Nina mtaji wa milioni 1 naombeni kufahamishwa biashara ya kufanya

Nina mtaji wa milioni 1 naombeni kufahamishwa biashara ya kufanya

Nikopeshee Mimi kwa mwaka kila mwezi ntakuwa nakupa elfu 80 kama interest
 
Hivi huwa inaanaza wazo ndo mtaji unafuata au unaanza mtaji kwanza
Wazo kwanza mtaji baadae.
Mtu asiye na pesa lakini ana Ideas za nini cha kufanya, aanzie wapi na afanye vipi mpaka afikie hatua fulani ana uwezekano mkubwa wa kufanikiwa kuliko mwenye pesa lakini asijue azifanyie nini na aanzie wapi.

Wa pili ni kama kipofu mwenye gari anayekwenda njia asiyoijua na hajui anaelekea wapi na wakwanza ni mtu anayeijua njia vyema na anajua anaelekea wapi lakini kibaya yeye ni kiwete!.
 
Million 1 sipesa ndogo kwenye biashara Bali unatakiwa hapa ni kufanya biashara ww unayoweza maana kila biashara iliyo kufa Kuna watu wamefanikiwa sas ndg mtoa mada Kuna vitu unapaswa kufikili kabda ujaingia kwenye biashara moja ya ivyo vitu.
1 usifanye biashara kwa 7bu Kuna mtu kafanikiwa uwezi juwa kapita njia gani mpaka yeye kafanikiwa kinacho itajika hapa tafuta biashara inayo lingana na mtaji wako Kisha tathimini zijue changamoto zake masoko yake wapi kwa kupata Kisha fanya utafanikiwa Sana

2 unapofanya biashara usimwangalie mtu wew fanya biashara yako kwa umakini utafanikiwa

Nimeshindwa kukupa full mipango nikipata nafasi nitakupa Tena michongo mim nipo kahama najiusisha mazao Kama alizet karanga nk
 
Back
Top Bottom