Nina mpango wakuzuia TV nyumbani kwangu naona watoto wanaharibika

amarina

Member
Joined
Jan 5, 2025
Posts
69
Reaction score
140
Wakuu za usiku.

Nina TV na madishi ya azam na mengine. TV mbili. Nawaza hapa, enzi zetu hatukuwa na TV hivi sasa watoto wanapoteza muda kwenye katuni na movies. Hii inanipa picha najenga kizazi cha kukaa na kuangalia TV, Watu wavivu, Ombaomba na Maskini. Hii haikubaliki

Naomba kutoa hoja..naomba mniunge mkono au kutoa maoni
 
Acha ukoloni waache watoto waenjoi tuna utoto wao. Enzi zetu tulikuwa tunatembea kilometres za kutosha kwenda kuangalia tv sehemu.

Cha msingi wawekee ratiba maalum ya kuangalia tv baada ya kumaliza majukumu yao uliowapangia eg inaweza kuwa kulima bustani ,kupalilia majani, au kufanya usafi
 
Sawa
 
Waangalie TV kwenye mambo ya maana ambayo watajifundisha,kitu muhimu ni wanaangalia nini kwenye hiyo Tv? wawekee ratiba na uwawekee vipindi ambavyo vitawaelimisha na kuwafurahisha,

Usifananisha maisha ya enzi zako na enzi zao,hii ni Dunia nyingine kabisa,kila zama na kitabu chake.
 
Wakuu za usiku.

Nina TV na madishi ya azam na mengine. TV mbili. Nawaza hapa, enzi zetu hatukuwa na TV hivi sasa watoto wanapoteza muda kwenye katuni na movies. Hii inanipa picha najenga kizazi cha kukaa na kuangalia TV, Watu wavivu, Ombaomba na Maskini. Hii haikubaliki

Naomba kutoa hoja..naomba mniunge mkono au kutoa maoni
Kuwa Mkoloni, waangalie siku za weekend TU, Kuanzia asubuhi mwisho saa 3 usiku baada ya taarifa ya habari

Siku zingine za masomo, Wasome wasiangalie kabisa
 
Wakuu za usiku.

Nina TV na madishi ya azam na mengine. TV mbili. Nawaza hapa, enzi zetu hatukuwa na TV hivi sasa watoto wanapoteza muda kwenye katuni na movies. Hii inanipa picha najenga kizazi cha kukaa na kuangalia TV, Watu wavivu, Ombaomba na Maskini. Hii haikubaliki

Naomba kutoa hoja..naomba mniunge mkono au kutoa maoni
Kuangalia TV sio vibaya Bali weka tu ratiba itakayowasaidia. Ni muhimu pia wakafanya na shughuli ndogo ndogo.
 
Hii ifafanue itaokoa wengi. Kama hutojali mkuu
Pdf yake ni ndefu kidogo ila kanuni ya malezi ni kwamba watoto hawafanyi kile unawaambia wasifanye au wafanye Bali hufanya kile unachofanya
Wakiume hufanya kama baba yake na WA kike hufanya kama mama yake kuanzia wakati wa kuamka hadi wakati wa kulala
Sikiliza "coward of the county"wa Ken Rogers utaelewa vizuri zaidi ni SoMo la malezi nami sio mzuri sana wa kuandika
 
Wakuu za usiku.

Nina TV na madishi ya azam na mengine. TV mbili. Nawaza hapa, enzi zetu hatukuwa na TV hivi sasa watoto wanapoteza muda kwenye katuni na movies. Hii inanipa picha najenga kizazi cha kukaa na kuangalia TV, Watu wavivu, Ombaomba na Maskini. Hii haikubaliki

Naomba kutoa hoja..naomba mniunge mkono au kutoa maoni
Vipi smartphone na platforms kama jamiiforums zilikuwepo? Huoni wewe kuendelea kutumia smartphones na jamiiforums kunakufanya kuwa mvivu, ombamba na masikini huenda sasa ungekuwa kama dangote kama ungetupa hiyo smartphone ukaachana na matumizi ya internet
 
Imeleweka. Asante
 
Ni kweli hili nalo neno, wanakuona kila mara ukiwa unashika simu. Sasa tutafanya nini.

Najutahidi mara kwa mara nisime vitabu. Na kuwaonyesha umuhim wake.
 
Acha ukoloni waache watoto waenjoi tuna utoto wao. Enzi zetu tulikuwa tunatembea kilometres za kutosha kwenda kuangalia tv sehemu.

Cha msingi wawekee ratiba maalum ya kuangalia tv baada ya kumaliza majukumu yao uliowapangia eg inaweza kuwa kulima bustani ,kupalilia majani, au kufanya usafi
uzi ufungwe hapa
 
Usilikimbie tatizo, Face changamoto na tafuta njia sahihi ya kuitatua..
Kuzuia matumizi ya TV si sahihi hata kidogo. Malezi ya watoto ni mapana Sana ingawa uangaliaji wa tv kwa sasa unachangia kuharibu maadili ya vijana wetu.
Beba wote peleka shule za bweni
 
Ni kweli hili nalo neno, wanakuona kila mara ukiwa unashika simu. Sasa tutafanya nini.

Najutahidi mara kwa mara nisime vitabu. Na kuwaonyesha umuhim wake.
Mkuu ni kuwawekea tu ratiba maana huwezi kushindana na teknolojia mwisho wa siku itashinda. Hata kabla ya zama zako kulikuwa na zama za wa kabla yako nao hawakuwa na vitu ulivyokuwa navyo wewe huenda na wao walikuwa wanakuona wewe mvivu.
Just wawekee muda tu na ratiba. Teknolojia si mbaya ikitumika ipasavyo. Kwa mfano mimi nina kiajana mtoto wa dadangu ana miaka 10 nishaanza kumfundisha programming. Nishaanza kumfundisha namna ya kutumia Chatbots kuandika vitu, kuuliza maswali, kupata ufafanuzi. Hopeful mpaka anakuja kufika labda form two atakuwa ana uelewa mkubwa na huenda atakuwa tayari ana uwezo wa kuandika viprogamu fulani fulani.
 
Wakuu za usiku.

Nina TV na madishi ya azam na mengine. TV mbili. Nawaza hapa, enzi zetu hatukuwa na TV hivi sasa watoto wanapoteza muda kwenye katuni na movies. Hii inanipa picha najenga kizazi cha kukaa na kuangalia TV, Watu wavivu, Ombaomba na Maskini. Hii haikubaliki

Naomba kutoa hoja..naomba mniunge mkono au kutoa maoni
Uko Sahihi kabisa, kuna kipindi sikulipa king'amuzi kwa makusudi, nikagundua kuwa saa mbili usiku watoto walikua wameshaoga, wameshakula, wamefanya homeworks na saa TATU WAKO kitandani.

Sasa ukilipia Tu, utarudi saa tatu home HAKUNA cha maana Ndio Kwanza wanakula..... UKo Sahihi. Mimi kipindi cha mitihani silipi
 
Back
Top Bottom