Tajiri wa matajiri
Senior Member
- Apr 17, 2024
- 166
- 649
Niko kwenye mahusiano na huyu Binti ana miaka 28, huu ni mwaka 3. Nampenda sana na tulishapanga mipango mingi, shida nikuwa hivi karibuni kabadilika sana na sioni kama nawezana naye.
Kwanza amekua mtu wa kisirani, kakitu kadogo ataongea mpaka inaboa, ukichelewa kupokea simu hata kama ulikua na kazi atalalamika mpaka basi.
Mbaya ziadi nikuwa anapenda kusema tuachane, sijui kama umenichoka bora kuniacha, huna mipango na mimi, yaani ni kulalamika kiasi kwamba nakosa amani.
Nilimuahidi ndoa, na nina mipango hiyo, ila naona sitaweza, kitu kidogo atawapigia rafiki zangu kulalamika, amekua ni mtu wa kunipangia maisha, sitaki uongee na flani, sitaki hiki sitaki kile.
Kuna wakati sitaki hata kuonana naye kwani nikikaa naye kidogo lazima tutagombana. Kila dakika anazungumzia ndoa na nikimuambia mipango bado atanuna mpaka nahisi ana mtu mwingine ananifanyia vituko ili nimuache aendelee naye.
JIBU LANGU; sidhani kama ana mtu mwingine, ana miaka 28, mmekaa kwenye mahusiano miaka 3. Umemuahdii vitu vingi ila anaona kama hutekelezi.
Wanawake katika umri huo wanaanza kupaniki, unakuta rafiki zake wote wameolewa, Mama yake anampigia kelele kuhusu ndoa. Lakini pia kuna mjinga flani huko alimdanganya kuwa unatakiwa kuzaa kabla ya kufikisha miaka 30.
Basi anajikuta anapaniki na kushindwa kuzuia hisia zake. Kama hujamfumania, hakudharau, ila ana kisirani, najua kinaboa ila shida kubwa ni kwakua anaona kama hueleweki, akikuambia kuhusu ndoa humuambii mambo ya kueleweka.
Una mipango yako sawa, ila kama unataka muwe na amani muambie. Mkalishe chini, muambie sikiliza, mimi nakupenda, lakini kwasasa nataka nifanye 1, 2, na 3. Baada ya hapo nitakuja kwenu.
Sasa kama haya mambo yasipokaa sawa basi mwezi flani au baada ya miezi 6, tuanze mipango ya kuoana. Kuwa muwazi, ajue kitu kinachoendelea kichwani kwako, wanaume tuna kawaida ya kuwekea mambo vichwani.
Una mipango mizuri na yeye lakini humuambii, unataka yeye aote. Anachokiona yeye ni hueleweki kwakua unamkwepa kuongea na yeye! Inawezekana kuna mwanaume anamtongoza na kama hutakua muwazi atamkubalia kwakua anahisi unamdanganya.
Mmekaa miaka mitatu, hueleweki, anaona umri unaenda, halafu kuna jamaa tena anamdanganya yeye anakuja na ndoa mkononi, atakubali na wewe utampoteza mwanamke mzuri kwakua tu hujaamua kuwa muwazi!
MREJESHO; nilikutafuta mwaka jana kwakua mambo yangu yalikua yamesimama, kuna dada nilikua nampenda ila alikua ananisumbua kisirani kingi. Uliniambia niwe muwazi kwake, nimuambie malengo yangu ili iwe rahisi yeye kunielewa, Kwamba hata kama anasubiri ajue anasubiri nini.
Nashukuru sana, niliamua kuongea na mpenzi wangu, nilimuambia kuhusu hali ya nyumbani kwetu kuwa kwasasa namalizia kujenga nyumbani kwakua najua jinsi wazazi wangu walivyo, kama nikioa bila kujenga watanisumbua sana na nitashindwa kufurahia ndoa.
Nilimuambia asiwe na wasiwasi, alikua anashida sana na simu yangu kwakua nilikua sichepuki nilimpa uhuru. Alianza kunielewa na mimi nilibadilika, nikawa hata kama sijapokea simu nitamtumia meseji kumuambia niko bize kidogo baadaye namcheki.
Nashukuru nina amani sana nayeye, tunakaa tunapanga mambo, kelele zimepungua, ingawa bado anauliza ila kwakua nimekua muwazi basi ananielewa. Nimemaliza kujenga nyumbani sasa ndiyo wananilazimishia kuoa na Mwezi ujao naenda kutoa mahari.
Kutokana na kipato tunafunga ndoa ya watu wachache msikitini tu mambo mengine yatakuja baadaye, ameridhika na anafuraha kwakua nimekua muwazi sana kwake. Kusema kweli nashukuru kwani imeniondolea mzigo mkubwa, sasa hivi naweza kuongea kitu akanielewa.