Mkuu, mimi nilifungua duka la spare kwa mtaji wa 15m miaka miwili iliopita. Sasa hivi nina mtaji approximately 80m na turn over kwa mwezi btn 12-15m. Ila naomba nikufahamishe magari na spares nazijua vizuri sana ila biashara nimejifunza baada ya ku fail kwenye biashara kadhaa.
Inahitaji nidhamu ya hali ya juu,kila hela unayoipata unairudisha kukuza mtaji,bado nafanya hivyo. Tatizo watz wengi wakifanya biashara tu wanaanza kujenga,kununua magari ndio maana biashara hazikui.
Uwe na malengo,usikate tamaa na nidhamu ya hali ya juu.