Nina mtaji mil 5 nifanye biashara gani?

Latoya

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2013
Posts
660
Reaction score
457
Habari wanabodi

Nina mtaji wa mil 5 naomben mawazo ya biashara ya kufanya.

Binafsi nawaza kufungua ofisi ya masuala nilosomea na ninayofanyia kazi, (professional office) then niweke na mpesa,tigopesa plus stationary sehemu moja.

Kwani ndoto yangu ni kujiajiri kwa professional yangu nikikaa sawa niquit serikalini na kuwa na big office in near future.

Naomba msaada wa mawazo wadau.
 
anza hivohivo utatoboa
 
Kwangu mimi biashara ya mazao ni bora zaidi hasa mchele na maharage, unatafuta soko kwanza unaenda huko kwa wakulima unanunua mazao yako unapeleka sokoni baada ya mwaka utakuwa mbali sana.

Kuna biashara ya kusambaza bidhaa madukani hasa maduka yaliyo pembeni ya mjini, hapa unaweza kutafuta kijana akawa anakusaidia kusambaza bidhaa zako madukani kwa kutumia pikipiki.

Azisha ufugaji wa kuku wa kienyeji.

Kwa pesa hiyo unaweza anzisha mgahawa mzuri, ukatafuta wapishi wazuri na ukazingatia usafi huku chakula chako ukiuza kwa bei ndogo.

Kwa hela hiyo unaweza fanya biashara ya mitumba ya jumla, unafuata mzigo Kenya (wanachukua nguo zao Korea miili yetu na yao inaendana) ukawa unawauzia wale wanaouza kwa reja reja.

Kwa pesa hiyo unaweza kutafuta eneo lenye rutuba nzuri na mvua za kutosha ukaiwekeza kwenye kilimo hutajutia.

Kuna biashara ya mifugo mfano mbuzi na ng'ombe unanunua eneo moja unaenda kuuza eneo jingine mfano toka huko usukumani unaleta Dar au Dodoma

Are you there.
 
Thanks mkuu. Maelezo zaidi kuhusu hyo biashara ya nguo huko Nairobi
 
Thanks mkuu. Maelezo zaidi kuhusu hyo biashara ya nguo huko Nairobi
I am,hayo yote unayosema nishayasikia but nimeamua kufanya hivi ili baada ya like 3 to 4 years niache kazi
Wananibana sana kazini
Seenjoi kazi yangu
Halafu bonge la performer

Nataka niondoke govt nijitawale
Ishu za plots na nini nina access
Bt i want to run

Boss wangu ana roho mbaya sana afu nimemzid uwezo ingawa ananizid umri so anatumia kila mbinu kunikwamisha,simdharau wala nn sema anajistukia

Ananibana sana,najitahid sana kupiga kazi ila anaona kama nashindana naye
Nilikuwa na ndoto za kustaafia govt but kwa huyu jamaa naona atanikwamisha mipango yangu mingi

Nataka nitoke then ujuzi wangu niutumie mtaani kujijenga,najua baada ya 5 years watanitafuta tu waniajiri but no
Nataka toa ajira kwa vijana wenzangu
 
never lose this fire, good luck.
 
never lose this fire, good luck.
Thanks man nimekuwa na hii ndoto since nasoma chuo, niliwaza nigrafuate niajiriwe govt then after some years niwe somebody in this country ili niibadil industry niliyomo

But naona kadri siku zinavyoenda naumia,am not happy at all,nina kazi,usafiri,makazi but I always feel the gap inside

Nimekuwa nalia mara kibao mwenyewe and ask my God kwann ukaniweka hapa ?kwa watu hawa?nilikosea wapi?
Mwishoni nilimkumbuka mwalimu wangu wa entrepreneurship ingawa haikuwa core subject aliwahi sema usichukulie problems kama obstacle hali oportunities

Nimeamua na nitafanya,inshallah nitarudi toa mrejesho humu,may be niliwekwa kwenye situation hii ili niact na niwanyanyue na wengine

Nisiongee sana but nimeamua and am going to do it

May be its about time.
 
Usitoke gvt kwa ajili ya huyo boss toka gvt kwa ajili ya kufuata na kutekeleza ndoto zako maana huyo boss leo yupo kesho unaweza kuwa wewe au mwingine, usimuogope boss bali fuata ndoto zako na uzitekeleze naamini utafanikiwa.
 

Mie kwenye nguo Kenya kufuata takuuliza vema mkuu
 
Sorry mkuu naomba unipe mwangaza kwenye hyo biashara ya kusambaza bidhaa kwa pikpik kwenye maduka yaliyo pembezoni ntaman kuifanya sijajua wapi pakuanzia
 
Ninao uzoefu wa biashara ya mbao...
1. Unanunua iringa vijijini kwa bei ndogo then unasafirisha kwenda mikoa mingine kwenye uhitaji wa mbao (sio nyanda za juu kusini). Unauza jumla km mtaji unaruhusu (around 12 to 14M) faida ni kubwa sana, min ni 3M.
2. Unaweza kufungua kijiwe pembezoni mwa mji (kunakoendelea kujengwa) then unanunua mzigo wa jumla (mbao) say mzigo wa 3M then unauza rejareja. 2M inayobaki tafuta mashine ya kupiga tofali, mchanga, cement, tank la maji, nk. Ukaweka vijana wanapiga tofali na kuuza+mbao pembeni hakika itakulipa tu.
3. Msimu wa kuvuna huu huko moro mchele haujapanda sana bei, tafuta soko huko manzese nk then unafanya simple survey ya bei ya mkoani ili uwe na uhakika. Ukishajiridhisha unaenda kuchukua mchele na kuuleta town. Binam yangu anafanya hz mishe kila mwez lzm alete gari 1 au 2 dsm... inamlipa kwa kweli.
4. Fungua duka la madawa hasa pemben ya mji hakika utauza vzr. Pawe mbali kidogo na dispensary. Utahitaji documents chache sana hata za kukodi tu kwa watu ambao tayari wako na hizo biashara.
5.. zipo nyingi tu mkuu japo kuna wadau wazoefu zaidi wanakuja isee
 
hello naomba nku DM kwa more information please....
 
forex
 
pambana na huyo bosi wako wewe mpaka kieleweke
 
Kamata machine ya kusaga karanga 2mil vifungashio vya kuanzia pamoja na labels na vitu vidogo vidogo 1.5ml, malighafi 500k hiyo 1m itakua standby kwa chochote pungufu, unaanzisha Kiwanda Cha peanut butter
 
Sasa unaacha kazi kwa ajili ya boss daah. Think twice Mkuu. Acha kwakua una ndoto zako ila sio kwa ajili ya boss mzushi. Serikali haina boss permanent huyo anytime anahamishwa or anaondoka so komaa mkuu.

Biashara unaweza kufanya na bado ukabaki kazini tafuta watu sahihi tu kwa sababu hata ukiamua kuacha kazi bado utahitaji kuajiri watu ufanye nao hiyo kazi yako. sasa kwa nini usiwajiri then ukaendelea kubaki serikalini huku ukisoma upepo wa biashara yako.
Ni ushauri tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…