Nina mpango wa kuhamia Morogoro kwa nia ya kutafuta maisha

Binafsi nataka niamie Moro kibiashara hvyo embu tangulia ukifikaa tujulishane
 
Sema hata kukusanya mchele siku hiz haupandi km zaman..hukuti sasa hv mchele wa 2300 sokoni..unajikuta unahangaikia sh 200@! unajua hata km una 5m kama huna akili ya kujiongeza unaweza jikuta inaishia tu...shida inakuja hapo...!
Unakwama wapi kutoa wazo mbadala mkuu ?
 
Mkuu,, nikushaur tu kwa morogoro mjini kuanza maisha itakua ishu kwa hiyo hela coz mimi nimekulia hapo napajua vizur Sana,,, ila Kuna sehemu inaitwa ifakara, kule maisha very cheap unaweza kuanza maisha bila shida na kilimo utafanya,, maoni yangu tu,,
 
Nimemchagulia malinyi sababu ni wilaya mpya, viwanja bado cheap sana, maisha ni cheap sana japokua ni sawa na mngeta lakini faida ya malinyi ni wilaya mpya..akinunua ardhi sehem ambayo nguzo za umeme hazipo mbali sana bei around 400,000 hadi 700,000.....trust me baada ya miaka miwili atakua yuko vzr....

Kukodi mashamba ndo usiseme ya kumwaga.....
Pesa aliyonayo kwa malinyi hatojuta
Yeye anataka Mngeta! Napo ni pazuri sana tu. Akipata mtaji asisahau kuanzisha biashara pale Mchombe!
 
Hujakosea, Karibu Mji kasoro bahari. Kutokana na standard zako ulizo orodhesha ziko makini. Maeneo ambayo utaweza kupanga kwa unafuu mzuri na ukaribu wa mjini ni Mkundi, Kihonda na Nane Nane. Kuhusu maswala ya kilimo ni kweli haswaa tena unaweza kuaanza kujifunza biashara ya kuuza mazao ya vyakula kwa jumla kama maharage, mchele, dagaa, vitunguu n.k. Ni vyema ukiaanza biashara rasmi utege ofisi yako maeneo ya mjini "centre" au karibu na soko kuu.
 
Sawa benKaile,,, na mpango wangu mkubwa ni kuja kufanya biashara za mazao huko morogoro
 
Nashkuru nimeliweka akilini wazo lako na ntalifanyia kazi
 
Ndio naelekea huko mwez unaokuja na nakuahidi nitaleta mrejesho kaka
Anza na kununua mchele kisha peleka kwenye masoko kama dar,dom na kwingineko au nunua mpunga na baadae kuuza

kama ni kilimo cha hiyo ekari moja hakikisha ni cha umwagiliaji
 
Maisha ya hapo mngeta unayaonaje?? Hamna ndumba za ajabuajabu?
 
Mngeta ni town mkuu?? Naomba nieleweshwe tu coz m ndio mgeni wenu mtarajiwa?
 
Kwa mtaji alionao biashara ya kununua mchele ni ngumu
Anza na kununua mchele kisha peleka kwenye masoko kama dar,dom na kwingineko au nunua mpunga na baadae kuuza

kama ni kilimo cha hiyo ekari moja hakikisha ni cha umwagiliaji
 
Ningekua mimi na huo mtaji mchanganuo wangu ungekua hv

Iwe mngeta au Malinyi

Nauli:= 100,000
Nikifika gest:= 20,000(siku mbili)
Chumba cha kupanga 7000×6= 42,000
Nikifika nanunua gunia 15 za mpunga debe nane naweka mashineni: debe 8000= 64000×15= 960,000
Pesa ya mtafutaji mpunga roba 15:= 30,000
JUMLA KUU: 1,122,000
Chench inabaki kama m1 hv.

Mengine yatafata badae mf. Kukodi shamba nk.

Kumbuka swala la kula kule akinunua roba moja mpunga 64,000 unakula mchele mwaka mzima, kuni zipo kiberiti sh 100, maji yapo ya kumwaga

All the best hii plan inahitaji action sio kuomba ushauri ni kusacrifice tu
 
Mm nikushauri kwamba Niliwahi kaa wilaya ya imalinyi kule biashara wakat wa mavuno iko vizur sema kwako mgeni inaweza kuwa changamoto koz hujui maeneo yake kulingana na umbali na njia zenyewe
Lkn ukienda na biashara ya viatu hasa vya akina mama utauza sana miezi hii
Hilo mm nililiona
 
Maisha ya hapo mngeta unayaonaje?? Hamna ndumba za ajabuajabu?

Hizo stori kwa Mngeta sidhani kama zipo. Jamii nyingi za watanzania kwa sasa zime elimika hivyo hisia za ushirikina zimepungua kama siyo kuisha kabisa. Muhimu ni kujichanganya tu na jamii na pia kufuata taratibu zikiwemo za kutoa taarifa zako kwenye serikali ya kijiji ili utambulike.
 
Nmekuelewa sana mkuu ni mchanganuo mzuri yaliyobaki yote ntajiongeza mwenyewe ikiwemo kukoboa ili niuze mchele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…