Nina mtaji wa milioni 1 naombeni kufahamishwa biashara ya kufanya

Nina mtaji wa milioni 1 naombeni kufahamishwa biashara ya kufanya

dks1131

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Posts
225
Reaction score
161
Wale mnaoishi Kahama na viunga vyake naombeni msaada wa maoni yenu, nina mtaji wa milioni 1 naombeni kufahamishwa biashara ya kufanya ili na mimi niweze kuishi mjini vizuri. Natanguliza shukrani
 
Nunua mazao then yauze kwa faida,utarudi kunishukuru.
 
Hivi huwa inaanaza wazo ndo mtaji unafuata au unaanza mtaji kwanza
 
Wale mnaoishi Kahama na viunga vyake naombeni msaada wa maoni yenu, nina mtaji wa milioni 1 naombeni kufahamishwa biashara ya kufanya ili na mimi niweze kuishi mjini vizuri. Natanguliza shukrani
Inawezekana vipi una hela halafu hujui cha kuifanyia! Pitia hili jukwaa kwa umakini, angalia mawazo ya biashara mbalimbali ya wenzako; halafu chukua wazo la ile biashara inayoendana na mazingira uliyopo.

Ukitaka kufanikiwa kirahisi kwenye biashara, angalia fursa inayo kuzunguka! Fursa ni sawa tu na matatizo yaliyo izunguka jamii yako. Halafu biashara yako igeuke sasa na kuwa suluhisho la yale matatizo!

Lakini haya mambo ya kutaka kusaidiwa wazo, kana kwamba tulisaidiana pia kwenye kuipata hiyo milioni 1, kiukweli yanaumiza sana kichwa.
 
Hela ndogo sana hiyo haitoshi hata kidogo.

Hapo bado kulipia fremu bado matengenezo.

Jitahidi ifike angalau milioni 5 uje tukushauri nini cha kufanya.
 
Nenda kwenye mji au Jiji lililo jirani na wewe,ingia kwenye maduka ya jumla,nunua Perfume za kike za bei ya kati na sabuni za kuogea,nunua na begi moja la mgongoni ambalo ni imara,anza kutembeza hizo bidhaa kwenye nyumba wanazoishi watu na maofisini,hakikisha unavaa nguo nadhifu usiwe rafu,halafu usikopeshe fanya biashara ya cash sababu huo mtaji ni mdogo,baada ya mwezi mmoja rudi na mrejesho wako hapa kwenye hili jukwaa.
 
Back
Top Bottom