nina milioni 200

thats very interesting - naomba usibadilishe contacts - na Mungu akupe uhai - na mimi nitakutafuta one of these days - napenda kuanzisha shule ila sikujua inakuwaje - tuelezee tena "how about a boarding school" - ikiwa mbali na mji si unatakiwa uwe na dispensary ndogo pia???
 

Mkulu vifaa hivyo viwili tu yaani concrete mixer na concrete pump zilizotumika kwa bei ya chini kabisa ni TzShs 123,000,000....kama lily ana pesa za tz basi anabakiwa na chenji.....Lakini hajatuambia hizo pesa ni madafu ama green....Kwa sababu yuko nje tu fikirie ni green hivyo basi ni tosha sana
 

Hizi TZS 2million ni ada ya shule yenye madarasa 3, maktaba, maabara na toilet?? Mi nadhani hadi umshawishi mtanzania atumie 2m kumsomesha mtoto kwenye shule kama hiyo inahitaji ufanye zaidi ya hapo! Kwa haraka haraka naona kama huu mpango haujakaa sawa hebu recheck hesabu hizo vzuri.... afu mwambie kabisa shule ni long term investment cos haitaweza kumpa returns immediately incase na yeye anazitegemea 100% hizo hela alizochanga km mtaji.
 
afu mwambie kabisa shule ni long term investment cos haitaweza kumpa returns immediately incase na yeye anazitegemea 100% hizo hela alizochanga km mtaji.

Kweli Mkuu ndio maana nimesisitiza hapo mwanzo yeye mwenye mapenzi yake.., sababu biashara zote ingawa zinalipa lakini inategemea na person behind hiyo biashara na management nzuri.. (shule sio majengo peke yake, ni waalimu, marketing na promotion) mpaka watu wajue kwamba hiyo shule ni nzuri itabidi waone matokeo yapo vipi na shule ipate sifa nzuri.

Je Muhusika anataka biashara ambazo ni hands on ambazo zinataka a keen management au anataka zile ambazo hazihitaji kufuailia sana. Mfano kuna watu wanatajirika kwenye biashara za magari..., lakini wengi (sababu hawajui mtandao wa spea au hawajui ni wakati gani wauze gari wanunue jipya) wanafilisika... Kwahiyo hakuna Biashara Mbaya, Bali Management Ndio Mbaya.. Therefore inabidi tujiangalie wenyewe kama tunaweza kufanya kitu fulani.
 
hizo milioni 7 ziweke bank ktk Dola siyo Shilingi.baada ya mwaka milioni saba inashuka thamni kuwa milioni 5.nikimaanisha vitu vya milioni7 mwaka huu mwakani vinakuwa milioni 9.hiyo ndiyo inflation ya bongo vitu huwa havishuki bei ni kupanda kwa kwenda mbele.kinachoshuka bei bongo ni gharama za kupiga simu ktk mitandao ya tigo and Zain na zantel
 
Utapokea ushauri mwingi, na kila mtu atakueleza kulingana na matakwa yake, (na hilo ndilo ulililohitaji.
Suala moja la msingi ambalo hujalijibu - wewe una utaalamu gani? maana hii itatupatia picha ya aina ya biashara kulingana na utaalamu wako. Unajua unapoanza biashara yoyote ni vizuri wewe mwenyewe ukawa na abc za uataalamu husika vingievyo hapa bongo watakuchakachua.
Pili umeulizwa kama una mkoa specific ambayo ungetaka kuwekeza. Kuna biashara ambazo ni profitable kila mahali lakini mzunguko wa fedha nyingi hivyo unahitaji mahali papana zaidi; huwezi kuzungusha fedha hizo katika wilaya nyingi za vijijini.
Ushauri wangu:
Don't put all your eggs in one basket (wekeza katika miradi ya aina tofauti tofauti na maeneo tofauti tofauti.)
Kwenye kilimo wekeza say 75million kwa kufungua shamba la migomba (mimi ni mkulima), ni vyema upate eneo unaloweza kumwagilia na uchague aina maalum ya ndizi zinazouzika, Kwa mfano ukipanda migomba 10,000 ndani ya miaka 3, una uhakika kuanzia mwaka wa tatu ile migomba 3000 uliyopanda mwanzo (mwaka wa kwanza) itakuwa imefikia uwezo wa kukupa ndizi 6000 kwa mwaka x 20,000 = 120,000,000. Hata bei ikishuka hadi 10,000 (which is unlikely maana ongezeko la walaji ni kubwa sana kuliko ongezeko la wakulima) unapata 60,000,000. Mwaka wa 4 unapata ndizi 12,000 wa 5 ndizi 18,000 and so on.
Mabaki ya migomba waweza kutengeneza biogas, huhitaji wafanyakazi wako kutumia kuni!..
Then wekeza say 100m kwenye uuzaji wa mafuta. Hii inalipa pia na risk iko chini sana. Afterall kama unaaminika biashara hii haihitaji fedha nyingi maana waweza kupata mafuta kwa mkopo na mashine kwa mkopo pia. nk.
Kuna mambo mengi ya kufanya kama kweli unazo hizo hela.
karibu sana atupatie ajira.
 
fafanua tafadhali
ufafanuzi:
unaweza kujenga a small Cement production line from India kwa hizo pesa.in 2009 niliattend trade fair pale DiaMond in Dar.kuna kampuni inauza Cement production lines.
Founder wa hiyo kampuni alianza kutengeneza cement ya 250Kg per day kulikuwa na shida sana ya cement in India by then ,baada ya miaka kadhaa akawa na kiwanda cha kutengeneza machine za cement.so the strory goes now they are a major cement production line co. in India.
so anaweza kuanza na prodouction line ya 50Ton per day ,the akauza kwa wateja directly e.g. Construction companies na kwa kuwa ni kampuni ndogo overheads zitakuwa ndogo sana kulinganisha na Twiga cement, etc.
Watanzania tunafikiri viwanda huwa ni lazima viwe vikubwa sana,la hasha .
my personal experience ni kiwanda cha sababuni ambacho production line inatoa 200 cartoons per day. na quality ni nzuri kuliko ya viwanda vikubwa ,pia inafaa zaidi ktk maji chumvi ya visima.demand ni kubwa sana tatizo ni Raw materials hapo ndo unapobanwa na viwanda vikubwa.
 
wajameni mie nataka kurudi bongo kufanya business, nina mtaji wa kama milion200 hivi, je ni biashara gani ambayo itanifaa? nilikuwa nawaza kufungua warehouse ya kuhuza vitu vya ujenzi lakini sijui pa kuanzia any ideas pls. niko abroad! thanx

Kuna biashara moja ya PVC pipes itakuwa hot soon maana kuna miradi ya maji inatarajia kuanza nchi nzima na hamna reliable supplier wa hiyo kitu contractors wengi wanategemea plasco lakini anachemsha sasa kama huko uliko kuna viwanda vya plastic pipes jaribu kutembelea viwili vitatu utafute marafiki,ungewea kupata viwanda vya china ingekuwa bora zaidi au Dubai ni nafuu ukitafuta pipe za ulaya hazilipi kwa hapa kwetu.
 

mkuu...NM ... wazo ni zuri...lakini kwa mahitaji ya construction industry 50T ni ndogo sana..... hizi nisawa na mifuko 1,000 ....cubic meter moja ya zege (concrete grade 30) inatumia roughly mifuko sita ... ukigawa kwa mifuko elfu moja unapata 166 CBM ambazo ni kidogo sana kwa miradi ya ujenzi hususan civil works kama vile madaraja au migodini... hivyo kiwanda hiki kinaweza kikawa kinamuuzia cement mteja/mkandarasi mmoja tu ....
 
Nimefanya reseach Bishara ya printing (large format, pepar printing, tshirt), promotion items, sign making, car branding inalipa kwa hapa Bongo makampuni hayazidi 6 na niwawindi tu wanafanya na inawalipa sana madhali ukipata machine ya printing hata ya roland kwa $30000 pia ukipata na machine ya Tshirt kwa $ 6000, vinly cutter ya $ 12000 , then unapanda hapo china unakuja na embrodery machine $30000 na material chache nakuhakikishia itakulipa sana kwa mawasiliano niandikie emal sadetmediatz@gmail.com nitakutumia some printing machine na tukahabarishana zaidi
 
lily kuna jamaa juzi kaniambia yeye anatafuta viwanja cheap na kujenga standard houses. The total cost kwa kiwanja na nyumba mpaka isimame ni 80 mill. Then yeye ana uhakika wa kuuza 150 mpaka 200. Sikufwatilia madai yake na inaonekana ni kazi ya ku hustle hustle hivi.
Ingine iliyotulia ni uwe na compressor zakuzibua visima.Zinauzwa 10 mill na apparently zina guarantee ya kukuletea not less than 400,000 per week. Kahela kazuri kakupush vimambo kidogo kidogo hapa bongo.
 
Ingine iliyotulia ni uwe na compressor zakuzibua visima.Zinauzwa 10 mill na apparently zina guarantee ya kukuletea not less than 400,000 per week. Kahela kazuri kakupush vimambo kidogo kidogo hapa bongo.


Mkulu hio imetulia ...je unaweza kutoa spec ya hiyo compressor na ina uwezo wa kuzibua kisima cha urefu wa mita ngapi?


Mbona wapo wale jamaa Kiboko,Simba na vingine vidogo vidogo?

KURUNZI said:
niandikie emal sadetmediatz@gmail.com nitakutumia some printing machine na tukahabarishana zaidi

Mkulu si ungemwaga tu hapa ili sote tufaidike?
 
Ni wazo zuri sana kuwekeza nyumbani lakini pia ni lazima utilie maanani hali ya upatikanaji wa umeme na maji ambayo inaweza kabisa kwa namna moja au nyingine kuongeza gharama ya biashara yako na hivyo kupunguza profit. Pia unaweza kuwekeza nchi za nje hasa kwa kununua apartments za ghorofa mbili au hata zaidi na kuzipangisha. Ni biashara yenye faida kubwa sana hasa ukibahatika kupata maeneo yaliyo jirani na vyuoni.
 
Pia unaweza kuwekeza nchi za nje hasa kwa kununua apartments za ghorofa mbili au hata zaidi na kuzipangisha. Ni biashara yenye faida kubwa sana hasa ukibahatika kupata maeneo yaliyo jirani na vyuoni.

Mjomba mbona unataka umtoe nje na wakati akiwekeza hapa anatuletea ajira kwa waanetu
 
Mjomba mbona unataka umtoe nje na wakati akiwekeza hapa anatuletea ajira kwa waanetu

Hapana Mkuu kuwekeza ni popote siku hizi si lazima iwe nyumbani anaweza kabisa kuwekeza nusu nyumbani na nusu nje. Kumbuka miaka michache ya nyuma wabongo tulikuwa hatutaki kabisa kufanya kazi nje ya Tanzania lakini sasa hivi Wabongo wako karibu kila kona ya dunia, hivyo hivyo kuwekeza hakuna ubaya wowote ule kuwekeza nyumbani lakini wakati huo huo tusijiwekee vizingiti vya kuwekeza nje ambako profit margin inaweza kuwa maradufu au hata zaidi ya ile ya Bongo na hivyo kuwa na uwezo mkubwa zaidi wa kuwekeza Bongo.

 
Ni wazo zuri sana kuwekeza nyumbani . Pia unaweza kuwekeza nchi za nje hasa kwa kununua apartments za ghorofa mbili au hata zaidi na kuzipangisha. Ni biashara yenye faida kubwa sana hasa ukibahatika kupata maeneo yaliyo jirani na vyuoni.
nimelipenda hili wazo. Tena wanafunzi wengi huwa wanahangaika kupata hostel. Nafikiri itamlipa.
 
Pia unaweza kuwekeza nchi za nje hasa kwa kununua apartments za ghorofa mbili au hata zaidi na kuzipangisha. Ni biashara yenye faida kubwa sana hasa ukibahatika kupata maeneo yaliyo jirani na vyuoni.

Mkuu ni kweli hakuna biashara inayolipa na ni investment ya kudumu kama real estate (nyumba), lakini kucheza huu mchezo vizuri inabidi usitumie pesa zako (invest a lot of your liquid cash) wanasema dawa ya huu mchezo ni OTHERS PEOPLES MONEY.., yaani mfano unachukua mortgage (kama upo ulaya) au kwa bongo unachukua mkopo na unajenga nyumba, unapangisha, kodi za unaopangisha ndio unalipia benki na unalipa riba, baada ya hapo hiyo nyumba ndio unaweka collateral unapata mkopo na unaendelea kujenga hivyo hivyo..., kuliko atumie 200m yake

kama yupo comfortable kuingia kwenye hii biashara asisahau hii cardinal rule ya Real Estate OTHERS PEOPLES MONEY...

Am sure kama anataka kufanya hii ulaya na ana kazi na mshahara anaweza akapata mortgage kwa down payment ndogo sana ila asisahau ule mtikisiko wa uchumi nyumba zilikuwa overvalued lakini wanasema wakati wengine wanauza wewe ndio wakati wa kununua
 
Kwangu mi hiyo fedha ni nyingi sana. Unaweza kufungua shule kama wengi walivyoshauri, hapo si tu utapata faida lakini pia utasaidia kuinua kiwango cha ubora wa elimu nchini.

Kama vipi tukopeshe wenzio. Kusema kweli vijana Tanzania tunaangushwa sana na ukosefu wa mitaji. Utakuwa umefanya la maana sana.

All the best.
 
mimi nakushauri kama unaweza pata dalali mzuri ukanunua mtaa mzima kama manzese ambao unaweza pata na barabara inayotoka. unaweza jenga hoteli ambayo itakulipa kwa haraka sana.
Mkuu Manzese hipi unayonzungumzia ya kununua mtaa mzima kwa 200m:coffee:
 
duh asante sana mkuu this is really helpful man.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…