Nina milioni 20 nataka kujenga nyumba ya vyumba 3 Dar es Salaam. Naweza fikia hatua gani?

Ngoja waje
Habari wadau! Naomba kuuliza ukiwa na TZS 20 Milioni na unataka kujenga nyumba ya Vyumba 3 na Master unaweza kuanza na kufika hatua Gani?

Ntashukuru kama mtanipa estimate za kila hatua

Asantee
 
Hili nalo neno
 
Unazungumzia vyumba 4 vya kulala! Tayari huo mradi ni mkubwa. Ingekuwa vyumba 3 ya kawaida isiyo na mbwembwe, pesa ingetosha 95%. Kwa kupanga, yaani mbao za kenchi unapaka oil. Tiles za Tz. Bati iliyo nafuu no colour. Ramani punguza corridor kuokoa blocks. Milango ya ndani "flush doors" na mengine mengi. Ila usibane cement katika ujenzi wako. Simamia fundi material yote itumike sawa na hakikisha nyumba inanyooka. Wewe uwe pima maji. Nunua Square, kila kona pima.
 
Ni typing Error! Master Bedroom na Vyumba viwili Plain
 
Asantee kwa mawazo yako Kaka
 
Habari wadau! Naomba kuuliza ukiwa na TZS 20 Milioni na unataka kujenga nyumba ya Vyumba 3 na Master unaweza kuanza na kufika hatua Gani?

Ntashukuru kama mtanipa estimate za kila hatua

Asantee
Utamaliza hadi kupaua, finishing ndo itakubidi ujikusanyekusanye tena kulingana na kiwango unachotaka. Utaweza kuhamia kabisa japo ni kukiri udhaifu
 
Vitisho vimeanza. Nyumba zetu za kawaida anaweza kuhamia kabisa akaremba akiwa ndani
Amna bana jamaa kaongea ukweli lakini, usije kumpa mtu moyo akapewa liramani la kufa mtu uko kwasababu tu ni ya room 3 akaishia kwenye lenta
 
Kama utasimamia mwenyewe unamaliza ila kama kuna mpambe imekula kwako.
 
Ficha ujinga wako mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…