nina milioni 200

Njoo uje ufungue kabenki kadogo zitazaana sana mtaji wa kabenki ka wananchi ni Tsh. 50 milioni sasa hizo 200 ni nyingi sana nitafute tushauriane pia mawazo ya biashara ni mengi. Nipigie tuongee 0755394701
 
wajameni mie nataka kurudi bongo kufanya business, nina mtaji wa kama milion200 hivi, je ni biashara gani ambayo itanifaa? nilikuwa nawaza kufungua warehouse ya kuhuza vitu vya ujenzi lakini sijui pa kuanzia any ideas pls. niko abroad! thanx

Mimi ningekushauri ufungue kiwanda cha kusindika mafuta Kigoma ...utakuwa umeletea faida kubwa sana nchi kwa vile unatoa ajira na kwa vile mafuta ya mawese yana soko kubwa nje hivyo basi utaingizia wewe na nchi fedha za kigeni
 

Mkuu nimependa wazo lako je kuna uwezekano wa kuweka ka rough breakdown?
 
Mkuu kibogo bongo hiyo ni pesa nyingi sana kama ukitulia, ndio maana naona wengi hawatoi majibu ya kueleweka, most of time humu tumezoea kushauriana na vimitaji vya milioni 3 hadi 20 hivi, sasa hii ni changamoto mpya.
Kwa mtaji huo nakushauri ukija bongo kawaone business consultant ya kueleweka watakushauri vizuri zaidi jinsi ya kuinvest pesa yako.
Hongera mkuu, mimi nina milioni 7 nimeshindwa hata nianzishe nini kila mradi nikifanya tafiti nakuta haitoshi, matokeo nimeikimbiza bank ktk fix account navuta subira
 

Kuna mwanajamii alieleta wazo la kujenga nyumba za mbao bongo,ukiangalia bongo tuna mbao nyingi yu na nyumab zingekuwa rahisi kujenga.

Watu wakamjibu kuwa haiwezakani kwa vile ati mbao zitaliwa na mchwa


....mfano universities zetu zina uhaba wa mabweni you will be in position to resolve hi shida na pia utapewa viwanja au maeneo ya wazi ya chuo husika bure kwa vile utakua uwasaidia sana kwa upande wa accommodation.

Mkuu je ni kweli kuna uwezekano huo wa kupewa viwanja?
 
Kibongo bongo hostel za wanafunzi hazilipi kivile kama nyumba za kupangisha
 
Inategemea wewe upo comfortable kufanya kitu gani na una experience kiasi gani,

Ushauri kwa kuanzia Dont Put All Your Eggs in One Basket, unaweza ukaspread pesa yako katika investment tofauti
There is no substitute for experience biashara yoyote anza polepole na kidogo kidogo learn as you go along

Be carefull na wabongo, wabongo uliowaacha enzi unaondoka sio wabongo wa sasa..., sound nyingi, hawawezi kusema hawajui wala kitu hakiwezekani ila utekelezaji ni sifuri (trust me I know this through experience..)

Tumia advantage uliyonayo ya exposure ya huko nje ulipo, Je kuna product huko unazoweza kuleta huku au product huku ambayo unaweza kupeleka huko (sometimes contacts and who you know can do wonders)

Kabla hujaja angalia auctions za huko unaweza kupata vitu vya agriculture ambavyo ushuru wake ni mdogo sana na unaweza ukaleta huku na kuuza au kukodisha (what I mean unaweza ukaja na vifaa ambavyo ni bargain huko na huku vikakusaidia)

Kumbuka.., we are our own worse enemies...,
 
kwa millioni 200 unaweza kununua kiwanda cha Cement kidogo,unakifunga in a place near Dar.pesa yako itarudi fasta tu.ukilipenda wazo eleza nitakufafanulia hapa wazi kabisa
fafanua tafadhali
 
What is your passion.
My passion lies in hotels!
With your 200M you can have a very nice lodge of 15 rooms. Just take a price of 25k per room.
Ukipata wahudumu wazuri(wasafi) Utakua unajaza Daily.
Trust me this is a very paying business
 

Hapo kenye nyekundi nimecheka sana Kiongozi. I once had a very terible accisent. Ukiangalia ile gari huwezi amini kama nilitoka mzima. Funny enough nilienda kuihifadhi in a certain garage. wale mafundi wakaniambia hii gari mzee tunaweza kunyoosha, walivyokua wanaongea utafikiri gari yaweza rudi kua mpya.
Jamaaa walishusha gharama zao nikaona ni reasonable. Si wakaanza kazi, Baada ya ku dismantle gari wakagundua some parts were totally written of.
They came back to me " mzee hii inyoosheka lakini haitakaa vizuri saana, ukinunua Half cut itakua bora" yaan half cut maana yake ni nunue nusu kipande cha gari ingine ili waunge.
hapo hapo nikagundua wanataka kunifilisi. nilichokifanya nilimtafuta muuza used spare parts nikamuuzia kama scrapper.
Baadae nilikuja gundua yule jamaa aliproceed na ushauri wa wale jamaa kunyoosha ila gari. Kilichompata only God knows!!!
 
Unaweza kufanya biashara ya distribution au you can decide to invest in being a dealer wa telecom company. One thing i can advise you is

1. IDENTIFY YOUR PASSION
2. DO YOUR RESEARCH
3. SET FIXED GOALS
4. HAVE AN EXIT STRATEGY
 
mimi nakushauri kama unaweza pata dalali mzuri ukanunua mtaa mzima kama manzese ambao unaweza pata na barabara inayotoka. unaweza jenga hoteli ambayo itakulipa kwa haraka sana.
 
Asanteni sana wadau, comments zune zimenifungua snaa macho, nimeziprint and then nitazifania kazi. si unajua tena Dar land it is very expensive, nitaangalia maeneo ya morogoro pia. mungu awabariki sana.

Shughuli za kufanya zipo nyingi sana, lakini uwe makini. Mfano kama nilivyoona baadhi ya watu wanakushauri kutumia BUSSINESS CONSULTANTS (Experienced ones!!!!).

Pia mbona hata Agrobusiness inalipa!
Unaweza kuwa unanunua mazao toka kwa wakulima wakati wa mavuno, unaweka stock. U just spend not more than 2 months buying you keep you stock for about 6 months you sell your products. Haiumizi kichwa. Mbona wafanyabiashara wengi wakubwa tu wanafanya hizo kazi!

Mfano: Unanunua gunia la mpunga mwzezi wa tano/sita kwa sh. 35,000/40,000 unauza mwezi November-January kwa sh. 50,000 - 80,000. This means your investment yields >50% as a profit in 6-8 months!

Ni ushauri tu!

YOU CAN TAKE THE DONKEY TO THE RIVER BUT YOU CAN'T FORCE IT TO DRINK!
PEOPLE MAY HELP A PERSON TO THINK, BUT THEY CAN'T THINK FOR HIM!

Nakutakia mafanikio.
 
Nakushauri uendelee na wazo lako la Vifaa vya Ujenzi

Kigamboni ipo mbioni kuwa modern city

tafuta eneokubwa anza biashara yako.
 
Asanteni sana wadau, comments zune zimenifungua snaa macho, nimeziprint and then nitazifania kazi. si unajua tena Dar land it is very expensive, nitaangalia maeneo ya morogoro pia. mungu awabariki sana.

Mdau ninakuhakikishia kuwa shule inalipa lakini pia Dsm ardhi siyo ghali kila kona. Nipigie 0655 583 330 nikuoneshe maeneo ya pembezoni mwa Dsm - Ilala ambayo unaweza kupata Ardhi ya kuanzisha shule na ukapata wanafunzi wa kutosha ukiwa na usafiri wa uhakika.
 
Nakushauri uendelee na wazo lako la Vifaa vya Ujenzi

Ndio sababu Nikamshauri mwanzo experience yake ni muhimu? Sababu hakuna substitute ya experience...


Mfano kama ana experience na ujenzi anaweza hata akaja na vifaa vya ujenzi na kukodisha...
  • Hivi unajua vitu kama concrete mixer, au vile vifaa vile vya kujengea ghorofa (kwenye nguzo) unaweza kukodisha kwa shs ngapi kwa siku?
  • Sababu kulikuwa na mtikisiko wa uchumi ulimwenguni vifaa vingi unaweza kupata kwa bargain huko ulaya, na kwa bei ya chee ukaja kukodisha huku dar
  • Pia watu huku bado wanamwaga zege kwa kupokezana karai.., unaweza ukaja na concrete pump ambayo zege linachanganywa chini na kwa pipe linarushwa mpaka ghorofani kazi ya masaa inafanywa kwa dakika
Kwa hiyo mkuu usi-underestimate experience yako, au ujuzi wako sababu that is what will put you miles apart from the rest
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…