Ujenzi unategemea unaufanyia wapi, mara nyingi ujenzi nje ya mji unakuwa kidogo nafuu. Kwa sie tuliojenga Dar katikati ya mji tunaelewa. Kuna tofauti ya kujenga nyumba na mchoro maana wengi wanapachika marofali tu, ndio hao wanaosema nyumba unajenga kwa million 20 mpaka finishing, ushawahi kuona wapi?
Nina nyumba nilijenga ya kibabe huo msingi tu ulikula million 20, hapo sijasimamisha. Hapo chini tu nilitumia tofali elfu 4, nyumba ya appartment ya wapangaji wanne chumba sebule vyoo viwili, jiko na dining ya kizushi, na kibaraza. .
Nyumba yangu ya vyumba viwili, kimoja self, kuna public toilet, kuna sebule na dining ya kizushi, kuna jiko ndani na baraza za ft 4 mbele na nyuma ilinigharimu 70 millions. .
-Msingi tu nilijenga course kumi matofali ya kulala ili niongeze uimara
-Grills nilinunua nondo nikachongesha mwenyewe zile ngumu kutoka kamata
-Milango yangu ya mkongo nilitengeneza kipindi hicho tabora, milango 15 iligharimu 7 million
- Tiles nimeweka granite nyumba zimegharim 5.5 million na ufundi
- Baada ya lender juu baraza mbele na nyuma nimejenga course tisa mpaka kwenye bati kuzuia watu wasitoboe barazani wakarukia ndani
-Nyumba nzima iko na gypsum sebuleni nimeweka urembo wa kawaida na taa juu kwenye gypsum inapendeza sikutaka niweke mambo mengi sana
-Nyumba yote nimefunga Aluminium
-Jikoni nimeweka makabati ya juu mbao mpodo sikutaka kuweka makabati mninga wala mkongo kwa sababu yatakuwa mazito sana imenigharim laki 5
- Bati nimeweka msauzi ufundi nakumbuka pamoja na blandering uligharimu 2,500,000 TZS
- Mbao zilinigharimu 4 million, nilinunua na za kupigia lenter
-Plasta ilinigharimu 1.2 million
-Kuchimba karo la choo ilinighaarimu 250000/- ufundi uligharimu 240,000/ TZS
- Kujenga nyumba mpaka lenta ufundi ulinigharimu 4 million.
-Geti mbele na nyuma na grills iligharimu 3,500,000/-
Hata hivyo mie ni msomi vitu niliandika mwanzo mwisho gharama zote ninazo. Ujenzi ni gharama asikwambie mtu, mpaka lenta nilitumia 23 million kitu ambacho sikuwahi kutegemea kabisa. Finishing inakula hela hatari kuna vitu vingi kama vifaa vya bomba kifaa kigodo tu unaambiwa laki na nusu, gharama ni kubwa. .
Kuna gharama nyingi za ziada, kama ubebaji, usafiri, ulinzi, NK. Ila siwezi kataa wapo wanaofanya ujenzi mpaka finishing kwa million 20, ila nyumba kuagiza mchanga pwani kuleta huku lori tu laki tatu. Hapo sijapiga gharama za tofali na mambo mengine