Nina mtaji wa milioni 10, spea za pikipiki ni sahihi?

Pipidarling

Member
Joined
Jul 19, 2016
Posts
29
Reaction score
12
Nambeni ushari, na uzoefu wenu spea za pikipiki zinalipa? Na changamoto ya hii biashara ni ipi na natakiwa kufanya nini ili nitoboe location Arusha.
 
Nambeni ushari, Na uzoefu wenu spea za pikipiki zinalipa? Na changamoto ya hii biashara ni ipi na natakiwa kufanya nini ili nitoboe location Arusha.
Zinalipa mkuu ila weka nusu ya hiyo pesa ndo uanze kama mtaji na wewe ndio uwepo kwenye duka au wife wako.

Zingine wekeza kwenye biashara nyingine ambayo haitakulazimu wewe usimamizi wako.

Zipo biashara nyingi tu hapa Arusha, tuwasiliane Kwa mawazo zaidi na ushauri zaidi. (Nipo Arusha pia)
 
Ikiwa wewe ni fundi wa pikipiki au unaye mtu ambaye ni fundi mzuri asiyekuwa na longolongo, basi utafanikiwa.

Ikiwa hakuna chochote kati ya nilivyosema hapo juu, kuna asilimia kibwa sana za kufeli.
 
Biashara inalipa ila weka bidhaa zinazotoka tu iwapo utaweka kila kitu mwisho wa siku kuna vitu hautauza
Kwa ushauri mimi naona uuze oil za Aina zote kubwa na ndogo, matairi ya bei kubwa, maji ya batteries, hydrolic oil na kama mtaji utabaki batteries basi
 
Duka ufungue sehém ambayo pikipik zinatengenezwa... Duka ulisimamie mwenyew... Ujue aina za spea zinatoka mara kwa mara... Million 10 nyingi sana, unaweza toa million 3.5 ukaanzisha hapohapo na huduma ya Pesa kwa mitandao ya cm...
 
Mpuuze huyu, usimtafute anataka kukuibia[emoji23][emoji23]
 
Mkuu Kama unaendesha mwenyewe sawa

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
Hivi ni kwa nini pikipiki mnang'ang'ania kuendesha wenyewe?, Kwa maana hiyo maisha yako yote utazeeka na pikipiki moja tu au ukinunua ya pili napo unakuwa unaziendesha zote mbili?

Huwa ninashangazwa sana na akili ya kusema ukinunua bodaboda lazima uendeshe mwenyewe!, huwa ninadhani ni mawazo ya hovyo sana.
 
Mbadala wake kimawazo ni nini sasa?

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
 
Mambo ya pm ya kazi gani, weka hapa kwa faida ya wengine.
 
Hela ndogo sana hiyo,njoo tuinywee hapa tabata
 
Mbadala wake kimawazo ni nini sasa?

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
Ni kujifunza kutafuta madereva waaminifu na kuwa makini kufuatilia mienendo yao na namna wanavyotunza vyombo vyako.

Huwezi kufanikiwa kimaisha kama utataka kila kazi yako uifanye wewe, ni lazima ujifunze kuweka watu wakusaidie kuzifanya. Kikubwa ni kuwa makini kufuatilia na kusimamia.
 
Upo sahihi bro, lazima tujaribu na ufanisi Wa watu wengine pia.

Sasa Mimi Nina Pikipiki 13 sasa na kila mwezi naweka mpya 2 barabarani, so mnataka hizi Pikipiki zote niendeshe pekeyangu barabarani.

Ukiona kila mwezi naweka Pikipiki 2 barabarani ni kwasababu naweka mambo vzuri na madereva nachagua vzuri na kikubwa zaidi Pikipiki nazifatilia kila baada ya Siku 10 maana zote ni Pikipiki za MKATABA na Dereva anaitunza maana baada ya Miezi 12 ni Mali yake Halali.
 
Nibiadhara inayo lipa Ila inaitaji ubunifu. Nunuwa spaner zako zakutosha. Tafuta mafundi 2au 3 hakikisha ni waziri na kwenye Bei za ufundi wazibiti wasiwe waranguaji.
Weka mtungi wa upepo. Bei zako zisiwe za kifukuza wateja.
 
Hongera sana, mwenye masikio na asikie!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…