Nina milioni 3(tsh) nianzishe mradi gani

nakupongeza sana kwa nia na bidii ya kutaka kujikwamua,usikatishwe tamaa na upuuzi wa wanao kubeza
 
Anzisha WAKALA WA M-PESA INALIPA BALAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA::::
 
ongeza mtaji kwenye kilimo kisha utafute tenders za kusupply mchele mashuleni
 
Mkuu i think you need to have your original idea. You will get so many ideas here but no one can impose his idea on you. Try to come up with your own idea, document it has your goal, strategy, market research, description of your product, marketing strategy, an action plan, e.t.c

Then after try to talk to the right people around you or you can still bring it here at Jf. Jf can be one of your network where you can meet people with whom you can share opportunities and information, here people give their best only voluntarily.
 
Sasa, hiyo milioni tatu ndio mtaji wako au? Mi nafikiri hicho kiasi si mtaji, si kwa maana ni kidogo, la-hasha, bali ni kwamba pesa kama pesa, haiwezi kuwa mtaji bali wewe mwenyewe ndio mtaji...

aah! isije nikakuchanganya zaidi...
 
IDEA zote hizi ziko Valid and Bankable . huyu aliyeomba msaada ni mwalimu. hajasema yupo mkoa gani,kwa ideas za mkopo na kuku wa mayai ziko valid kama akiwa mkoani/Dar/wilaya zilizochangamka. ila kama yupo vijijini interior madongo kuinama ,hapo itabadi awekeze ktk shares and partnership.e.g Atafute mtu mwenye biashara aongeze mtaji,yeye awe anapata riba.mfano mzuri ampatie mwenye kampuni ya mikopo,alafu yeye awe anapata 5% ,and mwenye kampuni anachukua 5%.

 
katika watu makini naowajua wewe umo ,naamini unafaa uwe kiongozi ,i appreciate you .your a gentleman and certified to be my close friend .go on vijana wengi hawaja attain hiyo point .good comment ever
 
sijuhi uko location gani, maana hata huu ushauri unaopewa unaweza usiwe na faida maana shauri nyingi zinalenga mazingira ya miji mikubwa,
jaribu kueleza uko eneo gani, ili ushauri uendane na mazingira uliyopo
 
Mi nadhani hata kama umepata ideas za kutosha,
Ukiweza kama hujajiandaa vya kutosha nunua hisa
Hata hivyo original project yako usiiache maana ndo imekufikisha hapa
Jitahidi kuchukua mawazo ya wanaJF na kisha uchanganye na yako
Naamini utafika pazuri tu.
 
Tumia hii pesa kufanya training au education kwenye chochote unachopenda. Kama haufanyi biashara kajifunze jinsi ya ku manage business popote pale
 
nilikua nina wekeza kidogokidogo pia nililima mpunga na kuuza ndivyo nilivyo pata hiyo fedha.

teacher,,,nakushauri lima vitunguu. Tena hekta 5 zinakutosha. Hekari 1 utapata gunia 80 ukilima kitaalamu na gharama kwa hekari ni sh laki5 . Ukiuza kwa sh 80000 @ *80=6400000. Mara 5 ni forty million with in 6 month.
 
Nimefanya tafiti online ni kweli kabisa kitunguu kina bei nzuri na ukilima HEKTA 1 utapata tani 7-9.ila inahitaji umakini ktk kutunza hilo shamba.kama muda unao na ukizingatia wewe mwalimu unaweza kupata resources at reasonable price
teacher,,,nakushauri lima vitunguu. Tena hekta 5 zinakutosha. Hekari 1 utapata gunia 80 ukilima kitaalamu na gharama kwa hekari ni sh laki5 . Ukiuza kwa sh 80000 @ *80=6400000. Mara 5 ni forty million with in 6 month.
 


Kanyagio umewakuna wengi sana
 
Thats why JF are great thinker japo wengine bogaz, kip it up
 
Ideas nyingi ni nzuri ingawa wengine wanaleta mzaha wakati Mwalimu yuko serious...Mwalimu, nadhan ushaanza kupata mwanga wa nini ufanye na hizo 3m zako. Ukitumia hayo mawazo uliyoambiwa na ukichanganya na yako, utapata best idea. Kila la kheri.
 
Hao wanao jitapa...sijui kuweka heshima Bar ndo wa kuwachukulia pesa zao, siku hizi kila mtu anakunywa beer hata kama bado hajaanza basi kesho kesho kutwa akizishika tu starehe ya kwanza pombe ndo akili ikae sawa...ts a potential business ambayo hutokuwa na hofu ya magonjwa, lishe wala uharibifu wa aina yeyote...katika kila crate moja ya bia unachukua faida sh.8000, siku pamechanganya vizuri mwsho wa mwezi ukadondosha crate zako zaid ya 10 una cha juu kama 100,000/=...kama haupo village(maana huko ni ulanzi) tafuta tu eneo linalokalika watu wakanywa na kustorisha..sio lazima iwe nyumba hata eneo la wazi tu ukawawekea tulubai na meza zako kumi na crate kadhaa za kuanzia wanywaji watakuja tu, usisahau kuweka soda kwa ajili ya watoto!...ubunifu na akili ya sales ukiwa navyo MIL.3 inatoshaa
 
nunua bodaboda mbili nina uhakika kila moja lina uwezo wa kukuingizia 45000/wk mara mbili mara nne ni 180000 kwa mwez mara 12 ni mil 2160000
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…