Nina mtaji wa milioni 6 nataka nianze biashara ya bodaboda

Nimejichanga nimefanikiwa kupata mtaji wa milion 6, nataka ninunue pikipiki 3 moja yangu na nyingne niwape vijana.

Kama unafahamu changamoto au ushauri tafadhali sema.
Changamoto ni hii best hao unaowapa unawaamini
 
Sikujua hili mm hua naona wamepaki wanapigwa upepo na toyo zao.
Ok ,toyo wanhoo mpya inaenda sh?

Sent from my TECNO-C9 using JamiiForums mobile app
 
Karma at work
 
Nimejichanga nimefanikiwa kupata mtaji wa milion 6, nataka ninunue pikipiki 3 moja yangu na nyingne niwape vijana.

Kama unafahamu changamoto au ushauri tafadhali sema.

Hongera sana mkuu. Kukusanya 6m si jambo dogo.

Kwanza nikuambie kila biashara ina changamoto zake, juhudi yako ndio itakufanya uone matunda ya biashara.

Achana na biashara za bahati nasibu, kama unaishi Dar tafuta boda boda moja tu kwanza halafu njoo nikupe mikate na vitafunwa (mimi ninayo Bakery) then wewe tafuta masoko yako zungusha mzigo masaa manne asubuhi na masaa manne jioni. Kulala na Laki moja kwa siku ni jambo la kawaida.

Nimesema uanze wewe kwanza na ukishazimudi changamoto zake ndio uwanunulie vijana wengine unaowaamini nao wabebe mikate.

Achana na kubeba abiria huko ndiko risk nyingi zilikojificha.


MCHANGANUO KIDOGO TU KUHUSU HILI:

1. Mkate kiwandani utachukua kwa Sh. 690-700 kwa kila mkate (Hii ni ile inayouzwa Sh. 1000-1200 dukani)

2. Utapeleka kwenye maduka na unaweza kuuza kwa Sh. 850-900 kutegemeana na maeneo. (mfano Tabata utauza 900, Temeke utauza 850)

3. Mtu wa dukani atauza Tsh. 1000-1200/=

4. Let say utapata wastani wa Sh. 150 kwa kila mkate mmoja utakaouza.

5. Jiwekee malengo ya kuuza Pc 500 asubuhi na PC 500 jioni. (kwa kuanza unaweza usifikishe lakin ukishalizoea soko hii ni averahe ya maduka 50 tu ya Mangi)

6. Hapo utakuwa na 150*500 =75,000/= per shift. Ukifanya Shift mbili unakuwa Tsh. 150,000/= per day. Tumia 50,000 kujiendesha na 100,000/= ishi nayo kama faida. Utakuja kunishukuru.

7. Kabla ya kufanya maamuzi, tafuta wale jamaa wa pikipiki wanaosambaza mikate ufanye upelelezi utaelewa nimi nasema.

CHANGAMOTO ZAKE

1. Kupata wateja- Hii utaitatua kwa kuanza kazi mapema ili usikute wenzako wamepita

2. Mtaji wa kuanzia - Kununulia mikate (Hii tukiweka terms sawa maweza kuwa nakupa mzigo wa malikauli unaleta pesa ukirudi)

3. Upatikanaji wa Mikate- Lazima uwe na kiwanda cha uhakika ili soko lako likuamini. Hapa unaeza kuja PM tuyajenge nikupe uhakika wa kupata mzigo


Baada ya wewe kufanikiwa unaweza sasa ku-husisha vijana wako wengine mkawa mnakipiga pamoja.

Nakutakia kila la Kheri.
 
Dm Mkuu tuongee kuhusu hili
 
Njoo tuingie mkataba apa iyo ela yote ambayo unayo kisha niambie unataka boda walejeshe sh ngap kwa siku iyo pesa nitakuwa mi nakurejeshea na kwa muda ambao hao boda wangerejesha mkuu namaanisha njoo tuingie mkataba kwenye biashara yangu alafu niwe nakurejeshea izo pesa za pik pik 3 ambazo boda wengekuwa wanakurejeshea kwa siku mi nitakuwa nakurejeshea kaka kama uko serious plz njoo pm usifanye biashara ya kununua pik pik utalia mno broo nakusisitiza tena

Kama uko bize basi njoo tufanye mkataba unipe izo pesa na niwe nakurejeshea marejesho ambayo boda wengekulejeshea kwa siku plz kama uko interested njoo pm tuingie mkataba nitakuwa narejesha izo pesa ambazo hao boda wangekurejeshea per day na kwa duration iyo iyo ambayo ungewapa boda
 
PPi
Nimejichanga nimefanikiwa k Kkupata mtaji wa milion 6, nataka ninunue pikipiki 3 moja yangu na nyingne niwape vijana.

Kama unafahamu changamoto au ushauri tafadhali semaboda
Biashara ya boda inalipa sana sio Siri lakini inabidi upate dereva anayejielewa na anapassion ya iyo KAZI Kuna aina mbili za biashara ya boda Kuna mkataba na Kuna ya kipande.
MKATABA.
IPO Ivi Kwa siku elfu 12 Kwa dar es salaam. Baada ya miezi 12 kijana anachukua pikipiki mnaachana ambapo unakua umepata million 4 laki 3 na ishirini hapo boda boxer mpya million mbili na laki 6 kwaio faida ya million Moja na laki Saba na ishirini.
hii faida yake ni nzuri sana. Na watu wengi hufanya hii.

KIPANDE.
Kwa siku ni elf kumi lakini pikipiki inakua ya kwako mda wote. Na service unafanya wewe Kama za engine oil n.k hii hesabu zake ni million 3 na laki 6. Kwa mwaka. Hapo ukinununua used million 1 na laki 3 au 4 boxer mpya. Kwaio unaweza Kuta ndani ya miaka miwili unakua na boda 2 au 3 Kama ukiwa serious.
CHANGAMOTO.
Ajali nje nje
marejesho kutofika Kwa wakati kutokana na uaminifu.
matumizi mabaya ya chombo dereva uyo.
ila hakuna biashara ambayo Haina changamoto kikubwa ni kupambana.
NO RISK NO GAIN.






Nimejichanga nimefanikiwa kupata mtaji wa milion 6, nataka ninunue pikipiki 3 moja yangu na nyingne niwape vijana.

Kama unafahamu ctafadhWoto au ushauri tafadhali sema.

Nimejichanga nimefanikiwa kupata mtaji wa milion 6, nataka ninunue pikipiki 3 moja yangu na nyingne niwape vijana.

Kama unafahamu changamoto au ushauri tafadhali sema.

Ata ukimpa kijanaa
BIASHARA YA USAFIRISHAJI VYOMBO VYA MOTO INAHITAJI UWE SERIOUS I MEAN SIO KUCHEKA CHEKA. NA INAHITAJI RISKY YA HALI YA JUU.
BODA BODA Inalipa sana ukipata vijana waadilifu na wachapakazi na wenye nidhamu.
Kinachotakiwa kutoka kwako ni consistency bila kukata tamaa na uchapa KAZI. kanuni namba Moja usifanye BIASHARA bila kumuamini mtu. M nakutakia Kila la kheri Mungu akutangulie katika safari Yako ya mafanikio
 
Excellent
Kwa wastani duka hili linahitaji kianzio cha shiringi ngapi
 
Nimejichanga nimefanikiwa kupata mtaji wa milion 6, nataka ninunue pikipiki 3 moja yangu na nyingne niwape vijana.

Kama unafahamu changamoto au ushauri tafadhali sema.
Subira
 

Ndugu unafanya hii bishara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…