mihogo niliyopanda inaitwa MKIU, Jana nikawaza nikasema labda naweza kutengeneza unga wa muhogo nikauchanganya na mahindi nikaongezea ubora nikauza. Je hii imekaaje?
Dsm uhitaji ni mkubwa sana, kama utaweza safirisha ndg au ongea na wafanyabiashara wa sokoni waufate mzigo shambani (hapa watakulalia sana bei,ukisafirisha mwenyewe ni better zaidi)
 
Unakulaje loss ya vitunguu sasa nunua Nyanya katakata kachumbali mtafute huyu jamaa mwenye mihogo mchukue mkaange mle .
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Upo sahihi nakubaliana na ww
 
Mkuu ulijaribu kutafuta masoko masokoni??Mimi next week nadhani ntaanza kutafuta masoko ya mihogo
Nimejaribu lakini mbegu hii MKIU , watu wanaikwepa sana, Mihogo hii ganda lake ni jekundu. Wengi wanavutiwa na yenye ganda jeupe
 
unakosa vipi soko la mihogo wakati mihogo inaliwa kila siku ?

kipande cha 200 kidogo halafu unasema hakuna soko dahh
Unategemea na mbegu, Hii mbegu niliyonayo imekuwa kikwazo
 
sasa kiongozi mbona kazi ndogo sana fanya hivi chukua mihigo yako then pakia kwenye kirikuu then tafuta soko lolote tu paki then michache mwaga chini watu lazima wanunue tena mida ya jioni
Wiki ijayo nishaanda bajeti ya kufanya hivyo
 
Kama ni ile michungu beba kawauzie wachina watengenezee gas asilia.
 
sasa kiongozi mbona kazi ndogo sana fanya hivi chukua mihigo yako then pakia kwenye kirikuu then tafuta soko lolote tu paki then michache mwaga chini watu lazima wanunue tena mida ya jioni
Hiki ndo nataka nikifanye aisee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…