Nina mpango wa kuuza mali zangu baadhi nijikite kwenye Biashara

kwa kweli kuuza mali sija penda hata kidogo japo mtu anajisaidia kwa kile alichonacho nachokushauri achana na mali hizo, anza maisha upya tafuta vibarua vya nje ya taaluma yako mbona utapata mtaji tu hata ulinzi piga tu.ni jambo la kuogofya zaidi unauza mali zako zote afu unawekeza kwenye biashara baadaye biashara inakufa au kufirisika japo hatuombei litokee ,nachoshauri anza maisha upya,hizo mali achana nazo maana ukiziuza ukaweka kwenye biashara na biashara hizo baadaye zikafirisika itakuathiri sana kisaikolojia
 
kwa kweli kuuza mali sija penda hata kidogo japo mtu anajisaidia kwa kile alichonacho nachokushauri achana na mali hizo, anza maisha upya tafuta vibarua vya nje ya taaluma yako mbona utapata mtaji tu hata ulinzi piga tu.ni jambo la kuogofya zaidi unauza mali zako zote afu unawekeza kwenye biashara baadaye biashara inakufa au kufirisika japo hatuombei litokee ,nachoshauri anza maisha upya,hizo mali achana nazo maana ukiziuza ukaweka kwenye biashara na biashara hizo baadaye zikafirisika itakuathiri sana kisaikolojia
 
Ingekuwa unauza ili kukuza biashara ingekuwa vinzuri San

Ila kuuza ili kuazisha biashara hiyo ni risk japo biashara inaitaji risk taker hiyo haipingiki ndio kanun ya biashara.

Nchi yetu imekuwa ngumu San hasa Kwa mtu unayeaza biashara kutokana na ukiritimba mwingi.
 
Biashara sio option ya kufeli Mamb mengine uko... nakushauri endelea kutafuta ajira ww, biashara sio mahala kwako..
Mkuu usinichukulie Poa. Hapa napambana kweli kweli hata hicho kiwanja nilikinunua sababu ya biashara.
Nakopesha Kama wewe sema tu mambo yanaingiliana
 
Mkuu jaribu kuusikiliza moyo wako,achana na mtu anayekuogopesha kuwa ukiuza kiwanja utajuta,kwani ulizaliwa na kiwanja!? Vyote ni vyakutafuta,na mtu husaidiwa na chake,Mimi mwezi wa pili nimeuza nyumba yangu niliyoijenga kwa damu na jasho na Leo hii maisha yanasonga,

Katika kufanya maamuzi huwa kuna sauti inakuja ile ya kwanza kutoka kwa nafsi yako hiyo ndo unapaswa kuisikiliza.

Wote wanaokushauri usiuze kiwanja hawna msaada na wewe,hebu mfuate hata mmoja umwambie akupe hata laki tano kwa mkopo uone kama atakupa.

Fuata hisia zako,hakika utafanikiwa
 
Ujue hapa ata watu wakushauri nn unaweza usifuate maana kuna jambo tayari umeamua. Usikilize moyo wako unasema nini.
 
Naomba hiyo connection ndugu
Kuliko kuuza si Bora ukatafute vibarua tuu? Kuna kazi za ujenzi Kwa wakandarasi unapata walau 400k Kwa mwezi kama kibarua na nssf unalipiwa.

Kikubwa connection tu.
 
Una umri wa miaka mingapi kwanza kabla ya kukupa ushauri?
 
Naelewa mkuu umuhimu wa ardhi ila sina namna.

Nimejaribu kuongea na Madoni wa ukoo wanisapot ila nimetolewa Nje.

Sasa nashindwa nifanyeje, nahitaji kufanya Biashara na kuendelea na maisha mengine.
Brother kiwanja usiuze, utatukumbuka yaan teseka unavyoteseka kiwanja usiuze zuia hivyo hivyo kubari kula msoto wa kukaa bench na kukosa ajira Ila ukiuza kiwanja umepoteza kila kitu hata hela ya kununua kingine hautopata jifunze kwa waliokutangulia
 
Mpe Kinumbo connection mkuu
Aende site kwenye miradi hususani inayoanza atapata kazi ila kushinda jf bila kutafuta habari za serikali utaishia kusema hakuna kinachoendelea.

Ataje Mkoa alipo nimwambie miradi inayotarajia kuanza Ili awe anajipitisha Kwa washkaji wa huko apate kazi.

Akibahatika atapata ila in most cases lazima anyoshe mkono Kwa recruiters,this is reality.

Mwisho connection Huwa anapewa mtu mnaefahamian sio wa kukutana mtandaoni hiyo haipo maana hata Mimi nimewahi pewa connection na wanaonifahamu Ili kwamba Ukiharibu asije ingia lawamani.
 
Kwa ushauri wangu uza kiwanja then hama hapo katafute maeneo nafuu nunua shamba kwa bei NDOGO then inayobaki fanya biashara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…