Anzisha butchery mkuu.
Wewe tafuta frame kwenye juction, palipo busy na penye uhakika wa watu wenye kipato chao.
Lipa kodi ya mwaka au miezi sita.
Tengeneza frame ikae kima zingira ya kuuza nyama, kuku, mbuzi, maini, moyo na utumbo. Hakikisha pia pauze samaki, vitu vyakupikia kama tomato tins, vitunguu, unga, mawese, tomato sauces, chumvi, ndimu, stocks cubes etc etc.
Lisiwe bucha la kuuza tu nyama ya ng'ombe.
Ukisimamia mwenyewe unaweza faida pekee kwa zaidi ya 30,000/- mpaka 40,000/-.
Ukimpa mtu aendeshe kwa siku anatakiwa kukupa 20,000/- mpaka 25,000/-.
Pa kuzingatia:
Kodi labda 80,000 x 6 months= 480,000/-
Matenegenezo 1,500,000/-
Mizani 100,000/-
Vyuma vya kuning'niza nyama 50,000/-
Ndoo 3 + Beseni 3 + Mop + Sabuni + Gogo la kukatia nyama + Squige + Visu = 100,000/-
Freezer 400,000/=
Leseni ya Biashara na TIN na makadirio utayolipa mwanzoni 150,000/-
White coats x 2 = 5,000/-
Mifuko ya nyama = 3,500/-
Na utabakia na hela pia.
Kazi kwako!
p.s.
Usishangae na maoni pumba ya wapuuzi wengine, huwezi jua labda wao ni tegemezi kwa rushwa au wanakuonea wivu tu!
ALL THE BEST!