Ndio sababu Nikamshauri mwanzo experience yake ni muhimu? Sababu hakuna substitute ya experience...
Mfano kama ana experience na ujenzi anaweza hata akaja na vifaa vya ujenzi na kukodisha...
- Hivi unajua vitu kama concrete mixer, au vile vifaa vile vya kujengea ghorofa (kwenye nguzo) unaweza kukodisha kwa shs ngapi kwa siku?
- Sababu kulikuwa na mtikisiko wa uchumi ulimwenguni vifaa vingi unaweza kupata kwa bargain huko ulaya, na kwa bei ya chee ukaja kukodisha huku dar
- Pia watu huku bado wanamwaga zege kwa kupokezana karai.., unaweza ukaja na concrete pump ambayo zege linachanganywa chini na kwa pipe linarushwa mpaka ghorofani kazi ya masaa inafanywa kwa dakika
Kwa hiyo mkuu usi-underestimate experience yako, au ujuzi wako sababu that is what will put you miles apart from the rest