Nina mpango wa kuhamia Morogoro kwa nia ya kutafuta maisha

Yani badala ulime kitunguu huko ambacho kikitiki umeula unataka ukalime mpunga mbona unajichelewesha
 
Mkuu nimekusoma vizuri na asante kwa wazo lako
Yani badala ulime kitunguu huko ambacho kikitiki umeula unataka ukalime mpunga mbona unajichelewesha
Naomba urejee andiko langu la awali,,, cjasema naenda kulima mpunga,, ila naenda kua middle men wakununua mpunga, kukoboa na kuuza mchele
 
Mzee baba kama unataka kuanza maisha Moro usiende town, hakuna mzunguko wa pesa hakuna kazi za kuajiriwa nakushauri uende vijijini huko kama dumila, mgeta matombo, mvomero, kisaki na mkuyuni na ukifika huko fanya biashara ya kununua mazao usilime utafeli mjomba, ama fungua hata banda la kunesha mpira..kilimo kwa mtaji ulionao ni oesa ndogo, moro kutafta pesa kwa njia za halali ni mtihani mzee baba nimekaa hapo si chini ya miaka sita napafaham vizur na maraia wa hapo hawapendi watu watoboe, kama wewe ni mtu wa kaskazini tafta watu waliotokea pande hizo watakupa mwanga kwa maana wanaushirikiano sana na hawawezi kukupoteza lakini wenyeji si watu poa kwa kukushauri wengi wanapenda kuona unaanguka ama unakuwa kama wao.
 
Ni kweli kabisa,hasa ukikuta sehemu ina wazigua wengi ni mtihani sana
 
Nimekuelewa sana mkuu na nashkuru kwa ushauri wako,,, nimepanga kwenda mgeta
 
Morogoro ni kubwa jipe muda wa kufanya research unataka kulima nini na morogoro sehemu gani inafaa kwa kilimo unachotaka binafsi nipo morogoro ila eneo nililopo kilimo sio kihivyo ila hapa ufugaji nikama wote.... Fanya utafiti morogoro kubwa mno kuna sehemu nauli ni zaidi ya 20k kutokea morogoro mjini...
 
Unapatika morogoro wilaya gan mkuu, location yako hasa yan kwanzia kitongoji mpaka wilaya
 
Hiyo kwa mkoa kama mbeya unapiga hela nenda mbeya .
 

We kweli kilombero uliitembea, kuanzia ifakara adi mlimba pako vizur kwa kilimo ndo maaneo yangu ya kutafuta tonge
 
Tunasoma kimya kimya na kufatilia kwa ukaribu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…